عَنْ أَنَسٍ رَضيَ اللهُ عنهُ قَالَ: ضَحَّى النَّبِيُّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ بِكَبْشَيْنِ أَمْلَحَيْنِ أَقْرَنَيْنِ، ذَبَحَهُمَا بِيَدِهِ، وَسَمَّى وَكَبَّرَ، وَوَضَعَ رِجْلَهُ عَلَى صِفَاحِهِمَا.
Imepokelewa kutoka kwa Anas -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe ju yake- amesema: Alichinja Mtume rehema na amani ziwe juu yake kondoo wawili wazuri weupe wenye pembe, aliwachinja kwa mkono wake, akasema, Bismillahi Allaahu Akbar, na akaweka mguu wake ubavuni mwao.
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeDarajaSahihi
Maelezo
Ameeleza Anasi radhi za Allah ziwe juu yake kuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake alichinja kwa mkono wake siku ya Idil Adh-haa kondoo wawili madume wenye mapembe, weupe wenye mchanganyiko na weusi, na akasema: Bismillaahi wallaahu Akbaru, na akaweka mguu wake katika shingo zao.
Mafunzo
- Sheria ya kuchinja siku ya Idi kubwa (Adh-ha), na waislamu wote wamekubaliana hilo.
- Kilichobora zaidi ni kuwa kichinjwa kiwe cha aina hii aliyochinja Mtume rehema na amani ziwe juu yake; kwa muonekano wake mzuri lakini pia mafuta yake na nyama yake nzuri.
- Amesema Imam Nawawi: Hapa kuna sunna ya mtu asimamie mwenyewe kuchinja kichinjwa chake cha udhuhia, na wala asimuwakilishe yeyote ila kwa udhuru, na hapo pia ni sunna ashuhudie kichinjwa chake, na ikiwa atamuweka muislamu kwa niaba yake itafaa kwa itifaki ya wanachuoni.
- Amesema bin Hajari: Na hapa kuna sunna ya kutoa takbira (Allaahu Akbaru) pamoja na kumtaja Mwenyezi Mungu (Bismillaah) wakati wa kuchinja, na kuweka mguu katika weupe wa shingo wa kulia wa mnyama, na wamekubaliana wanachuoni kuwa ubavu wake unakuwa upande wa kushoto ataweka mguu wake wa kulia ili iwe rahisi kumchinja wakati wa kuchukua kisu kwa mkono wa kulia na kukamata kichwa chake kwa mkono wake wa kulia
- Ni sunna kichinjwa cha udh-hiya kiwe na pembe na inafaa pia kwa kinginecho.
Marejeo
صحيح البخاري (7/ 102) (5565).
صحيح مسلم (3/ 1556) (1966).
تيسير العلام شرح عمدة الأحكام، لعبد الله البسام (ص724).
الإعلام بفوائد عمدة الأحكام، لابن الملقن (10/ 179).
Hadithi hii kwenye HadeethEnc.comعَنْ رَافِعِ بْنِ خَدِيجٍ رَضيَ اللهُ عنهُ قَالَ: كُنَّا مَعَ النَّبِيِّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ بِذِي الحُلَيْفَةِ، فَأَصَابَ النَّاسَ جُوعٌ، فَأَصَابُوا إِبِلًا وَغَنَمًا، قَالَ: وَكَانَ النَّبِيُّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ فِي أُخْرَيَاتِ القَوْمِ، فَعَجِلُوا، وَذَبَحُوا، وَنَصَبُوا القُدُورَ، فَأَمَرَ النَّبِيُّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ بِالقُدُورِ، فَأُكْفِئَتْ، ثُمَّ قَسَمَ، فَعَدَلَ عَشَرَةً مِنَ الغَنَمِ بِبَعِيرٍ فَنَدَّ مِنْهَا بَعِيرٌ، فَطَلَبُوهُ، فَأَعْيَاهُمْ وَكَانَ فِي القَوْمِ خَيْلٌ يَسِيرَةٌ، فَأَهْوَى رَجُلٌ مِنْهُمْ بِسَهْمٍ، فَحَبَسَهُ اللَّهُ، ثُمَّ قَالَ: «إِنَّ لِهَذِهِ البَهَائِمِ أَوَابِدَ كَأَوَابِدِ الوَحْشِ، فَمَا غَلَبَكُمْ مِنْهَا فَاصْنَعُوا بِهِ هَكَذَا»، فَقَالَ أي رافع: إِنَّا نَرْجُو -أَوْ نَخَافُ- العَدُوَّ غَدًا، وَلَيْسَتْ مَعَنَا مُدًى، أَفَنَذْبَحُ بِالقَصَبِ؟ قَالَ: «مَا أَنْهَرَ الدَّمَ، وَذُكِرَ اسْمُ اللَّهِ عَلَيْهِ فَكُلُوهُ، لَيْسَ السِّنَّ وَالظُّفُرَ، وَسَأُحَدِّثُكُمْ عَنْ ذَلِكَ: أَمَّا السِّنُّ فَعَظْمٌ، وَأَمَّا الظُّفُرُ فَمُدَى الحَبَشَةِ».
