Ruka hadi kwenye maudhui
Hadithi zenye maelezo

Mambo mazuri na Adabu- Heshima.

Hadithi 386

Swala tano, na ijumaa mpaka ijumaa, na Ramadhani hadi Ramadhani, hufuta madhambi yaliyo kati yake, ikiwa mtu atayaepuka madhambi makubwa

عن أبي هريرة رضي الله عنه أن رسول الله صلى الله عليه وسلم كان يقول: «الصَّلَوَاتُ الْخَمْسُ، وَالْجُمُعَةُ إِلَى الْجُمُعَةِ، وَرَمَضَانُ إِلَى رَمَضَانَ، مُكَفِّرَاتٌ مَا بَيْنَهُنَّ إِذَا اجْتَنَبَ الْكَبَائِرَ».
Kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake- yakwamba Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- alikuwa akisema: "Swala tano, na ijumaa mpaka ijumaa, na Ramadhani hadi Ramadhani, hufuta madhambi yaliyo kati yake, ikiwa mtu atayaepuka madhambi makubwa"
Imepokelewa Imamu MuslimDarajaSahihi
Maelezo

Anaeleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa swala tano za faradhi za usiku na mchana, na swala ya ijumaa kila wiki, na funga ya Ramadhani kila mwaka, vyote hivi hufuta madhambi madogo madogo yaliyo kati yake, kwa sharti la kuyaepuka madhambi makubwa, Ama madhambi makubwa kama zinaa na kunywa pombe haya hayafutwi isipokuwa kwa toba.

Mafunzo
  1. Madhambi yako madogo madogo na yako makubwa.
  2. Kufutiwa madhambi madogo madogo kumewekwa sharti la ya kuyaepuka makubwa.
  3. Madhambi makubwa ni yale iliyokuja adhabu ndani yake katika dunia, au yaliyotajwa kuwa na ahadi ya adhabu huko Akhera; au Makasiriko, au kukawa na kemeo ndani yake, au kulaaniwa mfanyaji wake, kama zinaa na unywaji pombe.
Marejeo

صحيح مسلم (1/ 209) (233). شرح رياض الصالحين، لابن عثيمين (2/ 183). نزهة المتقين بشرح رياض الصالحين، لمصطفى سعيد الخن (1/ 158). تطريز رياض الصالحين، لفيصل آل مبارك (ص108). بهجة الناظرين شرح رياض الصالحين، لسليم بن عيد الهلالي (1/ 209).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Hakika watu wanaotumia mali ya Mwenyezi Mungu pasina haki, hao (wana adhabu ya) moto siku ya Kiyama

عن خَولة الأنصاريةِ رضي الله عنها قالت: سمعت النبي صلى الله عليه وسلم يقول: «إِنَّ رِجَالًا يَتَخَوَّضُونَ فِي مَالِ اللهِ بِغَيْرِ حَقٍّ، فَلَهُمُ النَّارُ يَوْمَ الْقِيَامَةِ».
Kutoka kwa Khaula Al-Answariya -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Nilimsikia Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akisema: "Hakika watu wanaotumia mali ya Mwenyezi Mungu pasina haki, hao (wana adhabu ya) moto siku ya Kiyama".
Imepokelewa na Al-BukhaariyDarajaSahihi
Maelezo

Anaeleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuhusu watu wanaotumia mali ya waislamu kwa batili, na wanaichukua pasina haki, na maana hii inajumuisha kuanzia ukusanyaji wake, na uchumaji wake bila uhalali wake, na utoaji wake katika sehemu zisizo sahihi, na inaingia katika hilo kula mali ya yatima na mali ya wakfu, na kutotunza amana, na kuchukua chochote katika mali ya umma bila ya haki. Ameeleza -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa malipo yao ni moto siku ya Kiyama.

