Ruka hadi kwenye maudhui
Hadithi zenye maelezo

Sifa za pepo na moto.

Hadithi 28

Ataletwa mtu siku ya Kiyama, kisha atupwe motoni, ujiviringishe utumbo na vyote vilivyomo tumboni mwake, atazunguka nao (motoni) kama punda anavyozunguka na jiwe la kusagia nafaka

عَنْ أُسَامَةَ بْنِ زَيْدٍ رضي الله عنه قَالَ: قِيلَ لَهُ: أَلَا تَدْخُلُ عَلَى عُثْمَانَ فَتُكَلِّمَهُ؟ فَقَالَ: أَتَرَوْنَ أَنِّي لَا أُكَلِّمُهُ إِلَّا أُسْمِعُكُمْ؟ وَاللهِ لَقَدْ كَلَّمْتُهُ فِيمَا بَيْنِي وَبَيْنَهُ، مَا دُونَ أَنْ أَفْتَتِحَ أَمْرًا لَا أُحِبُّ أَنْ أَكُونَ أَوَّلَ مَنْ فَتَحَهُ، وَلَا أَقُولُ لِأَحَدٍ يَكُونُ عَلَيَّ أَمِيرًا: إِنَّهُ خَيْرُ النَّاسِ بَعْدَمَا سَمِعْتُ رَسُولَ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ يَقُولُ: «يُؤْتَى بِالرَّجُلِ يَوْمَ الْقِيَامَةِ، فَيُلْقَى فِي النَّارِ، فَتَنْدَلِقُ أَقْتَابُ بَطْنِهِ، فَيَدُورُ بِهَا كَمَا يَدُورُ الْحِمَارُ بِالرَّحَى، فَيَجْتَمِعُ إِلَيْهِ أَهْلُ النَّارِ، فَيَقُولُونَ: يَا فُلَانُ مَا لَكَ؟ أَلَمْ تَكُنْ تَأْمُرُ بِالْمَعْرُوفِ، وَتَنْهَى عَنِ الْمُنْكَرِ؟ فَيَقُولُ: بَلَى، قَدْ كُنْتُ آمُرُ بِالْمَعْرُوفِ وَلَا آتِيهِ، وَأَنْهَى عَنِ الْمُنْكَرِ وَآتِيهِ».
Kutoka kwa Osama bin Zaidi radhi za Allah ziwe juu yake: Aliambiwa: Je, huingii kwa Othman uzungumze naye? Akasema: Hivi mnadhani kuwa mimi siwezi kumsemesha jambo mpaka nanyi msikie? Wallahi nimekwishamsemesha kwa mambo yaliyo kati yangu na yeye, na wala sitaki kufungua jambo ambalo sihitaji kuwa wa mwanzo kulifungua, na wala sitaki kumueleza yeyote awe kiongozi kwangu: Hakika yeye ni kiongozi baada yakuwa nimemsikia Mtume rehema na amani ziwe juu yake akisema: "Ataletwa mtu siku ya Kiyama, kisha atupwe motoni, ujiviringishe utumbo na vyote vilivyomo tumboni mwake, atazunguka nao (motoni) kama punda anavyozunguka na jiwe la kusagia nafaka, watamkusanyikia watu wa motoni, watamuuliza: We fulani umepatwa na nini? Hivi si ni wewe ulikuwa ukituamrisha mema na kutukataza maovu? Atasema: Ndiyo ni mimi, ila nilikuwa nikiamrisha mema wala siyafanyi, na nikikataza maovu ninayafanya".
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeDarajaSahihi
Maelezo

Aliambiwa Osama bin Zaid Mwenyezi Mungu awawie radhi wote wawili: Hivi huendi kwa Othman bin Affan, Mwenyezi Mungu amuwie radhi, ukamwambia kuhusu fitina zilizotokea baina ya watu na kutafuta kuzizima. Basi akawaeleza kuwa alizungumza naye kwa siri ili kutafuta maslahi, si kuchochea kwa fitina, na lengo lake lilikuwa kwamba hataki kuwashutumu viongozi hadharani, ikawa ni sababu ya kurefusha mzozo kwa kiongozi, na ni mlango wa fitina na uovu, na siwezi kuwa wa kwanza kuufungua. Kisha Osama Mwenyezi Mungu awawie radhi, akasema kuwa: Anawanasihi viongozi kwa siri na wala hambembelezi yeyote kwa kumsifu, hata akiwa kiongozi, na wala hawabembelezi kwa kuwasifu kwa uongo, na hiyo ni baada ya yeye kuwa alisikia kutoka kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa ataletwa mtu Siku ya Kiyama na kutupwa Motoni, na utumbo wake utatoka nje ya tumbo lake kutokana na ukali wa adhabu, na atasokota utumbo wake katika hali hii Motoni kama punda anayezunguka jiwe lake la kusagia nafaka, watu wa Motoni watamzunguka kwa duara kisha watamuuliza: Ewe fulani, je si wewe aliyekuwa ukiamrisha mema na kukataza maovu?! Atasema: Mimi nilikuwa nikiamrisha mema na wala siyafanyi, na ninakataza maovu na ninayafanya.

