Alieleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa Pepo na Moto viko karibu mno na mwanadamu kama ukaribu wa mwendo wa kiatu unaokuwa juu ya kisigino, kwa sababu anaweza kufanya twa'a (ibada) katika yale yanayomridhisha Allah Mtukufu akaingia Peponi kwa ibada hiyo, au dhambi moja likawa sababu ya kuingia motoni.
- Himizo la kufanya heri hata kama ni ndogo, na tishio la kufanya shari hata kama ni ndogo.
- Ni lazima muislamu katika maisha yake kukusanya kati ya kutaraji mazuri na kuogopa adhabu, na kumuomba Allah Mtukufu muda wote kuthubutu (Kudumu) katika haki mpaka asalimike na wala asihadaike na hali aliyonayo.
صحيح البخاري (8/ 102) (6488). شرح رياض الصالحين، لابن عثيمين (2/ 99). فتح الباري، لابن حجر(11/ 321). بهجة الناظرين شرح رياض الصالحين، لسليم الهلالي (1/ 186). نزهة المتقين شرح رياض الصالحين، لمصطفى الخِن وغيره (1/ 136).