Ruka hadi kwenye maudhui
Hadithi zenye maelezo

Kulikuwa na mtu akiwakopesha watu,basi alikuwa akisema kumwambia kijana wake (Akienda kudai): Ukifika kwa mwenye hali ngumu, basi msamehe, huenda nasi Allah akatusamehe

عن أبي هريرة رضي الله عنه أن رسول الله صلى الله عليه وسلم قال: «كان رجلٌ يُدَايِنُ الناسَ، فكان يقول لفتاه: إذا أتيتَ مُعسِرًا فتجاوز عنه، لعل اللهَ يَتجاوزُ عنا، فلقي اللهَ فتجاوز عنه».
Imepokelewa Kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake-yakwamba Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Kulikuwa na mtu akiwakopesha watu,basi alikuwa akisema kumwambia kijana wake (Akienda kudai): Ukifika kwa mwenye hali ngumu, basi msamehe, huenda nasi Allah akatusamehe (alipokufa) akakutana na Allah, akamsamehe".
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeDarajaSahihi
Maelezo

Anaeleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: Kuhusu bwana mmoja aliyekuwa akiamiliana na watu kwa mkopo, au akiwauzia kwa mkopo, Na alikuwa akisema kumwambia kijana wake aliyekuwa akikusanya madeni yaliyoko kwa watu: Utakapomwendea mdaiwa na akawa hana cha kulipa deni analodaiwa kwa sababu ya kushindwa "Basi, msamehe"; Ima kwa kumpa muda zaidi na kutong'ang'ania kumdai, Au kwa kukubali alichonacho hata kama kina mapungufu, na hiyo ni kwa hamu yake na tamaa yake ya kutaka Allah asimuadhibu na amsamehe, Alipofariki Allah akamsamehe na hakumuadhibu kwa makosa yake mengine.

Mafunzo
  1. Wema katika kuamiliana na watu na kuwasamehe na kumpa uhuru mwenye hali ngumu ni katika sababu kubwa za mja kusalimika siku ya Kiyama.
  2. Kuwafanyia wema viumbe na kutakasa matendo kwa ajili ya Allah na kutaraji katika rehema zake ni katika sababu za kupata msamha wa madhambi.
Marejeo

صحيح البخاري (4/ 176) (3480). صحيح مسلم (3/ 1196) (1562). بهجة الناظرين شرح رياض الصالحين، لسليم الهلالي (2/ 458). التنوير شرح الجامع الصغير، للصنعاني (8/ 123). كنوز رياض الصالحين، لمجموعة من الباحثين (16/ 402). مرقاة المفاتيح شرح مشكاة المصابيح، للقاري (5/ 1953). نزهة المتقين شرح رياض الصالحين (2/ 945).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com
Tabia njema.

Kila hadithi, daraja, maelezo na funzo hapa vinaonyeshwa kama HadeethEnc.com inavyovichapisha, kwa masharti yake ya kuchapisha upya. Daraja halimtaji aliyelitoa. Tafsiri na maelezo ni ya waandishi wake wenyewe, na baadhi hutaja hukumu; wahakiki wa Sabīl hawajavichunguza. Hadithi ya Kiarabu ndiyo matini. Chanzo: HadeethEnc.com