Ya kwamba mtu mmoja alimuuliza Mtume rehema na amani zimfikie: Ni Uislamu upi bora? Akasema: "Ni, ulishe chakula, na utoe salamu kwa unayemjua na usiyemjua
Kutoka kwa Abdallah Bin Amri -Radhi za Allah ziwe juu yake na baba yake-: Ya kwamba mtu mmoja alimuuliza Mtume rehema na amani zimfikie: Ni Uislamu upi bora? Akasema: "Ni, ulishe chakula, na utoe salamu kwa unayemjua na usiyemjua".
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeDarajaSahihi
Maelezo
Aliulizwa Mtume rehema na amani zimfikie: Ni jambo lipi katika Uislamu ni bora? Akataja mambo mawili:
La kwanza: Kukirithirisha kuwalisha masikini, na inaingia hapa sadaka na zawadi na kuwakirimu wageni na walima (harusi), na inatiliwa mkazo fadhila ya kulisha masikini katika nyakati za njaa na wakati wa bidhaa kupanda bei.
La pili: Kumpa salamu kila muislamu, unayemjua na usiyemjua.
Mafunzo
Pupa ya Masahaba katika kuyajua mambo yenye manufaa katika Dunia na Akhera.
Salamu na kulisha chakula ni miongoni mwa amali bora katika Uislamu; kwa sababu ya fadhila zake na uhitaji wa watu juu ya chakula katika wakati wote.
Kwa mambo haya mawili ihisani (wema) unakuwa kwa kauli na vitendo, nao ndio wema uliokamilika zaidi.
Mambo haya ni katika mambo yanayohusu maisha ya waislamu baina yao, na kuna mambo yanahusu mahusiano ya mja na Mola wake.
Kuanza kwa salamu ni maalumu kwa waislamu, haitolewi salamu kwa kumuanza asiyekuwa muislamu.
Marejeo
صحيح البخاري (1/ 12) (12).
صحيح مسلم (1/ 65) (39).
بهجة الناظرين شرح رياض الصالحين، لسليم الهلالي (1/ 604).
مرقاة المفاتيح شرح مشكاة المصابيح، لعلي القاري (7/ 2936).
Kila hadithi, daraja, maelezo na funzo hapa vinaonyeshwa kama HadeethEnc.com inavyovichapisha, kwa masharti yake ya kuchapisha upya. Daraja halimtaji aliyelitoa. Tafsiri na maelezo ni ya waandishi wake wenyewe, na baadhi hutaja hukumu; wahakiki wa Sabīl hawajavichunguza. Hadithi ya Kiarabu ndiyo matini. Chanzo: HadeethEnc.com