Ruka hadi kwenye maudhui
Hadithi zenye maelezo

Mlisheni mwenye njaa, na mtembeleeni mgonjwa, na mwacheni huru mateka

عَنْ أَبِي مُوسَى الأَشْعَرِيِّ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ عَنِ النَّبِيِّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: «أَطْعِمُوا الجَائِعَ، وَعُودُوا المَرِيضَ، وَفُكُّوا العَانِيَ».
Imepokewa kutoka kwa Abuu Mussa Al-Ash'ary -radhi za Allah ziwe juu yake- kutoka kwa Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Mlisheni mwenye njaa, na mtembeleeni mgonjwa, na mwacheni huru mateka".
Imepokelewa na Al-BukhaariyDarajaSahihi
Maelezo

Amebainisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa katika haki za Muislamu kwa ndugu yake Muislamu ni kumlisha mwenye njaa na kumtembelea mgonjwa, na kumuacha huru mateka.

Mafunzo
  1. Himizo la Waislamu kusaidizana.
  2. Himizo la kumlisha chakula mwenye njaa na uhitaji, huyu imeamrishwa kumlisha.
  3. Sheria ya kumtembelea mgonjwa; ili kumpa faraja, na kumuombea dua na kupata malipo, na mengineyo.
  4. Kufanya pupa kumwacha huru mateka aliyetekwa na makafiri, na hiyo ima kwa kulipa gharama inayohitajika ili kumuondoa mikononi mwao, au kwa kubadilisha nao na mateka wa kikafiri, yaani: Kwa njia ya kubadilishana.
Marejeo

صحيح البخاري (7/ 67) (5373). شرح رياض الصالحين، لابن عثيمين (4/ 468). نزهة المتقين شرح رياض الصالحين، لمجموعة من الباحثين (1/ 685).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com
Tabia njema.

Kila hadithi, daraja, maelezo na funzo hapa vinaonyeshwa kama HadeethEnc.com inavyovichapisha, kwa masharti yake ya kuchapisha upya. Daraja halimtaji aliyelitoa. Tafsiri na maelezo ni ya waandishi wake wenyewe, na baadhi hutaja hukumu; wahakiki wa Sabīl hawajavichunguza. Hadithi ya Kiarabu ndiyo matini. Chanzo: HadeethEnc.com