Mtume rehema na amani ziwe juu yake aliwauliza Maswahaba zake: Je, mnamjua aliyefilisika? Wakasema: Aliyefilisika miongoni mwetu ni yule asiye na fedha wala mali. Akasema: Aliyefilisika katika umma wangu Siku ya Kiyama ni yule anayefanya mambo mema kama Swala, Saumu na Zaka, na akaja akiwa kamshutumu huyu na kamtukana huyu, na kamsingizia mabaya mtu huyu katika heshima yake, na kala mali ya huyu na akakana, na akamwaga damu ya huyu na kumdhulumu, na kampiga huyu na akamdhalilisha, hivyo mtu aliyedhulumiwa atapewa kutoka katika matendo yake mema, mema yake yakimalizika kabla ya haki za watu na dhulma hazijamalizika, yatachukuliwa madhambi ya wale aliowadhulumu na kuwekwa katika vitabu vya dhalimu, kisha atatupwa na kurushwa motoni kwani hajabaki na jema.
- Tahadhari dhidi ya kutumbukia katika makatazo, hasa kuhusu haki za watu zenye kuonekana na zisizoonekana.
- Haki za viumbe wao kwa wao mfumo wake ni kutosameheana, na haki za Muumba isipokuwa ushirikina, zimejengeka katika msamaha.
- Kutumia njia ya mazungumzo ambayo humtia shauku msikilizaji, huvuta fikira zake, na huamsha hamasa yake, hasa katika elimu malezi na muongozo.
- Kumeelezwa maana halisi ya mtu aliyefilisika, naye ni yule waliyechukua wadai wake amali zake njema Siku ya Kiyama.
- Kisasi Akhera kinaweza kuja katika mema yote, kiasi kwamba kusibakie jema lolote.
- Muamala wa Mwenyezi Mungu kwa viumbe wake umesimama katika msingi wa uadilifu na haki.
صحيح مسلم (4/ 1997) (2581). بهجة الناظرين شرح رياض الصالحين، لسليم الهلالي (1/ 312). نزهة المتقين شرح رياض الصالحين، مجموعة من الباحثين (1/ 241). شرح رياض الصالحين، لابن عثيمين (2/ 527).