Mafunzo
  1. Mali iliyoko mikononi mwa watu ni mali ya Mwenyezi Mungu, amewamilikisha ili waitoe katika njia za kisheria, na waepuke kuitumia katika batili, na hii inawahusu viongozi na wasiokuwa viongozi.
  2. Sheria imetia mkazo katika mali ya umma, nakuwa yeyote atakayesimamia chochote basi atambue kuwa atahesabiwa juu ya ukusanyaji wake na matumizi yake.
  3. Anaingia katika ahadi hii ya adhabu mwenye kufanya matumizi yasiyokuwa ya kisheria katika mali, sawa sawa iwe ni mali yake, au mali ya mwingine.
Marejeo

صحيح البخاري (4/ 85) (3118). فتح ذي الجلال والاكرام بشرح بلوغ المرام، لابن عثيمين (6/ 372). منحة العلام في شرح بلوغ المرام، لعبد الله الفوزان (10/ 231). توضيح الأحكام من بلوغ المرام، للبسام (7/ 424).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Kumtukana Muislamu ni ufasiki (kutoka nje ya mipaka), na kupigana naye ni ukafiri

عَنْ عَبْدِ اللَّهِ بنِ مَسْعُودٍ رضي الله عنه أَنَّ النَّبِيَّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: «سِبَابُ المُسْلِمِ فُسُوقٌ، وَقِتَالُهُ كُفْرٌ».
Kutoka kwa Abdallah bin Masoud -radhi za Allah ziwe juu yake- yakwamba Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Kumtukana Muislamu ni ufasiki (kutoka nje ya mipaka), na kupigana naye ni ukafiri."
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeDarajaSahihi
Maelezo

Mtume rehema na amani ziwe juu yake amemkataza muislamu kumshutumu na kumtukana ndugu yake muislamu, nakuwa hilo ni katika ufasiki ambao ni kutoka nje ya utiifu wa Mwenyezi Mungu na Mtume wake rehema na amani ziwe juu yake, nakuwa muislamu kukabiliana na ndugu yake muislamu ni katika matendo ya ukafiri, lakini ni ukafiri mdogo.

Mafunzo
  1. Ulazima wa kuheshimu heshima ya muislamu na damu yake.
  2. Ukubwa wa hatima ya kumtukana muislamu pasina haki; mwenye kutukana pasina haki ni muovu.
  3. Kumtukana muislamu na kupigana naye kunadhoofisha imani na kuipunguza.
  4. Baadhi ya matendo huitwa ukafiri; hata yasipofika katika ukafiri mkubwa wenye kumtoa mtu katika Uislamu.
  5. Makusudio ya ukafiri hapa ni ukafiri mdogo usiomtoa mtu katika Uislamu kwa makubaliano ya watu wa sunna; kwa sababu Mwenyezi Mungu Mtukufu ameuthibitisha udugu wa kiimani kwa waumini wakati wa kupigana kwao, akasema Mtukufu: "Na ikiwa makundi mawili ya waumini yatapigana basi wasuluhisheni baina yao" mpaka katika kauli yake: "Hakika waumini wote ni ndugu".
Marejeo

صحيح البخاري (1/ 19) (48). صحيح مسلم (1/ 81) (64). فتح ذي الجلال والاكرام بشرح بلوغ المرام، لابن عثيمين (6/ 362). منحة العلام في شرح بلوغ المرام، لعبد الله الفوزان (10/ 216). توضِيحُ الأحكَامِ مِن بُلوُغ المَرَام، للبسام (7/ 412).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Msiwatukane wafu, kwani wao tayari wameyapata yale waliyoyatanguliza

عن عائشة رضي الله عنها قالت: قال النبي صلى الله عليه وسلم: «لَا تَسُبُّوا الْأَمْوَاتَ، فَإِنَّهُمْ قَدْ أَفْضَوْا إِلَى مَا قَدَّمُوا».
Kutoka kwa Aisha -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: "Msiwatukane wafu, kwani wao tayari wameyapata yale waliyoyatanguliza".
Imepokelewa na Al-BukhaariyDarajaSahihi
Maelezo

Anabainisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- uharamu wa kuwatukana wafu na kuchafua heshima zao, nakuwa hili ni katika tabia mbaya, kwani wao wameyafikia yale waliyoyatanguliza katika matendo mazuri au mabaya, kama ambavyo matusi haya hayawafikii basi hakuna lolote zaidi ya kuwaudhi waliohai.

