Ruka hadi kwenye maudhui
Hadithi zenye maelezo

Ni vyako vyote ulivyotamani, na mfano wake pamoja navyo

عَن أَبِي هُرَيْرَةَ رَضيَ اللهُ عنهُ عَنْ رَسُولِ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: «إِنَّ أَدْنَى مَقْعَدِ أَحَدِكُمْ مِنَ الْجَنَّةِ أَنْ يَقُولَ لَهُ: تَمَنَّ فَيَتَمَنَّى، وَيَتَمَنَّى، فَيَقُولُ لَهُ: هَلْ تَمَنَّيْتَ؟ فَيَقُولُ: نَعَمْ، فَيَقُولُ لَهُ: فَإِنَّ لَكَ مَا تَمَنَّيْتَ وَمِثْلَهُ مَعَهُ».
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira Allah amridhie kutoka kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake amesema: "Hakika, mwenye kiwango cha chini zaidi kati yenu katika Pepo ni kwamba ataambiwa: "Tamani!" Basi atatamani na atamani, na ataambiwa: "Je umeshatamani?" Atasema: "Nidyo." Ataambiwa: "Ni vyako vyote ulivyotamani, na mfano wake pamoja navyo."
Imepokelewa Imamu MuslimDarajaSahihi
Maelezo

Ameeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa mwenye nafasi na daraja ndogo zaidi kwa wale watakaoingia peponi, ataambiwa: Tamani, basi atatamani, na atatamani tena, mpaka atafikia mahali ataishiwa yote ya kutamani isipokuwa atayataja, hapo ataambiwa: Je, umetamani umefika mwisho? Atasema: Ndiyo, hapo ataambiwa: Basi ni vyako vyote ulivyotamani na mfano wake pamoja navyo.

Mafunzo
  1. Kutofautiana kwa nafasi za watu wa peponi.
  2. Kumebainishwa ukubwa wa karama ya Mwenyezi Mungu Mtukufu.
  3. Neema za peponi hazishii katika kitu maalumu, bali muumini atapata ndani yake kila anachokitamani na nafsi yake kuwa na hamu nacho, ikiwa ni fadhila na ukwasi na ukarimu kutoka kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu.
Marejeo

صحيح مسلم (1/ 167) (182). مرقاة المفاتيح شرح مشكاة المصابيح، لعلي القاري (9/ 3585). تطريز رياض الصالحين، لفيصل آل مبارك (ص1090). بهجة الناظرين شرح رياض الصالحين، لسليم الهلالي (3/ 348). نزهة المتقين شرح رياض الصالحين، لمجموعة من الباحثين (2/ 1292).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com
Maisha ya Akhera.

Kila hadithi, daraja, maelezo na funzo hapa vinaonyeshwa kama HadeethEnc.com inavyovichapisha, kwa masharti yake ya kuchapisha upya. Daraja halimtaji aliyelitoa. Tafsiri na maelezo ni ya waandishi wake wenyewe, na baadhi hutaja hukumu; wahakiki wa Sabīl hawajavichunguza. Hadithi ya Kiarabu ndiyo matini. Chanzo: HadeethEnc.com