Ruka hadi kwenye maudhui
Hadithi zenye maelezo

Ewe Aisha, hakika Mwenyezi Mungu ni Mpole anapenda upole, na hutoa malipo katika upole ambayo hayatoi katika ususuwavu (ukali), na wala hatoi kwa mengineyo

عَنْ عَائِشَةَ أُمِّ المُؤْمِنين رضي الله عنها زَوْجِ النَّبِيِّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ أَنَّ رَسُولَ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: «يَا عَائِشَةُ إِنَّ اللهَ رَفِيقٌ يُحِبُّ الرِّفْقَ، وَيُعْطِي عَلَى الرِّفْقِ مَا لَا يُعْطِي عَلَى الْعُنْفِ، وَمَا لَا يُعْطِي عَلَى مَا سِوَاهُ».
Kutoka kwa Aisha Mama wa Waumini radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, mke wa Mtume rehema na amani ziwe juu yake, ya kwamba Mtume rehema na amani ziwe juu yake alisema: "Ewe Aisha, hakika Mwenyezi Mungu ni Mpole anapenda upole, na hutoa malipo katika upole ambayo hayatoi katika ususuwavu (ukali), na wala hatoi kwa mengineyo".
Imepokelewa Imamu MuslimDarajaSahihi
Maelezo

Alimuhimiza Mtume rehema na amani ziwe juu yake mama wa Waumini Aisha radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake juu ya upole, na kwamba Mwenyezi Mungu ni Mpole kwa waja wake anawatakia wepesi na wala hawatakii ugumu, wala hawalazimishi juu ya uwezo wao, ni wajibu kwa mja wake ajipambe kwa ulaini na kuchukua kilicho rahisi; asiwe mkorofi wala mkali, na kwamba Mwenyezi Mungu Mtukufu hutoa malipo kwa sababu ya upole na ulaini katika dunia kama kusifia vizuri, na kutoa mahitaji ya watu na kurahisisha malengo, na Akhera kutoa thawabu nyingi zaidi kuliko jinsi anavyotoa katika ususuwavu na ukali na ukorofi, upole huja na mambo ambayo hayaji katika mambo mengine.

Mafunzo
  1. Himizo juu ya upole na katazo la ukali.
  2. Thamani ya nafasi ya upole katika tabia njema zote.
  3. Mtu mpole anastahiki sifa nzuri na malipo makubwa kutoka kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu.
  4. Amesema Assi-ndi: Ukali ni kinyume cha upole, yaani mwenye kuwaita watu kuja katika uongofu kwa upole na kwa huruma ni bora kuliko yule anayewaita kwa ugumu na ukali ikiwa mahali hapo panakubali mambo yote mawili, lau kama si hivyo basi achague kinachoendana na mahala, na Mwenyezi Mungu ndiye Mjuzi zaidi wa uhalisia wa hali.
Marejeo

صحيح مسلم (4/ 2003) (2593). بهجة الناظرين شرح رياض الصالحين، لسليم الهلالي (1/ 683). المنهاج شرح صحيح مسلم بن الحجاج، للنووي (16/ 145).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com
Tabia njema.

Kila hadithi, daraja, maelezo na funzo hapa vinaonyeshwa kama HadeethEnc.com inavyovichapisha, kwa masharti yake ya kuchapisha upya. Daraja halimtaji aliyelitoa. Tafsiri na maelezo ni ya waandishi wake wenyewe, na baadhi hutaja hukumu; wahakiki wa Sabīl hawajavichunguza. Hadithi ya Kiarabu ndiyo matini. Chanzo: HadeethEnc.com