Mafunzo
  1. Hadithi ni ushahidi wa uharamu wa kuwatukana wafu.
  2. Kuacha kuwatukana wafu kuna kuchunga masilahi ya waliohai, na kuhifadhi amani ya jamii kutokana na kutotiliana vinyongo na chuki.
  3. Hekima ya kukatazwa kuwatukana nikuwa tayari wao wameyafikia yale waliyoyatanguliza, kuwatukana hakusaidii, na kuna kuwaudhi ndugu zake wa karibu.
  4. Nikuwa haifai kwa mwanadamu kusema maneno yasiyo na manufaa.
Marejeo

صحيح البخاري (2/ 104) (1393). فتح ذي الجلال والاكرام بشرح بلوغ المرام، لابن عثيمين (2/ 631). منحة العلام في شرح بلوغ المرام، لعبد الله الفوزان (4/ 385). توضيح الأحكام من بلوغ المرام، للبسام (3/ 277).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Ni haramu kwa mtu kumhama ndugu yake zaidi ya siku tatu, wanakutana, huyu akampuuza huyu na huyu naye akampuuza huyu, na mbora wao ni yule anaye anza kwa salamu

عن أبي أيوب الأنصاري رضي الله عنه أن رسول الله صلى الله عليه وسلم قال: «لَا يَحِلُّ لِرَجُلٍ أَنْ يَهْجُرَ أَخَاهُ فَوْقَ ثَلَاثِ لَيَالٍ، يَلْتَقِيَانِ، فَيُعْرِضُ هَذَا وَيُعْرِضُ هَذَا، وَخَيْرُهُمَا الَّذِي يَبْدَأُ بِالسَّلَامِ».
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Ayub Al-Answari -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- Yakwamba Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Ni haramu kwa mtu kumhama ndugu yake zaidi ya siku tatu, wanakutana, huyu akampuuza huyu na huyu naye akampuuza huyu, na mbora wao ni yule anaye anza kwa salamu".
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeDarajaSahihi
Maelezo

Amekataza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- muislamu kumhama ndugu yake muislamu zaidi ya siku tatu, wanakutana wote hamsalimii wala hamsemeshi. Na mbora kati ya hawa wagomvi wawili ni yule anayejaribu kuondoa kuhamana huku, na akaanza kwa salamu, na makusudio ya kuhamana hapa ni sababu ya kujikweza, ama kuhamana kwa ajili ya Mwenyezi Mungu Mtukufu kama kuwahama waovu na wazushi na marafiki waovu, hili halina muda maalum, bali limeambatana na masilahi katika kuhama, na linamalizika kwa kuondoka maslilahi yake.

Mafunzo
  1. Uhalali wa kumhama mtu ndani ya siku tatu kurudi chini, kwa kulinda maumbile ya kibinadamu, itasamehewa ndani ya siku tatu, ili kiondoke kile kilichojitokeza baina yao.
  2. Ubora wa salamu, nakuwa huondoa yaliyoko ndani ya nafsi, nakuwa ni alama ya kupendana.
  3. Pupa ya Uislamu juu ya udugu na ukaribu baina waislamu.
Marejeo

صحيح البخاري (8/ 21) (6077). صحيح مسلم (4/ 1984) (2560). منحة العلام في شرح بلوغ المرام، لعبد الله الفوزان (10/ 111). فتح ذي الجلال والإكرام بشرح بلوغ المرام، لابن عثيمين (6/ 293). توضيح الأحكام من بلوغ المرام، للبسام (7/ 339).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Haingii peponi mkata udugu

