Kutoka kwa Abdallah bin Masoud -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: amesema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akisema: "La kwanza litakalohukumiwa kati ya watu siku ya kiyama ni katika damu".
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeDarajaSahihi
Maelezo
Ameeleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa jambo la kwanza litakalohukumiwa baina ya watu katika dhulma zao wao kwa wao siku ya Kiyama: Itakuwa katika damu, kama kuua na kujeruhi.
Mafunzo
Ukubwa wa swala la damu, kwani siku zote jambo muhimu zaidi ndio hutangulizwa.
Dhambi huwa kubwa kulingana na madhara yanayojitokeza, na kuua nafsi isiyo na hatia ni katika madhara makubwa na hakuna kubwa zaidi yake isipokuwa ukafiri na kumshirikisha Mwenyezi Mungu Mtukufu.
Marejeo
صحيح البخاري (9/ 2) (6864).
صحيح مسلم (3/ 1304) (1678).
خلاصة الكلام شرح عمدة الأحكام، لفيصل آل مبارك (ص319).
تيسير العلام شرح عمدة الأحكام، للبسام (ص640).
الإلمام بشرح عمدة الأحكام، لإسماعيل الأنصاري (2/ 103).
Kutoka kwa Haritha bin Wahabi Al-Khuzaai radhi za Allah ziwe juu yake amesema: Nilimsikia Mtume rehema na amani ziwe juu yake akisema: "Hivi nisikuelezeni watu wa peponi? Kila mnyonge mwenye kujishusha, na lau kama angeliapia kwa Mwenyezi Mungu basi angelimuepusha (na kutopokea kiapo chake), hivi nisikuelezeni watu wa motoni? kila jeuri mkaidi mwenye kiburi".
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeDarajaSahihi
Maelezo
Alieleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake baadhi ya sifa za watu wa peponi na za watu wa motoni.
Asilimia kubwa ya watu wa peponi ni: "Kila mnyonge mwenye kujishusha", yaani: Mnyenyekevu mwenye kujishusha kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu, mwenye kuidhalilisha nafsi yake kwake, mpaka baadhi ya watu wakamdhoofisha na kumdharau, na huyu mwenye kujidhalilisha kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu lau kama ataapa kwa Mwenyezi Mungu kiapo cha kutamani jambo katika karama za Mwenyezi Mungu Mtukufu, basi Mwenyezi Mungu angemuepusha na kutopokea kiapo chake, na angelimtimizia alichokiapia na angelijibu ombi lake na dua yake.
Na asilimia kubwa ya watu wa motoni ni: Kila "Mkaidi" Naye ni fidhuli mkorofi mwingi wa ugomvi, au muovu asiyetii kwa kufata jambo la kheri, "Jeuri" Naye ni mwenye kiburi, mlafi, mwenye mwili mkubwa, mwenye kutembea kwa maringo, mwenye tabia mbaya, "Mwenye kufanya kiburi" kwa kuikataa kwake haki, na kwa kumdharau mtu mwingine.
Mafunzo
Himizo la kujipamba na sifa za watu wa peponi, na tahadhari ya kusifika kwa sifa za watu wa motoni.
Unyenyekevu unakuwa kwa Mwenyezi Mungu Aliyetakasika na kutukuka, na kwa amri zake na makatazo yake na kutii, na unakuwa kwa viumbe kwa kutojikweza juu yao.
Amesema bin Hajari: Makusudio yake nikuwa asilimia kubwa ya watu wa peponi ni hawa, kama ambavyo watu wengi wa motoni ni sehemu hii nyingine, na wala makusudio yake si kueleza watu wote wa motoni watakuwa na sifa hizi.
Marejeo
صحيح البخاري (6/ 159) (4918).
صحيح مسلم (4/ 2190) (2853).
كنوز رياض الصالحين، لمجموعة من الباحثين (5/ 5).
شرح رياض الصالحين، لابن عثيمين (3/ 47).
بهجة الناظرين شرح رياض الصالحين، لسليم الهلالي (1/ 340).
نزهة المتقين شرح رياض الصالحين، لمجموعة من الباحثين (1/ 264).
عن أبي هريرة رضي الله عنه أن رسول الله صلى الله عليه وسلم قال: «إنَّ في الجنَّة مائةَ دَرَجَة أعَدَّهَا الله للمُجاهِدين في سَبِيل الله ما بَيْنَ الدَّرَجَتَيْنِ كما بين السماء والأرض».
Kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- yakwamba Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- Amesema: "Hakika peponi kuna daraja mia moja kaziandaa Mwenyezi Mungu kwaajili ya wenye kupigana katika njia ya Mwenyezi Mungu kati ya daraja mbili ni kama masafa ya baina ya mbingu na ardhi".