Mafunzo
  1. Asili katika kuwanasihi viongozi inatakiwa iwe kwa siri, na mtu asizizungumze kwa watu wote.
  2. Ahadi ya adhabu kali kwa atakayekwenda kinyume matendo yake na kauli zake
  3. Kua na adabu na viongozi na kuwa wapole kwao, na kuwaamrisha mema na kuwakataza maovu.
  4. Ubaya wa kujipendekeza kwa viongozi katika haki na kudhihirisha kinyume na kile kinachoonekana kama kujipendekeza kwa uongo.
Marejeo

صحيح البخاري (4/ 121) (3267). صحيح مسلم (4/ 2290) (2989). كنوز رياض الصالحين، لمجموعة من الباحثين (4/ 143). شرح رياض الصالحين، لابن عثيمين (2/ 358). تطريز رياض الصالحين، لفيصل آل مبارك (ص156). نزهة المتقين شرح رياض الصالحين، لمجموعة من الباحثين (1/ 220).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Hili ni jiwe lililotupwa Motoni muda wa (miaka) sabini iliyopita, na sasa linaanguka Motoni mpaka litafika katika kina chake

عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رضي الله عنه قَالَ: كُنَّا مَعَ رَسُولِ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، إِذْ سَمِعَ وَجْبَةً، فَقَالَ النَّبِيُّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: «تَدْرُونَ مَا هَذَا؟» قَالَ: قُلْنَا: اللهُ وَرَسُولُهُ أَعْلَمُ، قَالَ: «هَذَا حَجَرٌ رُمِيَ بِهِ فِي النَّارِ مُنْذُ سَبْعِينَ خَرِيفًا، فَهُوَ يَهْوِي فِي النَّارِ الْآنَ حَتَّى انْتَهَى إِلَى قَعْرِهَا».
Kutoka kwa Abuu Huraira -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- amesema: Tulikuwa pamoja na Mtume rehema na amani ziwe juu yake ghafla akasikia kishindo, akasema Mtume rehema na amani ziwe juu yake: “Je, mnajua ni nini hiki?” Akasema: Tukasema: Mwenyezi Mungu na Mtume wake wanajua zaidi, akasema: «Hili ni jiwe lililotupwa Motoni muda wa (miaka) sabini iliyopita, na sasa linaanguka Motoni mpaka litafika katika kina chake.
Imepokelewa Imamu MuslimDarajaSahihi
Maelezo

Mtume rehema na amani ziwe juu yake alisikia sauti ya kushtua kama kuanguka kwa mwili, akawauliza Masahaba aliokuwa nao Mwenyezi Mungu awawie radhi kuhusu sauti hiyo, wakasema: Mwenyezi Mungu na Mtume wake ndio wajuzi zaidi. Akawaambia rehema na amani ziwe juu yake: Sauti hii mliyoisikia ni ya jiwe lililorushwa kutoka ukingo wa Jahannam miaka sabini iliyopita lilikuwa likiporomoka na kuanguka humo, hivi sasa mliposikia kishindo ndio limefika katika kina chake.

