Ruka hadi kwenye maudhui
Hadithi zenye maelezo

Hakika katika wabora wenu ni mtu mwenye tabia njema kuliko wote

عن عبد الله بن عمرو رضي الله عنهما قال: لَمْ يَكُنِ النَّبِيُّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ فَاحِشًا وَلَا مُتَفَحِّشًا، وَكَانَ يَقُولُ: «إِنَّ مِنْ خِيَارِكُمْ أَحْسَنَكُمْ أَخْلَاقًا».
Kutoka kwa Abdallah bin Amri -Radhi za Allah ziwe juu yake na baba yake- amesema: Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- hakuwa na maneo machafu wala mwenye kuyatafuta, na alikuwa akisema: "Hakika katika wabora wenu ni mtu mwenye tabia njema kuliko wote".
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeDarajaSahihi
Maelezo

Haikuwa katika tabia za Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa na maneno machafu, au vitendo vibaya, na hakuwa anayataka hayo wala kuyatafuta kwa makusudi, basi Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- ni mwenye tabia tukufu. Na alikuwa -Rehema na amani ziwe juu yake- akisema: Hakika mbora wenu mbele ya Allah ni mwenye tabia nzuri zaidi kuliko wote, kwa kutenda wema, na kuwa na uso mkunjufu, na kuacha maudhi na kuyavumilia, na kujichanganya pamoja na watu kwa yale mazuri.

Mafunzo
  1. Ni lazima kwa muumini ajiweke mbali na maneno machafu na vitendo vibaya.
  2. Ukamilifu wa tabia za Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-, hayatokei kwake ila matendo mema na maneno mazuri.
  3. Tabia njema ni uwanja wa mashindano, atakayeshinda atakuwa ni muumini bora na mwenye imani iliyokamilika zaidi kuliko wote.
Marejeo

صحيح البخاري (4/ 189) (3559). صحيح مسلم (4/ 1810) (2321). بهجة الناظرين شرح رياض الصالحين، لسليم الهلالي (1/ 672). تطريز رياض الصالحين، لفيصل آل مبارك (ص410).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com
Tabia njema.

Kila hadithi, daraja, maelezo na funzo hapa vinaonyeshwa kama HadeethEnc.com inavyovichapisha, kwa masharti yake ya kuchapisha upya. Daraja halimtaji aliyelitoa. Tafsiri na maelezo ni ya waandishi wake wenyewe, na baadhi hutaja hukumu; wahakiki wa Sabīl hawajavichunguza. Hadithi ya Kiarabu ndiyo matini. Chanzo: HadeethEnc.com