Ruka hadi kwenye maudhui
Hadithi zenye maelezo

Moto umezingirwa na yenyekutamanisha, na Pepo imezingirwa na yenyekuchukiza

عن أبي هريرة رضي الله عنه أن رسول الله صلى الله عليه وسلم قال: «حُجِبَتِ النَّارُ بِالشَّهَوَاتِ، وَحُجِبَتِ الْجَنَّةُ بِالْمَكَارِهِ».
Imepokelewa Kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake- Yakwamba Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Moto umezingirwa na yenyekutamanisha, na Pepo imezingirwa na yenyekuchukiza".
Imepokelewa na Al-BukhaariyDarajaSahihi
Maelezo

Amebainisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa Moto umezungukwa na kuzingirwa na mambo ambayo nafsi inayatamani, kama kufanya maharamisho au uzembe katika mambo ya wajibu; Atakayeendekeza matamanio ya nafsi yake katika hilo atastahiki moto, nakuwa Pepo imezungukwa na kuzingirwa na mambo ambayo yanachukiwa na nafsi; kama kudumu katika maamrisho na kuacha maharamisho na kuvumilia juu ya hilo, atakapovumilia na akapigana vita na nafsi yake juu ya hilo atastahiki kuingia Peponi.

Mafunzo
  1. Miongoni mwa sababu za kuingia katika matamanio ni shetani kuyapamba maovu na machafu, mpaka nafsi inayaona kuwa ni mazuri na kisha kuyaelekea.
  2. Amri ya kujitenga mbali na matamanio yaliyoharamishwa; kwa sababu hayo ni njia ya kuelekea motoni, na kuvumilia juu ya kero; kwani ni njia ya kuelekea Peponi.
  3. Ubora na fadhila za kupigana na nafsi na kuwa na bidii katika ibada na kuvumilia kero na tabu zinazo zizunguka ibada.
Marejeo

صحيح البخاري (8/ 102) (6487). صحيح مسلم (4/ 2174) (2822). سنن أبي داود (7/ 122) (4744). سنن الترمذي (4/ 274) (2560). سنن النسائي (7/ 3) (3763). كنوز رياض الصالحين، لمجموعة من الباحثين (2/ 449). شرح رياض الصالحين، لابن عثيمين (2/ 87). المنهاج شرح صحيح مسلم بن الحجاج، للنووي (17/ 165). بهجة الناظرين شرح رياض الصالحين، لسليم الهلالي (1/ 183). نزهة المتقين شرح رياض الصالحين، لمصطفى الخِن وغيره (1/ 134).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com
Sifa za pepo na moto.

Kila hadithi, daraja, maelezo na funzo hapa vinaonyeshwa kama HadeethEnc.com inavyovichapisha, kwa masharti yake ya kuchapisha upya. Daraja halimtaji aliyelitoa. Tafsiri na maelezo ni ya waandishi wake wenyewe, na baadhi hutaja hukumu; wahakiki wa Sabīl hawajavichunguza. Hadithi ya Kiarabu ndiyo matini. Chanzo: HadeethEnc.com