Mafunzo
  1. Himizo la kujiandaa na siku ya mwisho kwa amali njema, na kutahadhari na Jahannam.
  2. Ni sunna kuiegemeza elimu kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu katika yale ambayo mtu hana elimu nayo.
  3. Mwalimu anatakiwa kuamsha hisia na umakini kwa wanafunzi kabla ya kuwaeleza; ili uwe ni msukumo wa wao kuelewa.
Marejeo

صحيح مسلم (4/ 2184) (2844). بهجة الناظرين شرح رياض الصالحين، لسليم الهلالي (1/ 476). نزهة المتقين شرح رياض الصالحين، لمجموعة من الباحثين (1/ 369). كنوز رياض الصالحين، لمجموعة من الباحثين (6/ 414).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Nilikuwa kwa Saidi bin Jubair akasema: Ni nani kati yenu aliyeiona nyota iliyodondoka jana usiku? Nikasema: Mimi, kisha nikasema: Ama mimi sikuwa katika swala, lakini niling'atwa (na Nge)

عن حُصين بن عبد الرحمن قال: كنتُ عند سعيد بن جُبير فقال: أيكم رأى الكوكب الذي انقَضَّ البارحة؟ فقلتُ: أنا، ثم قلتُ: أما إني لم أكن في صلاة، ولكني لُدغْتُ، قال: فما صنعتَ؟ قلت: ارتقيتُ، قال: فما حَمَلك على ذلك؟ قلت: حديث حدَّثَناه الشعبي، قال: وما حدَّثَكم؟ قلتُ حدثنا عن بريدة بن الحُصيب أنه قال: "لا رُقْية إلا مِن عَيْن أو حُمَة"، قال: قد أحسَن مَن انتهى إلى ما سمع، ولكن حدثنا ابن عباس عن النبي صلى الله عليه وسلم أنه قال: "عُرضت عليّ الأُمم، فرأيتُ النبي ومعه الرَّهط والنبي ومعه الرجل والرجلان، والنبي وليس معه أحد، إذ رُفع لي سواد عظيم فظننتُ أنهم أمَّتي، فقيل لي: هذا موسى وقومه، فنظرتُ فإذا سواد عظيم، فقيل لي: هذه أمَّتك، ومعهم سبعون ألفا يدخلون الجنة بغير حساب ولا عذاب، ثم نهض فدخل منْزله، فخاض الناس في أولئك؛ فقال بعضهم: فلعلهم الذين صحِبوا رسول الله صلى الله عليه وسلم وقال بعضهم: فلعلهم الذين وُلِدُوا في الإسلام فلم يشركوا بالله شيئا، وذكروا أشياء، فخرج عليهم رسول الله صلى الله عليه وسلم فأخبروه، فقال: هم الذين لا يَسْتَرقون، ولا يَكْتَوُون، ولا يَتَطَيَّرون، وعلى ربهم يتوكلون، فقام عُكاشة بن مِحصَن فقال: ادع الله أن يجعلني منهم، قال: أنت منهم، ثم قام جل آخر فقال: ادع الله أن يجعلني منهم، فقال: سَبَقَك بها عكاشة".
Kutoka kwa Huswain bin Abdirrahman amesema: Nilikuwa kwa Saidi bin Jubair akasema: Ni nani kati yenu aliyeiona nyota iliyodondoka jana usiku? Nikasema: Mimi, kisha nikasema: Ama mimi sikuwa katika swala, lakini niling'atwa na Nge, akasema: nini ulifanya? nikasema: nilijisomea Ruqya, akasema: Ni nini kilikupelekea kufanya hivyo? Nikasema: Ni hadithi aliyotuhadithia Sha'abiy, akasema: Aliwahadithia nini? Nikasema: Alituhadithia kutoka kwa Buraida bin Huswaib yakwamba yeye amesema:"Hakuna kisomo cha ruqya isipokuwa kwa kijicho au homa", Akasema: Amefanya vizuri aliyeishia pale aliposikia, lakini alituhadithia sisi bin Abbasi kutoka kwa Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- Amesema: "Nilikusanyiwa mimi Ummati, nikamuona Nabii akiwa pamoja na kundi na Nabii akiwa pamoja na mtu mmoja na watu wawili, Na Nabii akiwa hana hata mtu mmoja, Ghafla ukanyanyuliwa kwangu weusi mkubwa, nikadhania kuwa hao ni umma wangu, nikaambiwa: Huyu ni Musa na watu wake, nikatazama tena, Ghafla nikaona weusi mkubwa, nikaambiwa: Huu ni umma wako, Ukiwa pamoja na watu elfu sabini wanaingia peponi bila hesabu wala adhabu, kisha akanyanyuka akaingia nyumbani kwake, watu wakazungumza mengi kuhusu watu hao (wanaoingia peponi bila hesabu wala adhabu); Wakasema baadhi yao: Huenda hao ni wale waliosuhubiana (walioambatana) na Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- Na wakasema baadhi yao: Huenda hao ni wale waliozaliwa katika uislamu na wakawa hawakumshirikisha Mwenyezi Mungu na chochote, Na wakataja mambo mengi! Basi akatoka kwao Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- wakamueleza, Akasema: Hao ni wale ambao hawaombi watu kuwasomea ruqya, na wala hawajitibu kwa moto, na wala hawaamini mikosi ya ndege, na kwa Mola wao ndiko wanakotegemea, hapo akasimama (bwana mmoja akiitwa) Ukasha bin Mihswani akasema: Muombe Mwenyezi Mungu anifanye kuwa miongoni mwao, akasema: Wewe ni miongoni mwao, kisha akasimama mtu mwingine akasema: Muombe Mwenyezi Mungu anifanye kuwa miongoni mwao, Akasema: kakutangulia kwa hilo Ukasha".
Wamekubaliana Bukhaariy na MuslimDarajaSahihi
Maelezo

