Ameeleza mama wa waumini Aisha radhi za Allah ziwe juu yake, ya kwamba mwanamke mmoja alimjia akiwa na mabinti zake wawili akimuomba chochote kinacholiwa, Aisha akawa hakupata kwake zaidi ya tende moja, akampatia basi mwanamke yule akaigawanya tende hiyo baina ya watoto wake, na yeye hakula chochote, kisha akanyanyuka na akaondoka, punde akaingia Mtume rehema na amani ziwe juu yake, Aisha akamsimulia kisa hicho, akasema: Atakayesimamia chochote katika malezi ya mabinti hawa, akawatendea wema na akawalisha na akawanywesha na akawavisha, na akawa na subira juu ya hilo, basi watakuwa ni sitara na kinga kwake dhidi ya moto.
- Kuwalea watoto wa kike na kushughulika nao ni katika amali bora miogoni mwa amali njema zinazomuepusha mtu na moto.
- Sunna ya kutoa chochote kilicho ndani ya uwezo wa mtu hata kama ni kidogo.
- Huruma kubwa ya wazazi kwa watoto wao.
- Kumebainishwa hali ya nyumba za Mtume rehema na amani ziwe juu yake na kwamba riziki yake ilikuwa ya kumtosheleza pekee.
- Kumebainishwa fadhila za kujinyima kwa ajili ya watu wengine, na kwamba hilo ni katika alama za waumini; kwani Aisha alimpendelea yule mwanamke na watoto wake kuliko nafsi yake, na hii inaonyesha juu ya ukarimu wake na moyo wake wa kujitolea pamoja na kuwa ana uvihitaji.
- Zawadi ya watoto wa kike imeitwa kuwa ni mtihani; kwa sababu kuwalea kwake kuna shida na tabu nyingi, au kwa sababu ya baadhi ya watu kuwachukia, au ni kwa sababu mara nyingi wao huwa hawana vyanzo vya mapato ya maisha.
- Uislamu ulikuja kung'oa mizizi ya desturi mbovu za zama za ujinga, na miongoni mwake nikuwa uliusia watu kuwalea vizuri watoto wa kike.
- Mtu anapata malipo haya hata akiwa na binti mmoja kama ilivyokuja katika baadhi ya riwaya.
صحيح البخاري (8/ 7) (5995). صحيح مسلم (4/ 2027) (2629). بهجة الناظرين شرح رياض الصالحين، لسليم الهلالي (1/ 353). تطريز رياض الصالحين، لفيصل آل مبارك (ص199). كنوز رياض الصالحين، لمجموعة من الباحثين (5/ 151). شرح رياض الصالحين، لابن عثيمين (3/ 106). نزهة المتقين شرح رياض الصالحين، لمجموعة من الباحثين (1/ 277).