عن جُبَير بن مُطْعِم رضي الله عنه أنه سمع النبي صلى الله عليه وسلم يقول: «لَا يَدْخُلُ الْجَنَّةَ قَاطِعُ رَحِمٍ».
Kutoka kwa Jubairi bin Mutwim -Radhi za Allah ziwe juu yake- Yakwamba yeye alimsikia Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akisema: "Haingii peponi mkata udugu".
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeDarajaSahihi
Maelezo

Anaeleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- yakuwa atakayewakatia ndugu zake wa karibu zile haki za wajibu kwao, au akawaudhi au kuwafanyia ubaya, basi anastahiki asiingie peponi.

Mafunzo
  1. Kukata udugu ni dhambi kubwa katika madhambi makubwa.
  2. Kuunga udugu kunakuwa kulingana na desturi za watu, na kutatofautiana kulingana na mazingira na zama na jamii pia.
  3. Kuunga udugu kunakuwa kwa kutembeleana, na kwa sadaka, na kuwatendea wema, na kuwatembelea wagonjwa, na kuwaamrisha mema, na kuwakataza maovu, na mengineyo.
  4. Kila ambavyo kukata udugu kunavyozidi kuwa kwa ndugu wa karibu zaidi ndivyo ambavyo madhambi yanavyokuwa makubwa.
Marejeo

صحيح مسلم (4/ 1981) (2556). صحيح البخاري (8/ 5) (5984). شرح النووي على مسلم (16/ 113). منحة العلام في شرح بلوغ المرام، لعبد الله الفوزان (10/ 90). فتح ذي الجلال والإكرام بشرح بلوغ المرام، لابن عثيمين (6/ 277).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Hakika mtu anayechukiza zaidi kwa Mwenyezi Mungu ni mgomvi mkorofi

عن عائشة رضي الله عنها عن النبي صلى الله عليه وسلم قال: «إِنَّ أَبْغَضَ الرِّجَالِ إِلَى اللهِ الْأَلَدُّ الْخَصِمُ».
Imepokewa kutoka kwa Aisha -Radhi za Allah ziwe juu yake- kutoka kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Hakika mtu anayechukiza zaidi kwa Mwenyezi Mungu ni mgomvi mkorofi".
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeDarajaSahihi
Maelezo

Anaeleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa Mwenyezi Mungu -Aliyetakasika na kutukuka- anawachukia miongoni mwa watu mwenye ugomvi mkali na mwingi, asiyekubali kutii haki, na anajaribu kuikataa kwa mijadala, au akagombana kwa haki akapitiliza katika ugomvi na akatoka katika mpaka wa uadilifu, na akajadiliana bila elimu.

Mafunzo
  1. Haingii katika mlango wa mgomvi mbaya, aliyedhulumiwa kudai haki yake kwa njia ya kushitakiana kisheria.
  2. Mijadala na ugomvi ni katika maafa ya ulimi yanayosababisha kutengana na kupeana migongo kati ya waislamu.
  3. Mjadala ni mzuri utapokuwa katika haki na utaratibu mzuri, na unakuwa mbaya utapokuwa ni kwa kuikataa haki na kuitetea batili, au ukawa bila hoja wala ushahidi.
Marejeo

صحيح البخاري (3/ 131) (2457). صحيح مسلم (4/ 2054) (2668). توضيح الأحكام من بلوغ المرام، للبسام (7/ 476). منحة العلام في شرح بلوغ المرام، لعبد الله الفوزان (10/ 308). فتح ذي الجلال والإكرام، لابن عثيمين (6/ 416). سبل السلام بشرح بلوغ المرام، للصنعاني (2/ 685).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Atakayeitetea heshima ya ndugu yake basi Mwenyezi Mungu ataukinga uso wake na moto siku ya Kiyama