Imepokelewa na Al-BukhaariyDarajaSahihi
Maelezo
Anaeleza Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- katika hadithi hii kuhusu fadhila za wenye kupigana katika njia yake nakuwa Mwenyezi Mungu kawaandalia peponi daraja mia moja, masafa kati ya daraja mbili ni kama yaliyo baina ya mbingu na ardhi.
Marejeo
- رياض الصالحين من كلام سيد المرسلين؛ للإمام أبي زكريا النووي، تحقيق د. ماهر الفحل، دار ابن كثير-دمشق، الطبعة الأولى، 1428ه.
صحيح البخاري -للإمام أبي عبد الله محمد بن إسماعيل البخاري، عناية محمد زهير الناصر، دار طوق النجاة، الطبعة الأولى، 1422هـز
- بهجة الناظرين شرح رياض الصالحين؛ تأليف سليم بن عيد الهلالي، دار ابن الجوزي- الطبعة الأولى1418ه.
- نزهة المتقين شرح رياض الصالحين؛ تأليف د. مصطفى الخِن وغيره، مؤسسة الرسالة-بيروت، الطبعة الرابعة عشرة، 1407هـ.
- شرح رياض الصالحين؛ للشيخ محمد بن صالح العثيمين، مدار الوطن، الرياض، 1426هـ.
-شرح صحيح البخارى لابن بطال الأندلسي،تحقيق: أبو تميم ياسر بن إبراهيم مكتبة الرشد - السعودية، الرياض الطبعة: الثانية، 1423هـ - 2003م.
عن أبي هريرة رضي الله عنه عن رسول الله صلى الله عليه وسلم قال: «إنه لَيَأتي الرَّجلُ السَّمين العظيم يوم القيامة لا يَزِنُ عند الله جَناح بَعُوضة».
Kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- kutoka kwa Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- Amesema: "Hakika atakuja mtu mnene tena mkubwa siku ya kiyama akiwa halingani mbele ya Mwenyezi Mungu hata na uzito wa bawa la mbu".
Wamekubaliana Bukhaariy na MuslimDarajaSahihi
Maelezo
Hakika mtu mkubwa ni yule mwenye nia kubwa mwenye kujikweza kwa waja wa Mwenyezi Mungu duniani mwenye kujipa ujabari mwenye kujifaharisha kwa matendo yake na kauli zake, basi huyo siku ya kiyama hatolingana mbele ya Mwenyezi Mungu hata na uzito wa bawa la mbu, na wala hatokuwa na thamani wala nafasi.
Marejeo
كنوز رياض الصالحين، أ. د. حمد بن ناصر بن عبد الرحمن العمار، دار كنوز اشبيليا، الطبعة الأولى : 1430 هـ.
بهجة الناظرين، الشيخ: سليم بن عيد الهلالي، دار ابن الجوزي.
نزهة المتقين، د. مصطفى سعيد الخن، د. مصطفى البغا، محي الدين مستو، علي الشرجبي، محمد أمين لطفي، مؤسسة الرسالة، بيروت، الطبعة الأولى: 1397 هـ 1977 م- الطبعة الرابعة عشر 1407- هـ 1987م.
شرح رياض الصالحين، المؤلف: محمد بن صالح بن محمد العثيمين، الناشر: دار الوطن للنشر، الرياض، الطبعة: 1426هـ.
رياض الصالحين، د. ماهر بن ياسين الفحل، الناشر: دار ابن كثير للطباعة والنشر والتوزيع، دمشق - بيروت
الطبعة: الأولى، 1428 هـ - 2007 م .
صحيح البخاري، لمحمد بن إسماعيل البخاري، دار طوق النجاة، الطبعة : الأولى، 1422هـ.
صحيح مسلم، لمسلم بن الحجاج أبو الحسن القشيري النيسابوري، المحقق: محمد فؤاد عبد الباقي، الناشر: دار إحياء التراث العربي - بيروت.
تطريز رياض الصالحين، المؤلف: فيصل المبارك الحريملي النجدي، المحقق: د. عبد العزيزآل حمد، الناشر: دار العاصمة للنشر والتوزيع، الرياض، الطبعة: الأولى، 1423 هـ - 2002 م.
عن أبي هريرة رضي الله عنه قال: قال رسول الله صلى الله عليه وسلم: «مَنْ أَنْظَرَ مُعْسِرًا، أَوْ وَضَعَ لَهُ، أَظَلَّهُ اللهُ يَوْمَ الْقِيَامَةِ تَحْتَ ظِلِّ عَرْشِهِ يَوْمَ لَا ظِلَّ إِلَّا ظِلُّهُ».
Imepokewa Kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: "Atakayempa muda mwenye hali ngumu, au akamfutia deni, Allah atampa kivuli siku ya kiyama chini ya kivuli cha Arshi yake siku ambayo hapatokuwa na kivuli isipokuwa kivuli chake."
