Ruka hadi kwenye maudhui
Hadithi zenye maelezo

Hamshukuru Mwenyezi Mungu asiyewashukuru watu

عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ عَنِ النَّبِيِّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: «لَا يَشْكُرُ اللَّهَ مَنْ لَا يَشْكُرُ النَّاسَ»
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira radhi za Allah ziwe juu yake kutoka kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake amesema: "Hamshukuru Mwenyezi Mungu asiyewashukuru watu"
Imepokelewa na Abu Daud, Tirmidhiy na AhmadDarajaSahihi
Maelezo

Ameeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa kwa kawaida hamshukuru Mwenyezi Mungu asiyewashukuru watu kwa wema na mazuri waliyomfanyia, na hii ni kwa sababu mambo haya mawili yote yanaungana, kiasi kwamba katika tabia yake na desturi yake ni kukufuru neema na kuacha kushukuru, pia atakuwa katika kawaida yake ni kukufuru neema za Mwenyezi Mungu na kupuuza katika kushukuru kwa neema hizo.

Mafunzo
  1. Umuhimu wa kuwashukuru watu kwa mazuri.
  2. Mneemeshaji halisia ni Mwenyezi Mungu Mtukufu, na viumbe ni sababu, huileta Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa amtakaye, na kwa hivyo kuwashukuru watu ni miongoni mwa kumshukuru Mwenyezi Mungu Mtukufu.
  3. Kuwashukuru watu kwa wema ni dalili ya ukamilifu wa tabia njema.
Marejeo

سنن أبي داود (7/ 188) (4811). سنن الترمذي (3/ 403) (1954). مسند أحمد (13/ 322) (7939). شرح سنن أبي داود لابن رسلان (18/ 490). شرح سنن أبي داود للعباد (547/ 13).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com
Tabia njema.

Kila hadithi, daraja, maelezo na funzo hapa vinaonyeshwa kama HadeethEnc.com inavyovichapisha, kwa masharti yake ya kuchapisha upya. Daraja halimtaji aliyelitoa. Tafsiri na maelezo ni ya waandishi wake wenyewe, na baadhi hutaja hukumu; wahakiki wa Sabīl hawajavichunguza. Hadithi ya Kiarabu ndiyo matini. Chanzo: HadeethEnc.com