Ameeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa mwenye kunadi atanadi kuwaita watu wa peponi wakiwa humo wakineemeka: Hakika leo hii mtapata afya na hamtaugua peponi kamwe, kwa namna yoyote ile yatakavyokuwa madogo maradhi hayo, na hakika mtapewa uhai wala hamtakufa humo milele hata usingizi pia hamtaupata ambao ndio kifo kidogo, na leo mtaishi humo mkiwa vijana na wala hamtozeeka humo milele, nakuwa mtaneemeka humo wala hamtohuzunika milele, na hiyo ni kauli yake Mtukufu: "Na wataitwa (waambiwe) hiyo mbele yenu ndio pepo mliyorithishwa kwa sababu ya yale mliyokuwa mkiyafanya" [Al-Araf: 43].
- Mambo makubwa yanayodhoofisha neema za maisha ya dunia vyovyote vile zitakavyokuwa kubwa na akastarehe kwa namna yoyote ni mambo manne: Maradhi, kifo, uzee, ugumu na huzuni inayosababishwa na hofu ya kumuogopa adui na umasikini na vita na mengineyo, na watu wa peponi watasalimika na hayo, ikawa kwao ni neema iliyotimia.
- Kutofautiana kwa neema za pepo na neema za dunia; kwa sababu neema za peponi hakutokuwa na hofu ndani yake, ama neema za dunia hazidumu na huambatana na maumivu na magonjwa.
- Himizo la kufanya amali njema ambazo hutumika kuzifikia neema za pepo.
صحيح مسلم (4/ 2182) (2837). بهجة الناظرين شرح رياض الصالحين، لسليم الهلالي (3/ 348). شرح رياض الصالحين، لابن عثيمين (6/ 732). نزهة المتقين شرح رياض الصالحين، لمجموعة من الباحثين (2/ 1292).