Anatueleza Huswain bin Abdirrahman -Mwenyezi Mungu amrehemu- kuhusu mazungumzo yaliyojiri kati yake na Saidi bin Jubair -Mwenyezi Mungu amrehemu- kuhusu swala la kisomo cha Ruqya,Na hiyo ni kwasababu Huswain aling'atwa na nge na akajisomea kwaajili ya hilo ruqya ya kisheria, na alipomuuliza Saidi kuhusu ushahidi wake akamueleza kwa hadithi ya Sha'biy ambayo ina halalisha ruqya kwasababu ya kijicho au sumu,Saidi akamsifia kwa hilo,lakini yeye akampokelea hadithi ambayo inayopendekeza kuacha kufanya ruqya, nayo ni hadithi ya bin Abbasi ambayo inaambatana na sifa Nne ambazo atakayesifika nazo atastahiki kuingia peponi bila hesabu wala adhabu, nazo ni kutotafuta kisomo cha ruqya, na kutojitibu kwa moto,na kutoamini mikosi, na ukweli wa kutegemea kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu,na alipoomba Ukasha toka kwa Nabii-Rehema na Amani ziwe juu yake- kuwa amuombee ili awe miongoni mwao akamueleza kuwa yeye ni miongoni mwao,na aliposimama mtu mwingine kwa lengo hilo hilo akamjibu kwa upole Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- kwa kumzuilia hilo na kwa kufunga mlango na kukata muendelezo wa watu wengine.

Marejeo

-صحيح البخاري، المحقق: محمد زهير بن ناصر الناصر، الناشر: دار طوق النجاة (مصورة عن السلطانية بإضافة ترقيم محمد فؤاد عبد الباقي)، الطبعة: الأولى، 1422ه. -صحيح مسلم، المحقق: محمد فؤاد عبد الباقي - الناشر: دار إحياء التراث العربي - بيروت. -الملخص في شرح كتاب التوحيد، دار العاصمة، الرياض، الطبعة: الأولى، 1422ه - 2001م. -الجديد في شرح كتاب التوحيد، مكتبة السوادي، جدة، المملكة العربية السعودية، الطبعة: الخامسة، 1424هـ - 2003م.

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

, atamuingiza Mwenyezi Mungu peponi kulingana na yale aliyokuwa nayo katika matendo

عَنْ عُبَادَةَ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ عَنِ النَّبِيِّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: «مَنْ شَهِدَ أَنْ لَا إِلَهَ إِلَّا اللهُ وَحْدَهُ لَا شَرِيكَ لَهُ، وَأَنَّ مُحَمَّدًا عَبْدُهُ وَرَسُولُهُ، وَأَنَّ عِيسَى عَبْدُ اللهِ وَرَسُولُهُ وَكَلِمَتُهُ أَلْقَاهَا إِلَى مَرْيَمَ وَرُوحٌ مِنْهُ، وَالْجَنَّةُ حَقٌّ، وَالنَّارُ حَقٌّ، أَدْخَلَهُ اللهُ الْجَنَّةَ عَلَى مَا كَانَ مِنَ الْعَمَلِ».
Kutoka kwa Ubada bin -Radhi za Allah ziwe juu yake- kutoka kwa Mtume Rehema na amani za Allah ziwe juu yake amesema: "Atakaye shuhudia kuwa hapana Mola isipokuwa Mwenyezi Mungu yeye pekee asiye na mshirika nakuwa Muhammadi ni mjumbe wake na ni mja wake, nakuwa Issa ni mja wa Mwenyezi Mungu na Mtume wake na neno lake alilolipeleka kwa Mariam na ni roho toka kwake, na pepo ni kweli na moto ni kweli, atamuingiza Mwenyezi Mungu peponi kulingana na yale aliyokuwa nayo katika matendo".
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeDarajaSahihi
Maelezo

Anatueleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- yakuwa atakayetamka neno la tauhidi kwa kujua maana yake, kwa kuyafanyia kazi madhumuni yake, na akashuhudia utumwa wa Muhammadi -Rehema na amani ziwe juu yake- na ujumbe wake, na akakiri utumwa wa Issa na ujumbe wake, Na kuwa Mwenyezi Mungu alimuumba kwa kauli yake "Kuwa" na akawa, na kuwa yeye ni roho miongoni mwa roho alizoziumba Mwenyezi Mungu, Na akamtenga mbali mama yake kwa yale waliyomnasibisha nayo Mayahudi, Nakuwa atakayeamini pepo kuwa ni kweli, na kuwa Moto ni kweli, akaitakidi uwepo wake, nakuwa hizo ni neema za Mwenyezi Mungu na adhabu yake, Na atakayekufa katika imani hiyo; basi mafikio yake ni Peponi hata kama alikuwa mzembe katika ibada, na anamadhambi.

Mafunzo
  1. Mwenyezi Mungu Mtukufu kamuumba Issa mwana wa Mariamu kwa neno (Kuwa) bila baba.
  2. Kinachowakusanya pamoja kati ya Issa (Yesu) na Muhammadi amani iwe juu yao wote ni kuwa ni waja wa Mwenyezi Mungu na Mitume wake, basi wao wote wawili ni Mitume hawasemi uongo, na ni waja wala hawaabudiwi.
  3. Ubora wa tauhidi na kufuta kwake madhambi, nakuwa mafikio ya mtu wa tauhidi ni Peponi, hata kama yakajitokeza kwake baadhi ya madhambi.
Marejeo

صحيح البخاري (4/ 165) (3435). صحيح مسلم (1/ 57) (28). الملخص في شرح كتاب التوحيد، لصالح الفوزان (ص25). الجديد في شرح كتاب التوحيد، لمحمد القرعاوي (ص36).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Atakayekutana na Mwenyezi Mungu akiwa hamshirikishi na chochote basi ataingia Peponi, na atakayekutana naye akimshirikisha ataingia Motoni

عن جابر بن عبد الله رضي الله عنهما قال: سمعت رسول الله صلى الله عليه وسلم يقول: «مَنْ لَقِيَ اللهَ لَا يُشْرِكُ بِهِ شَيْئًا دَخَلَ الْجَنَّةَ، وَمَنْ لَقِيَهُ يُشْرِكُ بِهِ دَخَلَ النَّارَ».
Imepokelewa Kutoka kwa Jabiri bin Abdillah -Radhi za Allah ziwe juu yao- amesema: Nilimsikia Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akisema: "Atakayekutana na Mwenyezi Mungu akiwa hamshirikishi na chochote basi ataingia Peponi, na atakayekutana naye akimshirikisha ataingia Motoni".
Imepokelewa Imamu MuslimDarajaSahihi
Maelezo

Anaeleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa mwenye kufa hali yakuwa hamshirikishi Mwenyezi Mungu na chochote basi mafikio yake ni katika Pepo hata kama ataadhibiwa kwa baadhi ya madhambi yake, nakuwa atakayekufa hali yakuwa anamshirikisha Mwenyezi Mungu na chochote atabakizwa milele Motoni.

Mafunzo
  1. Ubora wa tauhidi, nakuwa ni sababu ya kuokoka na kukaa milele Motoni.
  2. Ukaribu wa Pepo na Moto kwa mja nakuwa hakuna baina yake na hivyo viwili isipokuwa kifo.
  3. Tahadhari inatolewa ya kujiepusha na ushirikina mdogo au mkubwa, kwa sababu kuokoka na moto ni kwa kuuepuka.
  4. Mazingatio katika matendo huangaliwa mwisho wake.
Marejeo

صحيح مسلم (1/ 94) (93). الملخص في شرح كتاب التوحيد، لصالح الفوزان (ص49). الجديد في شرح كتاب التوحيد، لمحمد القرعاوي (ص60).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Yeyote atakayenidhaminia mimi vilivyo kati ya Taya mbili na vilivyo kati ya miguu yake ninampa dhamana ya Pepo

