Alikataza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwapiga wanawake, akaja kiongozi wa Waumini Omari bin Khattwabi radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake akasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu wanawake wamepata ujasiri kwa waume zao, na wamekuwa na tabia mbovu. Akaruhusu rehema na amani ziwe juu yake kuwapiga kipigo kisichojeruhi inapopatikana sababu ya hilo, kama kukataa kwao kutimiza wajibu wao kwa waume zao na kuwaasi, na mfano wa hayo. Baada ya hapo wakaja wanawake kwa wake wa Mtume rehema na amani ziwe juu yake wakishitakia kupigwa na waume zao kipigo chenye kujeruhi, na matumizi mabaya ya ruhusa hii, akasema Mtume rehema na amani ziwe juu yake: Wanaume hao, wanaowapiga wake zao kipigo chenye kujeruhi, si watu bora kwenu.
- Kumebainishwa fadhila za kuishi vizuri na wanawake, na kwamba kuwavumilia na kufumbia macho yale yanayojitokeza kwao ni bora kuliko kuwapiga.
- Alifanya Mwenyezi Mungu Mtukufu kipigo kuwa hatua ya mwisho katika suluhisho la ujeuri, akasema: "Na wale mnaochelea kutoka kwao katika utiifu, waaidhini (wanasihini), na wahameni katika malazi, na wapigeni. Basi wakiwatii, msitafute njia yoyote dhidi yao. Hakika, Mwenyezi Mungu ndiye aliye juu, Mkubwa" [An-Nisaai: 34], na njia hizi tatu zimepangwa kwa utaratibu, na si zote kwa wakati mmoja, ataanza kwa nasaha na mawaidha, na kumkubusha, ikiwa itazaa matunda basi Alhamdulillaah, na isipoleta tija amuhame kitandani,, isipoleta tija, ampige kipigo cha kuadabisha nasi cha kulipa kisasi.
- Mwanaume ni msimamizi katika nyumba yake, anawajibu wa kuwalea na kuwaadabisha kwa hekima na mawaidha mazuri.
- Inafaa msomi kujirudi katika majibu yake; pale anapojua matokeo yake na mwisho wake.
- Inafaa kuweka kikao cha majadiliano na kiongozi au mwanachuoni, endapo alipatwa madhara anayeshitaki.
سنن أبي داود (3/ 479) (2146). سنن ابن ماجه (3/ 152) (1985). بهجة الناظرين شرح رياض الصالحين، لسليم الهلالي (1/ 363). مرقاة المفاتيح، لعلي القاري (5/ 2127).