Ruka hadi kwenye maudhui
Hadithi zenye maelezo

Fanyeni mambo kuwa mepesi na wala msiyafanye kuwa magumu, na wapeni watu bishara njema na wala msiwakimbize

عن أنس بن مالك رضي الله عنه عن النبي صلى الله عليه وسلم قال: «يَسِّرُوا وَلَا تُعَسِّرُوا، وَبَشِّرُوا وَلَا تُنَفِّرُوا».
Kutoka kwa Anasi bin Maliki -Radhi za Allah ziwe juu yake- kutoka kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Fanyeni mambo kuwa mepesi na wala msiyafanye kuwa magumu, na wapeni watu bishara njema na wala msiwakimbize".
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeDarajaSahihi
Maelezo

Anaamrisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwafanyia wepesi watu na kutowafanyia ugumu katika mambo yote ya Dunia na Akhera, na hili liwe katika mipaka aliyoihalalisha Mwenyezi Mungu na sheria. Na anahimiza kuwapa bishara kwa kheri, na kutowakimbiza.

Mafunzo
  1. Wajibu wa muumini ni kuwavutia watu kwa Mwenyezi Mungu na kuwahamasisha katika kheri.
  2. Ni wajibu kwa mwenye kuwaita watu kwa Mwenyezi Mungu atazame kwa hekima namna sahihi ya kufikisha ujumbe wa Uislamu kwa watu.
  3. Kutoa habari njema huleta furaha na watu kuelekea na kutulizana kwa mlinganiaji na yale anayowafundisha watu.
  4. Kuwatia ugumu watu husababisha kuwachukiza watu na kuwakimbiza, na kuyatia shaka maneno ya mfikishaji.
  5. Upana wa rehema ya Mwenyezi Mungu kwa waja wake nakuwa Yeye ameridhia kwao dini ya upole na sheria nyepesi.
  6. Wepesi ulioamrishwa ni ule uliokuja katika sheria.
Marejeo

صحيح البخاري (1/ 25) (69). صحيح مسلم (3/ 1358) (1732). شرح صحيح البخاري، لابن بطال (1/ 153). إرشاد الساري لشرح صحيح البخاري، لأبو العباس القسطلاني (1/ 169). بهجة الناظرين شرح رياض الصالحين، لسليم الهلالي (1/ 687).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com
Tabia njema.

Kila hadithi, daraja, maelezo na funzo hapa vinaonyeshwa kama HadeethEnc.com inavyovichapisha, kwa masharti yake ya kuchapisha upya. Daraja halimtaji aliyelitoa. Tafsiri na maelezo ni ya waandishi wake wenyewe, na baadhi hutaja hukumu; wahakiki wa Sabīl hawajavichunguza. Hadithi ya Kiarabu ndiyo matini. Chanzo: HadeethEnc.com