Ruka hadi kwenye maudhui
Hadithi zenye maelezo

Hakika Mwenyezi Mungu amewajibisha (kufanya) wema katika kila kitu

عن شداد بن أوس رضي الله عنه قال: ثِنْتَانِ حَفِظْتُهُمَا عَنْ رَسُولِ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: «إِنَّ اللهَ كَتَبَ الْإِحْسَانَ عَلَى كُلِّ شَيْءٍ، فَإِذَا قَتَلْتُمْ فَأَحْسِنُوا الْقِتْلَةَ، وَإِذَا ذَبَحْتُمْ فَأَحْسِنُوا الذَّبْحَ، وَلْيُحِدَّ أَحَدُكُمْ شَفْرَتَهُ، فَلْيُرِحْ ذَبِيحَتَهُ».
Imepokewa Kutoka kwa Shaddad bin Ausi -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Mambo mawili niliyahifadhi kutoka kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- alisema: "Hakika Mwenyezi Mungu amewajibisha (kufanya) wema katika kila kitu, mtakapoua basi ueni kwa namna iliyokuwa nzuri, na mtakapochinja basi kwa namna iliyokuwa nzuri, na anoe mmoja wenu zana yake ya kuchinjia, na akistareheshe kichinjwa chake".
Imepokelewa Imamu MuslimDarajaSahihi
Maelezo

Anaeleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu ametuwajibishia kutenda wema katika kila kitu, na wema: Ni kuchunga mipaka ya Mwenyezi Mungu daima, na katika ibada zake, na katika kutenda kheri na kuacha kuwaudhi viumbe, miongoni mwa hayo ni kutenda wema katika kuuwa na kuchinja. Wema katika kuuwa ni wakati wa kisasi: Achague njia nyepesi na rahisi zaidi na ya haraka zaidi kutoa roho kwa mwenye kuuawa. Na wema katika kuchinja ni wakati wa kuchinja: Amuhurumie mnyama kwa kunoa kifaa, na kisinolewe mbele ya mnyama akitazama, na asichinjwe hali yakuwa wanyama wenzake wanatazama.

Mafunzo
  1. Huruma ya Mwenyezi Mungu na upole wake kwa viumbe.
  2. Wema wa kuuwa na kuchinja uwe kwa namna ya kisheria.
  3. Ukamilifu wa sheria na kushughulikia kwake kila kheri, na miongoni mwake ni kuwahurumia wanyama na upole juu yao.
  4. Katazo la kusulubu (kumtesa) mwanadamu baada ya kumuua.
  5. Uharamu wa kila chenye kumtesa mnyama.
Marejeo

صحيح مسلم (3/ 1548) (1955). التحفة الربانية في شرح الأربعين حديثا النووية (ص38). شرح الأربعين النووية، لابن عثيمين (ص185). فتح القوي المتين في شرح الأربعين وتتمة الخمسين، للعباد (ص65). فتح الباري، لابن حجر (9/ 644). شرح النووي على مسلم (13/ 107).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com
Uchinjaji.

Kila hadithi, daraja, maelezo na funzo hapa vinaonyeshwa kama HadeethEnc.com inavyovichapisha, kwa masharti yake ya kuchapisha upya. Daraja halimtaji aliyelitoa. Tafsiri na maelezo ni ya waandishi wake wenyewe, na baadhi hutaja hukumu; wahakiki wa Sabīl hawajavichunguza. Hadithi ya Kiarabu ndiyo matini. Chanzo: HadeethEnc.com