Kutoka kwa Raafi bin Khadiji radhi za Allah ziwe juu yake amesema: Siku moja tulikuwa pamoja na Mtume rehema na amani ziwe juu yake maeneo ya Dhul-Hulaifa, watu wakapatwa na njaa, wakapata ngamia na mbuzi, akasema: Na Mtume rehema na amani ziwe juu yake alikuwa mwisho wa watu wote, wakaharakisha, wakachinja, na wakabandika vyungu, Mtume rehema na amani ziwe juu yake akaamrisha vyungu vikamiminwa, kisha akagawa na akalinganisha mbuzi kumi sawa na ngamia mmoja, ngamia mmoja akatoroka, wakamtafuta, akawashinda, na hawakuweza kumpata, na walikuwa na farasi wachache, mtu mmoja akarusha mshale, Mwenyezi Mungu akauzuia, kisha akasema rehema na amani ziwe juu yake: "Hakika wanyama hawa wafugwao ni wanyama kama walivyo wanyama pori, watakaokushindeni miongoni mwao (kuwachinja) basi fanyeni hivyo", Raafi akasema: Sisi tunawahofia maadui kesho, na hatuna visu, je tuchinje kwa miti mikavu iliyochongwa? Akasema: "Mnyama yoyote atakayemwagwa damu, na akatajiwa jina la Mwenyezi Mungu basi kuleni, isipokuwa jino na kwato, na nitakuelezeni kuhusu hilo: Ama jino ninamaanisha mfupa, na ama kwato ni visu vya wahabeshi".
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeDarajaSahihi
Maelezo
Ameeleza Raafi bin Khadiji radhi za Allah ziwe juu yake ya kwamba wao walikuwa pamoja na Mtume rehema na amani ziwe juu yake eneo la Dhul-Hulaifa, watu wakapatwa na njaa, na walikuwa wamepata ngawira kutoka kwa washirikina, ngamia pamoja na mbuzi, wakafanya haraka kabla ngawira hazijagawanywa wakazichinja, na wakabandika vyungu jikoni, pasina ya kumuomba idhini Mtume rehema na amani ziwe juu yake, na alikuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake akitembea mwishoni mwa watu, alipojua hilo Mtume rehema na amani ziwe juu yake aliamrisha vyungu vikamiminwa pamoja na mchuzi wake, kisha akawagawia ngawira baina yao, akafanya mbuzi kumi ni sawa na ngamia mmoja, ngamia mmoja katika hao akakimbia, wakashindwa kumkamata wala kumpata, na farasi walikuwa wachache, bwana mmoja akampiga yule ngamia kwa mshale, Mwenyezi Mungu akawazuilia, akasema rehema na amani ziwe juu yake: Hakika wanyama hawa wafugwao wana tabia kama tabia za wanyama pori, watakapokushindeni miongoni mwao na hamkuweza kuwakamata basi fanyeni hivyo. Akasema Raafi: Hakika sisi tunataraji kukutana na maadui zetu kesho na tunahofia kuharibu makali ya silaha zetu ikiwa tutazichinjia, na tunahaja kubwa ya kuchinja, na hatuna kisu, je tuchinje kwa miti ya mwanzi mikavu? Akasema rehema na amani ziwe juu yake: Kitakachomwaga damu na kikaitiririsha na kikaimwaga kwa wingi, na likatajwa jina la Mwenyezi Mungu, basi kuleni, isipokuwa jino na kwato, na nitakuhadithieni kuhusu hilo: Ama jino ni mfupa, na ama kwato hizo makafiri wa Ethiopia huzitumia.
