Hakika mtu anayechukiza zaidi kwa Mwenyezi Mungu ni mgomvi mkorofi
عن عائشة رضي الله عنها عن النبي صلى الله عليه وسلم قال: «إِنَّ أَبْغَضَ الرِّجَالِ إِلَى اللهِ الْأَلَدُّ الْخَصِمُ».
Imepokewa kutoka kwa Aisha -Radhi za Allah ziwe juu yake- kutoka kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Hakika mtu anayechukiza zaidi kwa Mwenyezi Mungu ni mgomvi mkorofi".
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeDarajaSahihi
Maelezo
Anaeleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa Mwenyezi Mungu -Aliyetakasika na kutukuka- anawachukia miongoni mwa watu mwenye ugomvi mkali na mwingi, asiyekubali kutii haki, na anajaribu kuikataa kwa mijadala, au akagombana kwa haki akapitiliza katika ugomvi na akatoka katika mpaka wa uadilifu, na akajadiliana bila elimu.
Mafunzo
Haingii katika mlango wa mgomvi mbaya, aliyedhulumiwa kudai haki yake kwa njia ya kushitakiana kisheria.
Mijadala na ugomvi ni katika maafa ya ulimi yanayosababisha kutengana na kupeana migongo kati ya waislamu.
Mjadala ni mzuri utapokuwa katika haki na utaratibu mzuri, na unakuwa mbaya utapokuwa ni kwa kuikataa haki na kuitetea batili, au ukawa bila hoja wala ushahidi.
Marejeo
صحيح البخاري (3/ 131) (2457).
صحيح مسلم (4/ 2054) (2668).
توضيح الأحكام من بلوغ المرام، للبسام (7/ 476).
منحة العلام في شرح بلوغ المرام، لعبد الله الفوزان (10/ 308).
فتح ذي الجلال والإكرام، لابن عثيمين (6/ 416).
سبل السلام بشرح بلوغ المرام، للصنعاني (2/ 685).
Kila hadithi, daraja, maelezo na funzo hapa vinaonyeshwa kama HadeethEnc.com inavyovichapisha, kwa masharti yake ya kuchapisha upya. Daraja halimtaji aliyelitoa. Tafsiri na maelezo ni ya waandishi wake wenyewe, na baadhi hutaja hukumu; wahakiki wa Sabīl hawajavichunguza. Hadithi ya Kiarabu ndiyo matini. Chanzo: HadeethEnc.com