Walikuwa Masahaba pamoja na Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- katika usiku mmoja akatazama katika mwezi (Usiku wa terehe kumi na nne (14), akasema: Hakika waumini wote watamuona Mola wao Mlezi kwa hakika kabisa kwa macho bila kutatizika, nakuwa hawatosukumana na wala hawatopata tabu wala uzito wakati wa kumuona Mwenyezi Mungu Mtukufu. Kisha akasema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: Ikiwa mtaweza kuzizuia sababu ambazo zinakuzuieni kuto swali swala ya Alfajiri na swala ya Alasiri basi fanyeni hivyo, na zitekelezini kikamilifu ndani ya wakati wake na katika jamaa, kwani hilo ni miongoni mwa sababu za kuuona uso wa Mwenyezi Mungu Mtukufu, kisha akasoma -Rehema na amani ziwe juu yake- Aya "Na utakase sifa za Mola wako kabla ya kuchomoza jua na kabla ya kuzama kwake"
- Habari njema kwa watu wa imani ya kumuona Mwenyezi Mungu Mtukufu peponi.
- Katika njia za kufikisha ujumbe ni: Kusisitiza na kuhamasisha na kupiga mifano.
صحيح البخاري (1/ 115) (554)، (6/ 139) (4851). صحيح مسلم (1/ 439) (633). بهجة الناظرين شرح رياض الصالحين، لسليم الهلالي (2/ 259). تذكرة المؤتسي شرح عقيدة الحافظ عبد الغني المقدسي، لعبدالرزاق البدر (ص177). شرح رياض الصالحين، لابن عثيمين (6/ 734). نزهة المتقين شرح رياض الصالحين، لمصطفى الخِن وغيره (2/ 776). كنوز رياض الصالحين، لمجموعة من الباحثين (13/ 271). تطريز رياض الصالحين، لفيصل آل مبارك (ص1091).