Mafunzo
- Kumewekwa wazi sehemu ya unyenyekevu wake rehema na amani ziwe juu yake kwa kutembea kwake nyuma ya jeshi, na kuchunga kwake Maswahaba wake, na kuwafuatilia, na kukubali kwake nasaha za Maswahaba wake radhi za Allah ziwe juu yake.
- Kiongozi anatakiwa kuwaadabisha raia wake na jeshi lake, kwani aliwaadabisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake kwa haraka hii na maamuzi haya waliyoyafanya, kabla ya kuchukua idhini yake, malipo yao yakawa ni kuwanyima walichokitaka.
- Uharaka wa kuitika amri za Mtume rehema na amani ziwe juu yake kwa Maswahaba radhi za Allah ziwe juu yao.
- Katazo la kuchukua ngawira mpaka zigawanywe.
- Uadilifu hasa hasa katika sehemu ya kupambana na maadui na makafiri; kwa sababu hilo ni miongoni mwa sababu za ushindi na kuwazidi maadui.
- Amesema Nawawi: Atakapofuga mtu kuwa ngamia au ng'ombe au farasi anaweza kumdhuru au mbuzi akakimbia au kinginecho basi anakuwa ni sawa kiwindwa kingine, kinakuwa halali kwa kukirushia mshale au kinginecho.
- Ni wajibu kumchinja mnyama ili awe halali kuliwa, na mnyama ni sharti: 1- Awe halali kuliwa, 2- Awe anawezekana kupatikana, ama asiyewezekana hukumu yake ni sawa na hukumu ya wanyama pori, 3- Awe ni mnyama wa nchi kavu; ama wanyama wa Baharini hao si sharti kuchinjwa.
- Sharti za kusihi kuchinja: 1- Mchinjaji awe na vigezo vya kuchinja, kwa kuwa na akili, na utambuzi, na awe muislamu au Ahlu kitab, 2- Ataje jina la Mwenyezi Mungu wakati wa kuanza kuchinja, 3- Kifaa cha kuchinjia kiwe chenye kufaa, yaani kifaa kinachotumika kuchinjia kiwe kikali cha madini ya aina yoyote ile isipokuwa mfupa na kwato, 4- Kuchinja kuwe mahala pa kuchinjia kwa mnyama anayewezekana kuchinjwa, kwa kukata mshipa wa fahamu na koo na mishipa ya shingo.
Marejeo
صحيح البخاري (3/ 138) (2488).
صحيح مسلم (3/ 1558) (1968).
تيسير العلام شرح عمدة الأحكام، لعبد الله البسام (ص721).
Hadithi hii kwenye HadeethEnc.comعن شداد بن أوس رضي الله عنه قال: ثِنْتَانِ حَفِظْتُهُمَا عَنْ رَسُولِ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: «إِنَّ اللهَ كَتَبَ الْإِحْسَانَ عَلَى كُلِّ شَيْءٍ، فَإِذَا قَتَلْتُمْ فَأَحْسِنُوا الْقِتْلَةَ، وَإِذَا ذَبَحْتُمْ فَأَحْسِنُوا الذَّبْحَ، وَلْيُحِدَّ أَحَدُكُمْ شَفْرَتَهُ، فَلْيُرِحْ ذَبِيحَتَهُ».
Imepokewa Kutoka kwa Shaddad bin Ausi -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Mambo mawili niliyahifadhi kutoka kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- alisema: "Hakika Mwenyezi Mungu amewajibisha (kufanya) wema katika kila kitu, mtakapoua basi ueni kwa namna iliyokuwa nzuri, na mtakapochinja basi kwa namna iliyokuwa nzuri, na anoe mmoja wenu zana yake ya kuchinjia, na akistareheshe kichinjwa chake".
Imepokelewa Imamu MuslimDarajaSahihi
Maelezo
Anaeleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu ametuwajibishia kutenda wema katika kila kitu, na wema: Ni kuchunga mipaka ya Mwenyezi Mungu daima, na katika ibada zake, na katika kutenda kheri na kuacha kuwaudhi viumbe, miongoni mwa hayo ni kutenda wema katika kuuwa na kuchinja.
