Ruka hadi kwenye maudhui
Hadithi zenye maelezo

Mche Mwenyezi Mungu popote ulipo, na ovu lifuatishe jema litalifuta, na ishi na watu kwa tabia njema

‌عَنْ ‌أَبِي ‌ذَرٍّ، ‌جُنْدُبِ ‌بْنِ ‌جُنَادَةَ، ‌وَأَبِي ‌عَبْدِ ‌الرَّحْمَنِ، ‌مُعَاذِ بْنِ جَبَلٍ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُمَا عَنْ رَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: «اتَّقِ اللَّهَ حَيْثُمَا كُنْت، وَأَتْبِعْ السَّيِّئَةَ الْحَسَنَةَ تَمْحُهَا، وَخَالِقْ النَّاسَ بِخُلُقٍ حَسَنٍ».
Kutoka kwa Abuu Dharri, Jundubi bin Junada, na Abuu Abdulrahman, Muadhi bin Jabali radhi za Allah ziwe juu yao kutoka kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake amesema: "Mche Mwenyezi Mungu popote ulipo, na ovu lifuatishe jema litalifuta, na ishi na watu kwa tabia njema"
Imepokelewa Imamu TirmidhiyDarajaAmesema Al-tirmidhiy: Hadithi hii ni Hasan
Maelezo

Ameamrisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake mambo matatu: La kwanza: Kumuogopa Mwenyezi Mungu na hii inakuwa kwa kutekeleza wajibu, na kuacha maharamisho, katika kila mahali na nyakati na hali, katika siri na wazi, na wakati wa afya na balaa na mengineyo. La pili: Ukiangukia katika ovu, basi fanya baada yake jambo jema kama swala na sadaka na wema na kuunga udugu na toba na mengineyo, kwani hayo hufuta madhambi. La tatu: Ishi na watu kwa tabia njema, kama kutabasamu katika nyuso zao, na upole na ulaini na kutenda wema na kuacha maudhi.

Mafunzo
  1. Fadhila ya Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa waja wake kwa kuwahurumia na kuwasamehe na kuwafutia makosa.
  2. Hadithi imekusanya haki tatu: Haki ya Mwenyezi Mungu ya kuogopwa, na haki ya nafsi kwa kufanya mema baada ya mabaya, na haki ya watu wengine kwa kuishi nao kwa tabia njema.
  3. Himizo la kufanya mema baada ya maovu na kuwa na tabia njema ni miongoni mwa sehemu ya uchamungu, isipokuwa alitaja peke yake kwa sababu ya haja ya kuliweka wazi.
Marejeo

الأربعون النووية (ص100) (ح18). سنن الترمذي (3/ 526) (1987). التحفة الربانية في شرح الأربعين حديثًا النووية، لإسماعيل الأنصاري (ص40). شرح الأربعين النووية، لابن عثيمين (ص195). فتح القوي المتين في شرح الأربعين وتتمة الخمسين، لعبد المحسن البدر (ص67).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com
Tabia njema.

Kila hadithi, daraja, maelezo na funzo hapa vinaonyeshwa kama HadeethEnc.com inavyovichapisha, kwa masharti yake ya kuchapisha upya. Daraja halimtaji aliyelitoa. Tafsiri na maelezo ni ya waandishi wake wenyewe, na baadhi hutaja hukumu; wahakiki wa Sabīl hawajavichunguza. Hadithi ya Kiarabu ndiyo matini. Chanzo: HadeethEnc.com