Ruka hadi kwenye maudhui
Hadithi zenye maelezo

Hakika Peponi kuna Soko, watakuwa wakienda hapo kila siku ya Ijumaa

عَنْ أَنَسِ بْنِ مَالِكٍ رَضيَ اللهُ عنهُ أَنَّ رَسُولَ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: «إِنَّ فِي الْجَنَّةِ لَسُوقًا، يَأْتُونَهَا كُلَّ جُمُعَةٍ، فَتَهُبُّ رِيحُ الشَّمَالِ فَتَحْثُو فِي وُجُوهِهِمْ وَثِيَابِهِمْ، فَيَزْدَادُونَ حُسْنًا وَجَمَالًا، فَيَرْجِعُونَ إِلَى أَهْلِيهِمْ وَقَدِ ازْدَادُوا حُسْنًا وَجَمَالًا، فَيَقُولُ لَهُمْ أَهْلُوهُمْ: وَاللهِ لَقَدِ ازْدَدْتُمْ بَعْدَنَا حُسْنًا وَجَمَالًا، فَيَقُولُونَ: وَأَنْتُمْ وَاللهِ لَقَدِ ازْدَدْتُمْ بَعْدَنَا حُسْنًا وَجَمَالًا».
Imepokelewa kutoka kwa Anas bin Maliki radhi za Allah ziwe juu yake: Ya kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu rehema na amani ziwe juu yake amesema: "Hakika Peponi kuna Soko, watakuwa wakienda hapo kila siku ya Ijumaa, basi utavuma upepo wa kaskazi utawamwagikia katika nyuso zao na nguo zao, na hapo wataongezeka uzuri na urembo, watarudi kwa familia zao wakiwa wameongezeka uzuri na urembo, watasema kuwaambia: Wallahi mmezidi uzuri na urembo baada yetu, watasema: Na nyinyi Wallahi hakika mmezidi uzuri na urembo baada yetu".
Imepokelewa Imamu MuslimDarajaSahihi
Maelezo

Ameeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake ya kwamba Peponi kuna sehemu watu watakuwa wakikusanyika hapo, hapatokuwa na kuuza wala kununua, bali watakuwa wakichukua kutoka hapo wanachokitaka, watakuwa wakienda hapo kwa kiasi cha siku saba, utavuma upepo wa kaskazi, utatikisa katika nyuso zao na nguo zao, wataongezeka uzuri na urembo, watarudi kwa familia zao wakiwa wameongezeka uzuri na urembo, watasema kuwambia: Wallahi hakika mmezidi uzuri na urembo baada yetu, na wao watasema: Na nyinyi Wallah hakika mmezidi uzuri na urembo baada yetu.

Mafunzo
  1. Kumebainishwa ya kwamba watu wa Peponi watakuwa wakiongezeka uzuri na urembo.
  2. Hadithi hizi zinampelekea mtu kuwa na hamu ya kutenda mema ambayo hutumika kumfikisha mtu katika nyumba hii.
  3. Ameutaja upepo wa kaskazi pekee; kwa sababu ndio uliokuwa upepo mzuri zaidi kwa waarabu kwani ndio ulikuwa ukija na kheri na mvua.
  4. Himizo la kuwaita watu kwa Mwenyezi Mungu kwa kuwahamasisha kuhusu pepo na neema zake.
Marejeo

صحيح مسلم (4/ 2178) (2833). نزهة المتقين شرح رياض الصالحين، لمجموعة من الباحثين (2/ 1290). بهجة الناظرين شرح رياض الصالحين، لسليم الهلالي (3/ 347). تطريز رياض الصالحين، لفيصل آل مُبَارَك (ص1088). شرح رياض الصالحين، لابن عثيمين (6/ 731).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com
Sifa za pepo na moto.

Kila hadithi, daraja, maelezo na funzo hapa vinaonyeshwa kama HadeethEnc.com inavyovichapisha, kwa masharti yake ya kuchapisha upya. Daraja halimtaji aliyelitoa. Tafsiri na maelezo ni ya waandishi wake wenyewe, na baadhi hutaja hukumu; wahakiki wa Sabīl hawajavichunguza. Hadithi ya Kiarabu ndiyo matini. Chanzo: HadeethEnc.com