Wema katika kuuwa ni wakati wa kisasi: Achague njia nyepesi na rahisi zaidi na ya haraka zaidi kutoa roho kwa mwenye kuuawa.
Na wema katika kuchinja ni wakati wa kuchinja: Amuhurumie mnyama kwa kunoa kifaa, na kisinolewe mbele ya mnyama akitazama, na asichinjwe hali yakuwa wanyama wenzake wanatazama.
Mafunzo
- Huruma ya Mwenyezi Mungu na upole wake kwa viumbe.
- Wema wa kuuwa na kuchinja uwe kwa namna ya kisheria.
- Ukamilifu wa sheria na kushughulikia kwake kila kheri, na miongoni mwake ni kuwahurumia wanyama na upole juu yao.
- Katazo la kusulubu (kumtesa) mwanadamu baada ya kumuua.
- Uharamu wa kila chenye kumtesa mnyama.
Marejeo
صحيح مسلم (3/ 1548) (1955).
التحفة الربانية في شرح الأربعين حديثا النووية (ص38).
شرح الأربعين النووية، لابن عثيمين (ص185).
فتح القوي المتين في شرح الأربعين وتتمة الخمسين، للعباد (ص65).
فتح الباري، لابن حجر (9/ 644).
شرح النووي على مسلم (13/ 107).
Hadithi hii kwenye HadeethEnc.comعَنْ أَبِي يَعْلَى شَدَّادِ بْنِ أَوْسٍ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ عَنْ رَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: «إِنَّ اللهَ كَتَبَ الْإِحْسَانَ عَلَى كُلِّ شَيْءٍ، فَإِذَا قَتَلْتُمْ فَأَحْسِنُوا القِتْلَةَ، وَإِذَا ذَبَحْتُمْ فَأَحْسِنُوا الذِّبْحَةَ، وَلْيُحِدَّ أَحَدُكُمْ شَفْرَتَهُ، وَلْيُرِحْ ذَبِيحَتَهُ».
Imepokewa kutoka kwa Abuu Ya'la Shaddad bin Ausi -radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Kutoka kwa Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- alisema: "Hakika Mwenyezi Mungu amefaradhisha (kutenda) wema katika kila kitu, hivyo mtakapoua basi uweni vizuri (kwa wema), na mtakapochinja basi chinjeni vizuri, na anowe mmoja wenu kisu chake, na akistareheshe kichinjwa chake".
Imepokelewa Imamu MuslimDarajaSahihi
Maelezo
Anaeleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu ametuwajibishia kutenda wema katika kila kitu, na wema: Ni kuchunga mipaka ya Mwenyezi Mungu daima, na katika ibada zake, na katika kutenda kheri na kuacha kuwaudhi viumbe, miongoni mwa hayo ni kutenda wema katika kuuwa na kuchinja.
Wema katika kuuwa ni wakati wa kisasi: Achague njia nyepesi na rahisi zaidi na ya haraka zaidi kutoa roho kwa mwenye kuuawa.
Na wema katika kuchinja ni wakati wa kuchinja: Amuhurumie mnyama kwa kunoa kifaa, na kisinolewe mbele ya mnyama akitazama, na asichinjwe hali yakuwa wanyama wenzake wanatazama.
Mafunzo
- Huruma ya Mwenyezi Mungu na upole wake kwa viumbe.
- Wema wa kuuwa na kuchinja uwe kwa namna ya kisheria.
- Ukamilifu wa sheria na kushughulikia kwake kila kheri, na miongoni mwake ni kuwahurumia wanyama na upole juu yao.
- Katazo la kusulubu (kumtesa) mwanadamu baada ya kumuua.
- Uharamu wa kila chenye kumtesa mnyama.
Marejeo
صحيح مسلم (3/ 1548) (1955).
التحفة الربانية في شرح الأربعين حديثا النووية (ص38).
شرح الأربعين النووية، لابن عثيمين (ص185).
فتح القوي المتين في شرح الأربعين وتتمة الخمسين، للعباد (ص65).
فتح الباري، لابن حجر (9/ 644).
شرح النووي على مسلم (13/ 107).
Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com