Ameeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa mtu mwenye adhabu nafuu katika watu wa motoni siku ya Kiyama ni yule atayekuwa na viatu viwili na soli mbili, utakuwa ukichemka ubongo wake kutokana na kuchemka kwake, kama linavyochemka sufuria la shaba, na wala hatoona kuwa kuna yeyote mwenye adhabu kali zaidi yake, kumbe yeye ndiye mwenye adhabu nafuu zaidi kuliko wote, na hii ni kwa sababu zitakusanyika kwake adhabu zote mbili, adhabu ya mwili na adhabu ya nafsi.
- Tahadhari hii ni kwa wanaoasi na makafiri kutokana na vitisho vya adhabu hii motoni; ili wajitenge mbali na yale yanayopelekea huko.
- Kutofautiana kwa vina vya waoingia motoni kulingana na ubaya wa matendp yao.
- Ukali wa adhabu ya moto, tunamuomba Allah atusalimishenayo.
صحيح البخاري (8/ 115) (6561). صحيح مسلم (1/ 196) (213). نزهة المتقين شرح رياض الصالحين، لمجموعة من الباحثين (1/ 366). كنوز رياض الصالحين، لمجموعة من الباحثين (6/ 394). بهجة الناظرين شرح رياض الصالحين، لسليم الهلالي (1/ 472). شرح رياض الصالحين، لابن عثيمين (3/ 295). المعجم الوسيط (1/ 256).