Hakika muumini hufikia kwa sababu ya tabia zake njema daraja ya mfungaji mwenye kusimama usiku
عن عائشة رضي الله عنها قالت: سمعت رسول الله صلى الله عليه وسلم يقول: «إنَّ المُؤْمِنَ ليُدرِكُ بِحُسْنِ خُلُقِهِ دَرَجَةَ الصَّائِمِ القَائِمِ».
Kutoka kwa Aisha -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Nilimsikia Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akisema: "Hakika muumini hufikia kwa sababu ya tabia zake njema daraja ya mfungaji mwenye kusimama usiku".
Imepokelewa na Abu Daud na AhmadDarajaNi sahihi kwa ushahidi wake mbalimbali
Maelezo
Anabainisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa tabia njema humfikisha mwenye tabia hiyo nafasi ya mwenye kufunga mchana daima na kusimama usiku, na tabia njema inakusanywa na: Kutenda wema, na kauli nzuri, na uso mkunjufu, na kuacha maudhi na kuyavumilia kutoka kwa watu.
Mafunzo
Uislamu umetilia umuhimu mkubwa kurekebisha tabia na ukamilifu wake.
Ubora wa tabia njema, mpaka mja humfikisha daraja ya mfungaji asiyefungua na mwenye kusimama usiku asiyechoka.
Kufunga mchana na kusimama usiku ni amali mbili kubwa, kuna uzito mkubwa sana kwa nafsi, lakini daraja yake ameifikia mwenye tabia njema kwa kupambana na nafsi yake ili kuwa na muamala mzuri na watu.
Marejeo
سنن أبي داود (7/ 176) (4798).
مسند أحمد (40/ 414) (24355).
بهجة الناظرين شرح رياض الصالحين، لسليم الهلالي (1/ 675).
تطرز رياض الصالحين، لفيصل آل مبارك (ص411).
مشكاة المصابيح، لمحمد العمري (3/ 1409).
Kila hadithi, daraja, maelezo na funzo hapa vinaonyeshwa kama HadeethEnc.com inavyovichapisha, kwa masharti yake ya kuchapisha upya. Daraja halimtaji aliyelitoa. Tafsiri na maelezo ni ya waandishi wake wenyewe, na baadhi hutaja hukumu; wahakiki wa Sabīl hawajavichunguza. Hadithi ya Kiarabu ndiyo matini. Chanzo: HadeethEnc.com