عَنْ عَبْدِ اللهِ بْنِ مَسْعُودٍ رَضيَ اللهُ عنهُ قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: «لاَ تَتَّخِذُوا الضَّيْعَةَ فَتَرْغَبُوا فِي الدُّنْيَا».
Kutoka kwa Abdallah bin Masoud -radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -rehema na amani ziwe juu yake-: "Msitengeze mabustani, mkajakuipenda sana dunia".
Imepokelewa na Tirmidhiy na AhmadDarajaNi nzuri kwa sababu ya hadithi nyinginezo
Maelezo
Amekataza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kujitengenezea makonde na mabustani na mashamba; kwa sababu hilo ni katika sababu za kuipenda sana dunia na kubweteka nayo na kuisahau Akhera.
Mafunzo
- Katazo la kukithirisha sana hadhi za kidunia kwa sababu hupelekea kuiacha Akhera.
- Katika hadithi hakuna katazo la kutengeneza yale yanayopelekea maisha, bali katazo ni kuzama katika dunia na kuisahau Akhera.
- Amesema Sanadi: Na makusudio yake: Nikuwa msizame katika kutengeneza mabustani, mkapumbazika nayo na mkajisahau kumtaja Mwenyezi Mungu.
Marejeo
سنن الترمذي (4/ 155) (2328). مسند أحمد (6/ 54) (3579). كنوز رياض الصالحين، لمجموعة من الباحثين (331/7). شرح رياض الصالحين لابن عثيمين (375/3).