عن سهل بن سعد رضي الله عنه عن رسول الله صلى الله عليه وسلم قال: «مَنْ يَضْمَنْ لِي مَا بَيْنَ لَحْيَيْهِ وَمَا بَيْنَ رِجْلَيْهِ أَضْمَنْ لَهُ الْجَنَّةَ».
Imepokelewa Kutoka kwa Sahal Ibn Sa'd -Radhi za Allah ziwe juu yake- kutoka kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: "Yeyote atakayenidhaminia mimi vilivyo kati ya Taya mbili na vilivyo kati ya miguu yake ninampa dhamana ya Pepo".
Imepokelewa na Al-BukhaariyDarajaSahihi
Maelezo

Anaeleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuhusu mambo mawili nayo muislamu basi ataingia Peponi, La kwanza: Kuhifadhi ulimi kutozungumza yale yenye kumchukiza Allah Mtukufu, La pili: Kuhifadhi tupu kutotumbukia katika machafu; Kwa sababu viungo viwili hivi hukithiri kutokea maasi kwavyo.

Mafunzo
  1. Kuhifadhi ulimi na tupu ni njia ya kuingia Peponi.
  2. Umetajwa mahususi ulimi na utupu; kwa sababu ndio vyanzo vikuu vya balaa kwa mwanadamu katika dunia na Akhera.
Marejeo

صحيح البخاري (8/ 100) (6474). بهجة الناظرين شرح رياض الصالحين، تأليف سليم الهلالي (3/ 9). نزهة المتقين شرح رياض الصالحين، تأليف د. مصطفى الخِن وغيره (2/ 1035). كنوز رياض الصالحين، لمجموعة من الباحثين (18/ 85). شرح رياض الصالحين، لابن عثيمين (6/ 117). إرشاد الساري لشرح صحيح البخاري، للقسطلاني (9/ 272).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Pepo iko karibu mno kwa mmoja wenu kuliko umbali wa kanyagio la kiatu na kisigino chake, na moto pia hivyo hivyo

عن ابن مسعود رضي الله عنه قال: قال النبي صلى الله عليه وسلم: «الْجَنَّةُ أَقْرَبُ إِلَى أَحَدِكُمْ مِنْ شِرَاكِ نَعْلِهِ، وَالنَّارُ مِثْلُ ذَلِكَ».
Imepokelewa Kutoka kwa Ibn Masoud -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: amesema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: "Pepo iko karibu mno kwa mmoja wenu kuliko umbali wa kanyagio la kiatu na kisigino chake, na moto pia hivyo hivyo".
Imepokelewa na Al-BukhaariyDarajaSahihi
Maelezo

Alieleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa Pepo na Moto viko karibu mno na mwanadamu kama ukaribu wa mwendo wa kiatu unaokuwa juu ya kisigino, kwa sababu anaweza kufanya twa'a (ibada) katika yale yanayomridhisha Allah Mtukufu akaingia Peponi kwa ibada hiyo, au dhambi moja likawa sababu ya kuingia motoni.

Mafunzo
  1. Himizo la kufanya heri hata kama ni ndogo, na tishio la kufanya shari hata kama ni ndogo.
  2. Ni lazima muislamu katika maisha yake kukusanya kati ya kutaraji mazuri na kuogopa adhabu, na kumuomba Allah Mtukufu muda wote kuthubutu (Kudumu) katika haki mpaka asalimike na wala asihadaike na hali aliyonayo.
Marejeo

صحيح البخاري (8/ 102) (6488). شرح رياض الصالحين، لابن عثيمين (2/ 99). فتح الباري، لابن حجر(11/ 321). بهجة الناظرين شرح رياض الصالحين، لسليم الهلالي (1/ 186). نزهة المتقين شرح رياض الصالحين، لمصطفى الخِن وغيره (1/ 136).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Hakika peponi kuna daraja mia moja kaziandaa Mwenyezi Mungu kwaajili ya wenye kupigana katika njia ya Mwenyezi Mungu kati ya daraja mbili ni kama masafa ya baina ya mbingu na ardhi

