Lilimfikia jambo Mtume rehema na amani ziwe juu yake kutoka kwa Maswahaba zake, nalo ni kwamba wao walimzidishia maswali, akakasirika, na akawahutubia, akasema: Nimeonyeshwa Pepo na Moto; sikuwahi kuona kheri nyingi kuliko nilizoziona siku ya leo Peponi, wala shari kubwa kuliko nilizoziona siku hiyo Motoni, na lau kama mngeliona nilichokiona, na mkajua ninachokijua katika yale niliyoyaona siku ya leo na kabla ya leo, basi mngelihuzunika huzuni kubwa, na kungepungua kucheka kwenu, na kungezidi kulia kwenu. Anasema Anasi radhi za Allah ziwe juu yake: Haikuwahi kutoka kwa Maswahaba wake rehema na amani ziwe juu yake siku ngumu kama hiyo, na wakafunika vichwa vyao huku wakitoa sauti ya kunung'unika inayotoka puani kwa sababu ya kulia sana. Akasimama Omari radhi za Allah ziwe juu yake akasema: Tumemridhia Mwenyezi Mungu kuwa Mola, na Uislamu kuwa dini, na Muhammadi kuwa Nabii. Akasema: Akasimama yule bwana, akasema: Nani baba yangu? Akasema: "Baba yako ni fulani", ikateremka: "Enyi mlioamini! Msiulize kuhusu mambo ambayo yakikudhihirikieni yatakuchukizeni" [Al-Ma’idah: 101].
- Ni Sunna kulia kwa kuhofia adhabu ya Mwenyezi Mungu, na kutokithirisha kucheka; kwa sababu hilo linaonyesha kughafilika na ugumu wa moyo.
- Waliathirika na mawaidha Maswahaba radhi za Allah ziwe juu yao, na hofu yao kubwa dhidi ya adhabu za Mwenyezi Mungu Aliyetakasika na kutukuka.
- Sunna ya kufunika uso wakati wa kulia.
- Amesema Al-Khattwabi: Hadithi hii ni kwa mtu aliyeuliza kwa kuchokonoa mambo au kwa ukaidi katika mambo ambayo hana haja nayo, ama atakayeuliza kwa dharura, kwa kutokewa na jambo akaliulizia, huyu hana dhambi juu yake wala lawama.
- Himizo la kuwa na msimamo katika kumtii Allah, na kujitenga mbali na kumuasi Allah, na kusimama katika mipaka ya Mwenyezi Mungu.
- Hapa inaonyesha kufaa kukasirika wakati wa mawaidha na wakati wa kufundisha.
صحيح البخاري (6/ 54) (4621). صحيح مسلم (4/ 1832) (2359). نزهة المتقين شرح رياض الصالحين، لمجموعة من الباحثين (1/ 367). بهجة الناظرين شرح رياض الصالحين، لسليم الهلالي (1/ 474). النهاية في غريب الحديث والأثر، لابن الأثير(1/ 45).