عن أبي الدرداء رضي الله عنه عن النبي صلى الله عليه وسلم قال: «مَنْ رَدَّ عَنْ عِرْضِ أَخِيهِ رَدَّ اللهُ عَنْ وَجْهِهِ النَّارَ يَوْمَ الْقِيَامَةِ».
Imepokewa kutoka kwa Abuu Dardaa -Radhi za Allah ziwe juu yake- kutoka kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Atakayeitetea heshima ya ndugu yake basi Mwenyezi Mungu ataukinga uso wake na moto siku ya Kiyama".
Imepokelewa na Tirmidhiy na AhmadDarajaSahihi
Maelezo

Anaeleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa atakayeitetea heshima ya ndugu yake muislamu akiwa hayupo (katika mazungumzo) kwa kukataza watu kumsema vibaya na kumkosea adabu, basi naye Mwenyezi Mungu ataizuia adhabu kwake siku ya Kiyama.

Mafunzo
  1. Katazo la kuzungumza kuhusu heshima za waislamu.
  2. Malipo huendana na matendo, atakayeirudisha heshima ya ndugu yake Mwenyezi Mungu naye atauzuia moto kwake.
  3. Uislamu ni dini ya udugu na kuteteana kati ya waislamu.
Marejeo

سنن الترمذي (3/ 488) (1931). مسند أحمد (45/ 528) (27543). توضيح الأحكام من بلوغ المرام، للبسام (7/ 499). منحة العلام في شرح بلوغ المرام، لعبد الله الفوزان (10/ 349). فتح ذي الجلال والإكرام، لابن عثيمين (6/ 437). سبل السلام بشرح بلوغ المرام، للصنعاني (2/ 692).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com
8 kati ya 12
Hadithi 12
  1. Swala tano, na ijumaa mpaka ijumaa, na Ramadhani hadi Ramadhani, hufuta madhambi yaliyo kati yake, ikiwa mtu atayaepuka madhambi makubwa
  2. Hakika watu wanaotumia mali ya Mwenyezi Mungu pasina haki, hao (wana adhabu ya) moto siku ya Kiyama
  3. Kumtukana Muislamu ni ufasiki (kutoka nje ya mipaka), na kupigana naye ni ukafiri
  4. Msiwatukane wafu, kwani wao tayari wameyapata yale waliyoyatanguliza
  5. Ni haramu kwa mtu kumhama ndugu yake zaidi ya siku tatu, wanakutana, huyu akampuuza huyu na huyu naye akampuuza huyu, na mbora wao ni yule anaye anza kwa salamu
  6. Haingii peponi mkata udugu
  7. Hakika mtu anayechukiza zaidi kwa Mwenyezi Mungu ni mgomvi mkorofi
  8. Atakayeitetea heshima ya ndugu yake basi Mwenyezi Mungu ataukinga uso wake na moto siku ya Kiyama
  9. Ogopeni dhulma, kwa hakika dhulma ni giza siku ya kiyama. Na ogopeni tamaa, kwa hakika tamaa iliwaangamiza walio kuwepo kabla yenu
  10. Ya kwamba mtu mmoja alimuuliza Mtume rehema na amani zimfikie: Ni Uislamu upi bora? Akasema: "Ni, ulishe chakula, na utoe salamu kwa unayemjua na usiyemjua
  11. Hakika wamekuja katika familia za Muhammad wanawake wengi wakiwashitakia waume zao, (wanaume) hao si bora kati yenu
  12. Msitengeze mabustani, mkajakuipenda sana dunia

Kila hadithi, daraja, maelezo na funzo hapa vinaonyeshwa kama HadeethEnc.com inavyovichapisha, kwa masharti yake ya kuchapisha upya. Daraja halimtaji aliyelitoa. Tafsiri na maelezo ni ya waandishi wake wenyewe, na baadhi hutaja hukumu; wahakiki wa Sabīl hawajavichunguza. Hadithi ya Kiarabu ndiyo matini. Chanzo: HadeethEnc.com