Imepokelewa na Tirmidhiy na AhmadDarajaSahihi
Maelezo
Ametueleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa atakayempa muda mdaiwa wake au akampunguzia katika deni lake, basi malipo yake: Nikuwa Allah atampa kivuli siku ya Kiyama ambayo jua litasogea karibu na vichwa vya waja na joto lake litakuwa kali mno, Hatopata yeyote kivuli isipokuwa atakayetiwa kivuli na Mwenyezi Mungu.
Mafunzo
Fadhila za kuwafanyia wepesi waja wa Mwenyezi Mungu Mtukufu, nakuwa hilo ni katika sababu za kuokoka na misukosuko ya siku ya Kiyama.
Malipo huenda sawa na matendo.
Marejeo
سنن الترمذي (2/ 575) (1306).
مسند أحمد (14/ 329) (8711).
كنوز رياض الصالحين، لمجموعة من الباحثين (16/ 412).
بهجة الناظرين شرح رياض الصالحين، لسليم الهلالي (2/ 459).
فيض القدير شرح الجامع الصغير، للمناوي (6/ 89).
نزهة المتقين شرح رياض الصالحين، لمجموعة من الباحثين (2/ 947).
Imepokelewa kutoka kwa Mikidadi bin Aswadi -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake amesema: Nilimsikia Mtume wa Mwenyezi Mungu -rehema na amani ziwe juu yake- akisema: "Jua litasogezwa karibu na viumbe Siku ya Kiyama mpaka liwe karibu nao umbali wa maili moja.", Sulaim bin 'Amir akasema: "Ninaapa kwa Mwenyezi Mungu, sijui (kiwango) alimaanisha nini kwa "maili"? Je, ni umbali katika ardhi au ni kile kijiti kinachotumiwa kupaka wanja wa manga kwenye jicho." (Mtume) Akasema: "Kisha, watu watakuwa ndani ya jasho yao kulingana na matendo yao. Miongoni mwao, kuna ambaye litakuwa hadi kwenye vifundo viwili vya miguu yake. Na miongoni mwao, kuna ambaye litakuwa hadi kwenye magoti yake mawili. Na miongoni mwao, kuna ambaye litakuwa hadi kwenye nyonga zake mbili. Na miongoni mwao, kuna ambaye jasho (lake) litammeza kabisa."
Imepokelewa Imamu MuslimDarajaSahihi
Maelezo
Ameeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake ya kwamba Jua litasogezwa siku ya Kiyama karibu na viumbe, mpaka liwe vichwani mwao kwa kiasi cha maili moja. Amesema taabii (Mwanafunzi wa swahaba) Saidi bin Aamiri: Wallahi sijui ni maili mbili zipi alikusudia, je ni masafa ya ardhi, ama ni maili (wanja) ambao hutumika kupaka macho? Akasema: Watakuwa katika jasho kulingana na amali zao; yuko miongoni mwao ambaye jasho lake litatiririka mpaka chini ya kongo mbili zake za miguu, na yuko ambaye jasho lake litatiririka mpaka magotini, na yuko ambaye jasho litakuwa katika kitovu chake na kiunoni kwake, na yuko ambaye jasho litafika katika mdomo wake na litamzuia kuzungumza. Amesema: Na akaashiria rehema na amani ziwe juu yake kwa mkono wake katika kinywa chake.
Mafunzo
Kumebainishwa misukosuko ya siku ya Kiyama na kuogopeshwa nayo.
Watu watakuwa katika shida siku ya Kiyama katika kisimamo kulingana na hesabu ya matendo yao.
Himizo la kufanya matendo ya kheri, kemeo la kutofanya matendo ya shari.
Marejeo
صحيح مسلم (4/ 2196) (2864)، (4/ 2196) (2863).
نزهة المتقين شرح رياض الصالحين، لمجموعة من الباحثين (1/ 368).
بهجة الناظرين شرح رياض الصالحين، لسليم الهلالي (1/ 475).
المعجم الوسيط (2/ 816).
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Barza Al Aslamia -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: "Hautonyanyuka unyayo wa mja siku ya Kiyama mpaka aulizwe kuhusu umri wake aliumaliza katika mambo yapi? Na kuhusu elimu yake aliifanyia kazi katika nini? Na kuhusu mali yake ni wapi aliichuma? Na aliitoa katika mambo gani? Na kuhusu mwili wake aliumaliza katika mambo yapi?"
Imepokelewa Imamu TirmidhiyDarajaSahihi
Maelezo
Ameeleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- yakuwa hatovuka mtu yeyote kisimamo cha hesabu siku ya Kiyama kwenda peponi au motoni mpaka aulizwe kuhusu mambo kadhaa:
La kwanza: Maisha yake aliyatumia na kuyamaliza katika nini?
