Alieleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake baadhi ya sifa za watu wa peponi na za watu wa motoni. Asilimia kubwa ya watu wa peponi ni: "Kila mnyonge mwenye kujishusha", yaani: Mnyenyekevu mwenye kujishusha kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu, mwenye kuidhalilisha nafsi yake kwake, mpaka baadhi ya watu wakamdhoofisha na kumdharau, na huyu mwenye kujidhalilisha kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu lau kama ataapa kwa Mwenyezi Mungu kiapo cha kutamani jambo katika karama za Mwenyezi Mungu Mtukufu, basi Mwenyezi Mungu angemuepusha na kutopokea kiapo chake, na angelimtimizia alichokiapia na angelijibu ombi lake na dua yake. Na asilimia kubwa ya watu wa motoni ni: Kila "Mkaidi" Naye ni fidhuli mkorofi mwingi wa ugomvi, au muovu asiyetii kwa kufata jambo la kheri, "Jeuri" Naye ni mwenye kiburi, mlafi, mwenye mwili mkubwa, mwenye kutembea kwa maringo, mwenye tabia mbaya, "Mwenye kufanya kiburi" kwa kuikataa kwake haki, na kwa kumdharau mtu mwingine.
- Himizo la kujipamba na sifa za watu wa peponi, na tahadhari ya kusifika kwa sifa za watu wa motoni.
- Unyenyekevu unakuwa kwa Mwenyezi Mungu Aliyetakasika na kutukuka, na kwa amri zake na makatazo yake na kutii, na unakuwa kwa viumbe kwa kutojikweza juu yao.
- Amesema bin Hajari: Makusudio yake nikuwa asilimia kubwa ya watu wa peponi ni hawa, kama ambavyo watu wengi wa motoni ni sehemu hii nyingine, na wala makusudio yake si kueleza watu wote wa motoni watakuwa na sifa hizi.
صحيح البخاري (6/ 159) (4918). صحيح مسلم (4/ 2190) (2853). كنوز رياض الصالحين، لمجموعة من الباحثين (5/ 5). شرح رياض الصالحين، لابن عثيمين (3/ 47). بهجة الناظرين شرح رياض الصالحين، لسليم الهلالي (1/ 340). نزهة المتقين شرح رياض الصالحين، لمجموعة من الباحثين (1/ 264).