عن أبي هريرة رضي الله عنه أن رسول الله صلى الله عليه وسلم قال: «إنَّ في الجنَّة مائةَ دَرَجَة أعَدَّهَا الله للمُجاهِدين في سَبِيل الله ما بَيْنَ الدَّرَجَتَيْنِ كما بين السماء والأرض».
Kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- yakwamba Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- Amesema: "Hakika peponi kuna daraja mia moja kaziandaa Mwenyezi Mungu kwaajili ya wenye kupigana katika njia ya Mwenyezi Mungu kati ya daraja mbili ni kama masafa ya baina ya mbingu na ardhi".
Imepokelewa na Al-BukhaariyDarajaSahihi
Maelezo

Anaeleza Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- katika hadithi hii kuhusu fadhila za wenye kupigana katika njia yake nakuwa Mwenyezi Mungu kawaandalia peponi daraja mia moja, masafa kati ya daraja mbili ni kama yaliyo baina ya mbingu na ardhi.

Marejeo

- رياض الصالحين من كلام سيد المرسلين؛ للإمام أبي زكريا النووي، تحقيق د. ماهر الفحل، دار ابن كثير-دمشق، الطبعة الأولى، 1428ه. صحيح البخاري -للإمام أبي عبد الله محمد بن إسماعيل البخاري، عناية محمد زهير الناصر، دار طوق النجاة، الطبعة الأولى، 1422هـز - بهجة الناظرين شرح رياض الصالحين؛ تأليف سليم بن عيد الهلالي، دار ابن الجوزي- الطبعة الأولى1418ه. - نزهة المتقين شرح رياض الصالحين؛ تأليف د. مصطفى الخِن وغيره، مؤسسة الرسالة-بيروت، الطبعة الرابعة عشرة، 1407هـ. - شرح رياض الصالحين؛ للشيخ محمد بن صالح العثيمين، مدار الوطن، الرياض، 1426هـ. -شرح صحيح البخارى لابن بطال الأندلسي،تحقيق: أبو تميم ياسر بن إبراهيم مكتبة الرشد - السعودية، الرياض الطبعة: الثانية، 1423هـ - 2003م.