La pili: Elimu yake, je aliitafuta kwa lengo la kupata radhi za Allah? na je aliifanyia kazi? na je aliifikisha kwa wenye kustahiki?
La tatu: Mali yake ni wapi aliichuma, je ni katika halali au haramu? Na aliitoa katika mambo gani, ni katika yale yenye kumridhisha Allah au yenye kumchukiza?.
La nne: Mwili wake na nguvu zake na afya yake na ujana wake, aliutumia na kuumaliza katika mambo gani?
Mafunzo
Himizo la kutumia fursa ya uhai katika yale yenye kumridhisha Allah Mtukufu.
Neema za Allah kwa waja ni nyingi, na atamuuliza kila mmoja kuhusu neema aliyoishi nayo, hivyo anatakiwa aiweke kila neema ya Allah katika yale yenye kumridhisha.
Marejeo
سنن الترمذي (4/ 217) (2417).
نزهة المتقين شرح رياض الصالحين، لمجموعة من الباحثين (1/ 371).
بهجة الناظرين شرح رياض الصالحين، لسليم الهلالي (1/ 478).
المعجم الوسيط (2/ 704).
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira radhi za Allah ziwe juu yake amesema: Amesema Mtume -rehema na amani ziwe juu yake: "Atakayekuwa na dhuluma yoyote ya ndugu yake kama heshima au chochote, basi na wamalizane leo hii, kabla ya wakati ambao hapatakuwa na Dinar wala Dirham, ikiwa atakuwa na amali njema basi zitachukuliwa kwake kwa kiasi cha dhuluma yake, na akiwa hana mema basi yatachukuliwa maovu ya mwenye haki na atabebeshwa yeye".
Imepokelewa na Al-BukhaariyDarajaSahihi
Maelezo
Amemuamrisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake mwenye kutumbukia katika dhuluma ya ndugu yake Muislamu katika heshima, au mali, au damu, basi amuombe aliyemdhulumu amsamehe madamu bado yuko Duniani, kabla haijafika siku ya Kiyama, kiasi ambacho Dinar ya dhahabu wala Dirham ya fedha haitofaa kitu kwa kumlipa aliyemdhulumu ili aikomboe nafsi yake; kwani kisasi siku hiyo kitakuwa kwa matendo mema na mabaya; kiasi kwamba aliyedhulumiwa atachukua kutoka katika mema ya aliyemdhulumu kwa kiwango cha dhuluma yake alichodhulumiwa, ikiwa dhalimu hatokuwa na mema basi yatapunguzwa maovu ya aliyedhulumiwa na kubebeshwa dhalimu kwa kiwango cha dhuluma yake.
Mafunzo
Kupupia kujiweka mbali na dhuluma na uadui.
Himizo la kufanya haraka kujiondoa katika dhima (haki za watu) katika zile alizonazo miongoni mwa haki.
Matendo mema huharibiwa na kutoweka tija yake kwa kuwadhulumu watu na kuwaudhi.
Haki za watu hazisamehi Mwenyezi Mungu isipokuwa kwa kuzirejesha kwa wenye nazo.
Dinar na Dirham ni njia za kuleta manufaa katika Dunia, ama siku ya Kiyama ni matendo mema na maovu pekee.
Wamesema baadhi ya wanachuoni katika maswala ya heshima: Ikiwa aliyedhulumiwa hakujua kama alivunjiwa heshima yake, hakuna haja ya kumjulisha, mfano kama alimtukana katika kikao miongoni mwa vikao na akatubia, basi haina haja ya kumwambia, lakini anatakiwa amuombee msamaha na amuombee mazuri pia, na amtaje kwa mazuri katika kikao hicho hicho alichokuwa akimtukana ndani yake, na kwa kufanya hivyo atakuwa kajivua na hilo.
Marejeo
صحيح البخاري (3/ 129) (2449).
نزهة المتقين شرح رياض الصالحين، لمجموعة من الباحثين (1/ 235).
شرح رياض الصالحين، لابن عثيمين (2/ 508).
بهجة الناظرين شرح رياض الصالحين، لسليم الهلالي (1/ 306).
مرقاة المفاتيح شرح مشكاة المصابيح، لعلي لقاري (8/ 3201).
Kila hadithi, daraja, maelezo na funzo hapa vinaonyeshwa kama HadeethEnc.com inavyovichapisha, kwa masharti yake ya kuchapisha upya. Daraja halimtaji aliyelitoa. Tafsiri na maelezo ni ya waandishi wake wenyewe, na baadhi hutaja hukumu; wahakiki wa Sabīl hawajavichunguza. Hadithi ya Kiarabu ndiyo matini. Chanzo: HadeethEnc.com