Ruka hadi kwenye maudhui
Hadithi zenye maelezo

Ewe baba Saidi, yeyote atakayeridhia kuwa Mwenyezi Mungu ndiye Mola, na Uislamu kuwa ndiyo dini, na Muhammadi kuwa ni Nabii, basi atakuwa kastahiki Pepo

عَنْ أَبِي سَعِيدٍ الْخُدْرِيِّ رَضيَ اللهُ عنهُ أَنَّ رَسُولَ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: «يَا أَبَا سَعِيدٍ، مَنْ رَضِيَ بِاللهِ رَبًّا، وَبِالْإِسْلَامِ دِينًا، وَبِمُحَمَّدٍ نَبِيًّا، وَجَبَتْ لَهُ الْجَنَّةُ»، فَعَجِبَ لَهَا أَبُو سَعِيدٍ، فَقَالَ: أَعِدْهَا عَلَيَّ يَا رَسُولَ اللهِ، فَفَعَلَ، ثُمَّ قَالَ: «وَأُخْرَى يُرْفَعُ بِهَا الْعَبْدُ مِائَةَ دَرَجَةٍ فِي الْجَنَّةِ، مَا بَيْنَ كُلِّ دَرَجَتَيْنِ كَمَا بَيْنَ السَّمَاءِ وَالْأَرْضِ»، قَالَ: وَمَا هِيَ يَا رَسُولَ اللهِ؟ قَالَ: «الْجِهَادُ فِي سَبِيلِ اللهِ، الْجِهَادُ فِي سَبِيلِ اللهِ».
Kutoka kwa Abuu Saidi Al-Khudry -radhi za Allah ziwe juu yake- yakwamba Mtume -rehema na amani ziwe juu yake amesema-: "Ewe baba Saidi, yeyote atakayeridhia kuwa Mwenyezi Mungu ndiye Mola, na Uislamu kuwa ndiyo dini, na Muhammadi kuwa ni Nabii, basi atakuwa kastahiki Pepo", Abuu Saidi likamshangaza sana hilo, akasema: Naomba uyarudie tena maneno hayo ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, akarudia, kisha akasema: "Na la mwisho mja ananyanyuliwa kwalo daraja katika Pepo, umbali ulio kati ya daraja mbili hizo ni kama baina ya mbingu na ardhi", Akasema: Ni lipi hilo ewe Mjume wa Mwenyezi Mungu? Akasema: "Ni kupigana Jihadi katika njia ya Mwenyezi Mungu, ni kupigana Jihadi katika njia ya Mwenyezi Mungu".
Imepokelewa Imamu MuslimDarajaSahihi
Maelezo

Alimueleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake Abuu Saidi Al-Khudri radhi za Allah ziwe juu yake kwamba yeyote atakayemuamini Mwenyezi Mungu na akamridhia kuwa Mola na Mungu na mmiliki na mtukufu na muamrishaji, na Uislamu kuwa ni dini, kwa kutii na kujisalimisha katika amri zake zote na makatazo yake yote, na Muhammadi rehema na amani ziwe juu yake kuwa ni Nabii, kwa yote aliyotumwa kwayo na akayafikisha; itamthibitikia kwake Pepo, Abuu Saidi akastaajabu radhi za Allah ziwe juu yake, akasema: Yarudie tena ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, akafanya hivyo, kisha akasema rehema na amani ziwe juu yake: Na nina jambo jingine ambalo Mwenyezi Mungu Mtukufu humnyanyua mja daraja mia moja Peponi kwalo, masafa yaliyoko kati ya daraja mbili hizo ni kama umbali ulioko baina ya mbingu na ardhi, akasema Abuu Saidi: Na nilipi hilo ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu? Akasema: Ni kupigana Jihadi katika njia ya Mwenyezi Mungu, ni kupigana Jihadi katika njia ya Mwenyezi Mungu.

Mafunzo
  1. Miongoni mwa mambo yanayopelekea kuingia peponi ni kuridhia kuwa Allah ndiye mola na Uislamu kuwa ni dini na Muhammadi rehema na amani ziwe juu yake kuwa ni Nabii.
  2. Kutukuzwa swala la Jihadi katika njia ya Mwenyezi Mungu Mtukufu.
  3. Kunyanyuliwa kwa daraja ya Jihadi Peponi.
  4. Peponi kuna daraja nyingi zisizohesabika, na nyumba zisizohesabika, na wapiganaji watakuwa na daraja mia moja ndani yake.
  5. Mapenzi ya Maswahaba wa Mtume rehema na amani ziwe juu yake ya kutaka kujua kheri, na milango yake na sababu zake.
Marejeo

صحيح مسلم (3/ 1501) (1884). نزهة المتقين، لمجموعة من الباحثين (2/ 910). بهجة الناظرين، لسليم الهلالي (3/ 423). النهاية في غريب الحديث والأثر، لابن الأثير (5/ 153).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com
Sifa za pepo na moto.

Kila hadithi, daraja, maelezo na funzo hapa vinaonyeshwa kama HadeethEnc.com inavyovichapisha, kwa masharti yake ya kuchapisha upya. Daraja halimtaji aliyelitoa. Tafsiri na maelezo ni ya waandishi wake wenyewe, na baadhi hutaja hukumu; wahakiki wa Sabīl hawajavichunguza. Hadithi ya Kiarabu ndiyo matini. Chanzo: HadeethEnc.com