Ruka hadi kwenye maudhui
Hadithi zenye maelezo

Aliulizwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuhusu mambo yatakayowaingiza watu peponi kwa wingi, akasema: "Ni uchamungu na tabia njema

عن أبي هريرة رضي الله عنه قال: سُئِلَ رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ عَنْ أَكْثَرِ مَا يُدْخِلُ النَّاسَ الْجَنَّةَ، فَقَالَ: «تَقْوَى اللهِ وَحُسْنُ الْخُلُقِ»، وَسُئِلَ عَنْ أَكْثَرِ مَا يُدْخِلُ النَّاسَ النَّارَ فَقَالَ: «الْفَمُ وَالْفَرْجُ».
Imepokewa kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: "Aliulizwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuhusu mambo yatakayowaingiza watu peponi kwa wingi, akasema: "Ni uchamungu na tabia njema", na akaulizwa kuhusu mambo yatakayowaingiza watu motoni kwa wingi akasema: "Mdomo na utupu".
Imepokelewa na Tirmidhiy, Ibn Majah na AhmadDarajaNi nzuri (Hasan) na ni sahihi
Maelezo

Anabainisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa sababu kubwa zinazowapeleka watu peponi ni mbili: Uchamungu na tabia njema. Uchamungu: Ni mtu kuweka kinga kati yako na adhabu ya Mwenyezi Mungu, nako ni kwa kufanya maamrisho yake na kuyaepuka makatazo yake. Na tabia njema: Inakuwa kwa kukunjua uso na kutenda wema na nakujizuia na kero. Na sababu kubwa zinazowaingiza watu motoni ni mbili nazo ni: Ni ulimi na utupu. ulimi miongoni mwa maasi yake: Ni uongo, kusengenya, kuchonganisha, na mengineyo. Na utupu katika maasi yake: Ni zinaa na kulawiti na mengineyo.

Mafunzo
  1. Kuingia peponi kuna sababu zake ambazo zinaambatana na Mwenyezi Mungu Mtukufu, na miongoni mwake: Ni kumcha yeye, na sababu zinazohusiana na watu, kama: Tabia njema.
  2. Hatari ya ulimi kwa mtu, nakuwa ni katika sababu za kuingia motoni.
  3. Hatari ya matamanio na machafu kwa mwanadamu, nakuwa hayo ni katika sababu kubwa za kuingia motoni.
Marejeo

سنن الترمذي (3/ 536) (2004). سنن ابن ماجه (5/ 318) (4246). مسند أحمد (13/ 287) (7907). توضيح الأحكام من بلوغ المرام، للبسام (7/ 509). منحة العلام في شرح بلوغ المرام، لعبد الله الفوزان (10/ 369). فتح ذي الجلال والإكرام، لابن عثيمين (6/ 453). سبل السلام بشرح بلوغ المرام، للصنعاني (2/ 696).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com
Tabia njema.

Kila hadithi, daraja, maelezo na funzo hapa vinaonyeshwa kama HadeethEnc.com inavyovichapisha, kwa masharti yake ya kuchapisha upya. Daraja halimtaji aliyelitoa. Tafsiri na maelezo ni ya waandishi wake wenyewe, na baadhi hutaja hukumu; wahakiki wa Sabīl hawajavichunguza. Hadithi ya Kiarabu ndiyo matini. Chanzo: HadeethEnc.com