Ruka hadi kwenye maudhui
Hadithi zenye maelezo

Atakayeelekeza katika jambo la kheri basi atapata malipo mfano wa malipo ya mfanyaji wake

عن أبي مسعود الأنصاري رضي الله عنه قال: جَاءَ رَجُلٌ إِلَى النَّبِيِّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ فَقَالَ: إِنِّي أُبْدِعَ بِي فَاحْمِلْنِي، فَقَالَ: «مَا عِنْدِي»، فَقَالَ رَجُلٌ: يَا رَسُولَ اللهِ، أَنَا أَدُلُّهُ عَلَى مَنْ يَحْمِلُهُ، فَقَالَ رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: «مَنْ دَلَّ عَلَى خَيْرٍ فَلَهُ مِثْلُ أَجْرِ فَاعِلِهِ».
Kutoka kwa Abuu Masoud Al-Answari -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Alikuja mtu mmoja kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akasema: Hakika kipandwa changu kimeangamia nakuomba msaada wa usafiri, akasema: "Sina uwezo" Mtu mmoja akasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, mimi nitamuonyesha kwa mtu atakayeweza kumbeba, akasema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: "Atakayeelekeza katika jambo la kheri basi atapata malipo mfano wa malipo ya mfanyaji wake".
Imepokelewa Imamu MuslimDarajaSahihi
Maelezo

Alikuja mtu mmoja kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akasema: Hakika mimi kimeangamia kipandwa changu, nipe msaada, na unipe kipandwa kitakachonifikisha, Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akampa udhuru yakuwa yeye hana kitu cha kumsaidia, mtu mmoja akasema na alikuwepo katika mazungumzo: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, mimi nitamuelekeza kwa mtu atakaye mbeba, akaeleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa yeye atashiriki katika kupata malipo na mtoaji, kwa sababu amemuelekeza muhitaji kwake.

Mafunzo
  1. Himizo la kuelekeza katika kheri.
  2. Himizo la kufanya kheri ni katika sababu za kuinyanyua jamii ya kiislamu na kutoshelezana.
  3. Upana wa fadhila za Mwenyezi Mungu Mtukufu.
  4. Hadithi hii ni kanuni kuu, yanaingia hapa matendo yote ya kheri.
  5. Mtu atakaposhindwa kutimiza hitajio la muombaji, basi amuelekeze kwa mwingine.
Marejeo

صحيح مسلم (3/ 1506) (1893). شرح النووي على مسلم (11/ 166). توضيح الأحكام من بلوغ المرام، للبسام (7/ 349). فتح ذي الجلال والاكرام بشرح بلوغ المرام، لابن عثيمين (6/ 298).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com
Tabia njema.

Kila hadithi, daraja, maelezo na funzo hapa vinaonyeshwa kama HadeethEnc.com inavyovichapisha, kwa masharti yake ya kuchapisha upya. Daraja halimtaji aliyelitoa. Tafsiri na maelezo ni ya waandishi wake wenyewe, na baadhi hutaja hukumu; wahakiki wa Sabīl hawajavichunguza. Hadithi ya Kiarabu ndiyo matini. Chanzo: HadeethEnc.com