Ruka hadi kwenye maudhui
Hadithi zenye maelezo

Hili ni jiwe lililotupwa Motoni muda wa (miaka) sabini iliyopita, na sasa linaanguka Motoni mpaka litafika katika kina chake

عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رضي الله عنه قَالَ: كُنَّا مَعَ رَسُولِ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، إِذْ سَمِعَ وَجْبَةً، فَقَالَ النَّبِيُّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: «تَدْرُونَ مَا هَذَا؟» قَالَ: قُلْنَا: اللهُ وَرَسُولُهُ أَعْلَمُ، قَالَ: «هَذَا حَجَرٌ رُمِيَ بِهِ فِي النَّارِ مُنْذُ سَبْعِينَ خَرِيفًا، فَهُوَ يَهْوِي فِي النَّارِ الْآنَ حَتَّى انْتَهَى إِلَى قَعْرِهَا».
Kutoka kwa Abuu Huraira -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- amesema: Tulikuwa pamoja na Mtume rehema na amani ziwe juu yake ghafla akasikia kishindo, akasema Mtume rehema na amani ziwe juu yake: “Je, mnajua ni nini hiki?” Akasema: Tukasema: Mwenyezi Mungu na Mtume wake wanajua zaidi, akasema: «Hili ni jiwe lililotupwa Motoni muda wa (miaka) sabini iliyopita, na sasa linaanguka Motoni mpaka litafika katika kina chake.
Imepokelewa Imamu MuslimDarajaSahihi
Maelezo

Mtume rehema na amani ziwe juu yake alisikia sauti ya kushtua kama kuanguka kwa mwili, akawauliza Masahaba aliokuwa nao Mwenyezi Mungu awawie radhi kuhusu sauti hiyo, wakasema: Mwenyezi Mungu na Mtume wake ndio wajuzi zaidi. Akawaambia rehema na amani ziwe juu yake: Sauti hii mliyoisikia ni ya jiwe lililorushwa kutoka ukingo wa Jahannam miaka sabini iliyopita lilikuwa likiporomoka na kuanguka humo, hivi sasa mliposikia kishindo ndio limefika katika kina chake.

Mafunzo
  1. Himizo la kujiandaa na siku ya mwisho kwa amali njema, na kutahadhari na Jahannam.
  2. Ni sunna kuiegemeza elimu kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu katika yale ambayo mtu hana elimu nayo.
  3. Mwalimu anatakiwa kuamsha hisia na umakini kwa wanafunzi kabla ya kuwaeleza; ili uwe ni msukumo wa wao kuelewa.
Marejeo

صحيح مسلم (4/ 2184) (2844). بهجة الناظرين شرح رياض الصالحين، لسليم الهلالي (1/ 476). نزهة المتقين شرح رياض الصالحين، لمجموعة من الباحثين (1/ 369). كنوز رياض الصالحين، لمجموعة من الباحثين (6/ 414).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com
Sifa za pepo na moto.

Kila hadithi, daraja, maelezo na funzo hapa vinaonyeshwa kama HadeethEnc.com inavyovichapisha, kwa masharti yake ya kuchapisha upya. Daraja halimtaji aliyelitoa. Tafsiri na maelezo ni ya waandishi wake wenyewe, na baadhi hutaja hukumu; wahakiki wa Sabīl hawajavichunguza. Hadithi ya Kiarabu ndiyo matini. Chanzo: HadeethEnc.com