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com
8 kati ya 28
Hadithi 28
  1. Ataletwa mtu siku ya Kiyama, kisha atupwe motoni, ujiviringishe utumbo na vyote vilivyomo tumboni mwake, atazunguka nao (motoni) kama punda anavyozunguka na jiwe la kusagia nafaka
  2. Hili ni jiwe lililotupwa Motoni muda wa (miaka) sabini iliyopita, na sasa linaanguka Motoni mpaka litafika katika kina chake
  3. Nilikuwa kwa Saidi bin Jubair akasema: Ni nani kati yenu aliyeiona nyota iliyodondoka jana usiku? Nikasema: Mimi, kisha nikasema: Ama mimi sikuwa katika swala, lakini niling'atwa (na Nge)
  4. , atamuingiza Mwenyezi Mungu peponi kulingana na yale aliyokuwa nayo katika matendo
  5. Atakayekutana na Mwenyezi Mungu akiwa hamshirikishi na chochote basi ataingia Peponi, na atakayekutana naye akimshirikisha ataingia Motoni
  6. Yeyote atakayenidhaminia mimi vilivyo kati ya Taya mbili na vilivyo kati ya miguu yake ninampa dhamana ya Pepo
  7. Pepo iko karibu mno kwa mmoja wenu kuliko umbali wa kanyagio la kiatu na kisigino chake, na moto pia hivyo hivyo
  8. Hakika peponi kuna daraja mia moja kaziandaa Mwenyezi Mungu kwaajili ya wenye kupigana katika njia ya Mwenyezi Mungu kati ya daraja mbili ni kama masafa ya baina ya mbingu na ardhi
  9. Moto umezingirwa na yenyekutamanisha, na Pepo imezingirwa na yenyekuchukiza
  10. Atakayetoa vitu vya namna mbili katika njia ya Mwenyezi Mungu huitwa katika milango ya pepo, ewe mja wa Mwenyezi Mungu hii ni kheri, atakayekuwa miongoni mwa watu wa swala ataitwa katika mlango wa swala, atakayekuwa katika watu wa jihadi ataitwa katika mlango wa jihadi
  11. Ewe baba Saidi, yeyote atakayeridhia kuwa Mwenyezi Mungu ndiye Mola, na Uislamu kuwa ndiyo dini, na Muhammadi kuwa ni Nabii, basi atakuwa kastahiki Pepo
  12. Hakika mtu mwenye adhabu nafuu katika watu wa motoni ni yule atakayekuwa na viatu viwili na soli mbili vitokanavyo na moto, utakuwa ukitokota kwa hivyo ubongo wake kama kinavyotokota chungu, hatoona kuwa kuna yeyote mwenye adhabu kali kuliko yeye, kumbe yeye ndiye ana adhabu nafuu kuliko wote
  13. Nilionyeshwa Pepo na Moto, katu sijawahi kuona katika kheri na shari mfano wa siku hiyo, na lau mngejua ninayoyajua basi mngelicheka kidogo na mngelia sana
  14. Aliulizwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuhusu mambo yatakayowaingiza watu peponi kwa wingi, akasema: "Ni uchamungu na tabia njema
  15. Atanadi mwenye kunadi: "Hakika, mtapata afya nzuri na wala hamtougua milele. Na hakika, mtakuwa hai na wala hamtokufa milele, na hakika mtakuwa vijana na wala hamtazeeka milele. Na hakika, mtastareheka na wala hamtapata shida yoyote milele
  16. Ni vyako vyote ulivyotamani, na mfano wake pamoja navyo
  17. “Mwenyezi Mungu, Aliyetakasika na Kutukuka, atawaambia watu wa Peponi: Enyi watu wa Peponi? Watasema: Labeka tumekuitikia na umetukuka, atasema: Je, mmeridhika? Watasema: Tuna nini mpaka tusiridhike hali yakuwa umetupa mambo ambayo hujampa yeyote katika viumbe wako?
  18. Wakati wakazi wa Peponi watakapoingia Peponi, Mwenyezi Mungu Aliyetakasika na kutukuka, atasema: "Je, mnataka kitu chochote niwazidishie?
  19. Hakika muumini peponi atakuwa na Hema moja la madini ya lulu lililo wazi urefu wake kwenda juu ni maili sitini, muumini humo atakuwa na wake, akiwazungukia na wala baadhi yao hawawaoni wenzao
  20. Hakika ndani ya Pepo kuna mti ambao anatembea aliyepanda kipando madhubuti chenye uimara na kasi kubwa ya kukimbia kwa muda wa miaka mia moja na haumalizi (kuuvuka) mti huo
  21. Hakika Peponi kuna Soko, watakuwa wakienda hapo kila siku ya Ijumaa
  22. Aina mbili za watu ni miongoni mwa watu wa motoni, sijawaona (katika zama zake Mtume), watu walio na mijeledi mithili ya mikia ya Ng'ombe wakiwapiga watu, na wanawake waliovaa na wako uchi, wanenguaji wakatikaji
  23. Enyi hadhara ya wanawake, toeni sadaka, kwani hakika mimi nilionyeshwa kuwa nyinyi ndio wengi katika watu wa motoni" Wanawake wakasema: Na ni kwa nini ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu? Akasema: "Mnazidisha sana kulaani (kutukana) na mnawapinga waume, na mimi sijapata kuona wapungufu wa akili na dini wenye kuweza kuteka moyo ya mwanaume makini kuliko nyinyi
  24. Amesema Allah Aliyetakasika na kutukuka: Nimewaandalia waja wangu wema, vitu ambavyo jicho halijawahi kuona, wala sikio kusikia, wala haijawahi kupita katika fikira ya moyo wa binadamu yeyote
  25. Mwenyezi Mungu alipoumba Pepo na Moto alimtuma Malaika Jibril -Amani iwe juu yake- aende peponi
  26. Mauti yataletwa yakiwa kama dume la Kondoo mwenye rangi mchanganyiko ya weusi na weupe
  27. Moto wenu wa Dunia ni sawa na sehemu tu ya sabini itokanayo na moto wa Jahannam
  28. Hakika kundi la kwanza la watu watakaoingia peponi watakuwa katika sura ya mwezi usiku wa tarehe kumi na tano, kisha wale wanaowafuata watakuwa katika sura ya nyota kali ing'aayo na iangazayo mbinguni

Kila hadithi, daraja, maelezo na funzo hapa vinaonyeshwa kama HadeethEnc.com inavyovichapisha, kwa masharti yake ya kuchapisha upya. Daraja halimtaji aliyelitoa. Tafsiri na maelezo ni ya waandishi wake wenyewe, na baadhi hutaja hukumu; wahakiki wa Sabīl hawajavichunguza. Hadithi ya Kiarabu ndiyo matini. Chanzo: HadeethEnc.com