عن أنس بن مالك رضي الله عنه قال: كَانَ رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ أَحْسَنَ النَّاسِ خُلُقًا.
Imepokelewa kutoka kwa Anas bin Maalik -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- amesema: Alikuwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- ni mtu mwenye tabia nzuri mno kuliko watu wote.
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeDarajaSahihi
Maelezo
Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- alikuwa na tabia zilizokamilika kuliko watu wote, na mtu wa mbele katika tabia njema na mambo mazuri, kama maneno mazuri, na kufanya heri, na uso mkunjufu, na kujizuia na maudhi na kuyavumilia kutoka kwa wengine.
Mafunzo
- Ukamilifu wa tabia ya Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-.
- Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- yeye ndiye kiigizo kamili katika tabia nzuri.
- Himizo la kuiga kutoka kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- katika tabia nzuri.
Marejeo
صحيح البخاري (8/ 45) (6203).
صحيح مسلم (4/ 1805) (2310).
بهجة الناظرين شرح رياض الصالحين، لسليم الهلالي (1/ 670).
نزهة المتقين شرح رياض الصالحين، لمصطفى الخِن وغيره (1/ 524).
كنوز رياض الصالحين، لمجموعة من الباحثين (9/ 57).
شرح رياض الصالحين، لابن عثيمين (3/ 556).
Hadithi hii kwenye HadeethEnc.comقال سعد بن هشام بن عامر -عندما دخل على عائشة رضي الله عنها-: يَا أُمَّ الْمُؤْمِنِينَ، أَنْبِئِينِي عَنْ خُلُقِ رَسُولِ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، قَالَتْ: أَلَسْتَ تَقْرَأُ الْقُرْآنَ؟ قُلْتُ: بَلَى، قَالَتْ: فَإِنَّ خُلُقَ نَبِيِّ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ كَانَ الْقُرْآنَ.
Amesema Sa'd bin Hisham bin Aamiri -alipoingia kwa Aisha -Radhi za Allah ziwe juu yake: Ewe mama wa waumini, nieleze kuhusu tabia ya Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-, akasema: Hivi si unasoma Qur'ani? Nikasema: Ndiyo! akasema: Basi tabia ya Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- ilikuwa ni Qur'ani.
Imepokelewa na Muslim katika ujumla wa hadithi iliyokuwa ndefuDarajaSahihi
Maelezo
Aliulizwa mama wa waumini Aisha -Radhi za Allah ziwe juu yake- kuhusu tabia ya Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-, akajibu kwa neno lilokusanya, na akamuhamisha muulizaji upande wa Qura''ani tukufu iliyo kusanya sifa za ukamilifu, kama alivyosema -Rehema na amani ziwe juu yake- akasema alikuwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akiiga tabia za Qur'ani, iliyoyaamrisha Qur'ani anayaamrisha, na yale inayoyakataza Qur'ani anayaepuka, basi ikawa tabia yake ni kuifanyia kazi Qur'ani, na kusimama katika mipaka yake na kua na adabu na adabu zake kuizingatia Qur'ani na matendo kwa ujumla na mfano wake.
Mafunzo
- Himizo la kumuiga Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- katika kujipamba kwake na tabia za Qur'ani.
- Kusifiwa kwa tabia za Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-, nakuwa tabia hizo zilikuwa zikitoka katika taa ya wahyi.
- Qur'ani ndio chimbuko la kila tabia njema.
- Tabia katika Uislamu zinakusanya dini yote, kwa kutekeleza maamrisho na kuacha makatazo.
Marejeo
صحيح مسلم (1/ 512) (746).
بهجة الناظرين شرح رياض الصالحين، لسليم الهلالي (3/ 308).
شرح رياض الصالحين، لابن عثيمين (6/ 660).
نزهة المتقين شرح رياض الصالحين، لمصطفى الخن وغيره (2/ 1253).
كنوز رياض الصالحين، لمجموعة من الباحثين (21/ 556).
Hadithi hii kwenye HadeethEnc.comعَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: «اللهُمَّ إِنَّمَا أَنَا بَشَرٌ، فَأَيُّمَا رَجُلٍ مِنَ المُسْلِمِينَ سَبَبْتُهُ أَوْ لَعَنْتُهُ أَوْ جَلَدْتُهُ فَاجْعَلْهَا لَهُ زَكَاةً وَرَحْمَةً».
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira radhi za Allah ziwe juu yake amesema: Amesema Mtume rehema na amani ziwe juu yake: "Ewe Mola wangu, hakika mimi ni mwanadamu, basi yeyote katika Waislamu niliyemtukana au kumlaani au kumpiga kwa mjeledi, basi hilo lifanye kwake kuwa ni utakaso na huruma".
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeDarajaSahihi
Maelezo
Aliomba Mtume rehema na amani ziwe juu yake akasema: Ewe Mola wangu, hakika mimi ni mwanadamu, hivyo basi, muumini yeyote niliyemuudhi au kumtukana au kumshutumu, au kumlaani, na nikamuombea kufukuzwa katika rehema yako, au nilimpiga mjeledi au kipigo chochote, basi lifanye hilo kwake kuwa ni utakaso na ibada na twahara na kafara na rehema utakayomhurumia kwayo.
Mafunzo
- Utukufu wa tabia ya Mtume rehema na amani ziwe juu yake.
- Amesema bin Hajari: Katika hadithi kuna ukamilifu wa huruma yake rehema na amani ziwe juu yake juu ya Umma wake na uzuri wa tabia yake na ukarimu wake, kiasi kwamba alikusudia kuyakabili yaliyotokea kwake kama ponyo na ukarimu.
- Amesema Nawawi: Pakisemwa: Kwa nini amuombee dua mbaya asiyestahiki, au amtukane au amlaani na mfano wa hayo? Jawabu ni lile walilojibu wanachuoni, na kwa ufupi, liko namna mbili: Ya kwanza: Ni kuwa makusudio yake si wastahiki wa hilo mbele ya Mwenyezi Mungu Mtukufu, na hata undani wa jambo, lakini kwa uwazi wa jambo ni kuwa anastahiki hilo, inamdhihirikia Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa anastahiki hilo kwa alama za kisheria, kumbe uhalisia wake ni kinyume na hivyo, naye Mtume rehema na amani ziwe juu yake ameamrishwa kuhumu kwa kile kinachodhihiri, na Mwenyezi Mungu ndiye anayesimamia siri. Ya pili: Ni kwamba kilichotokea katika kutusi kwake na dua yake mbaya na mfano wake, si makusudi, bali ni katika yale ambayo ndimi za Waarabu zilizoea katika kuunga kwao maneno yao pasina kukusudia, kama mtu kusema: Umepata hasara, au ushindwe kabisa, na katika hadithi hii: "Usiendelee kukua umri wako" na katika hadithi ya Muawia: "Mwenyezi Mungu asilishibishe tumbo lako" na mfano wa hayo hawakusudii chochote katika dua mbaya, akahofia Mtume rehema na amani ziwe juu yake maneno hayo yasijekukutana na muda wa kujibiwa dua yakampata mtu, akamuomba Mwenyezi Mungu Mtukufu, na akajipendekeza kwake ili ayafanye hayo yote kuwa rehema na kafara, na ibada na twahara na malipo, bali yalikuwa yakijitokeza haya kwake kwa nadra sana na nyakati ndogo, na hakuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake mwenye ulimi mchafu wala mtoa laana, wala mwenye kulipiza kisasi kwa masilahi ya nafsi yake.
Marejeo
صحيح البخاري (8/ 77) (6361).
صحيح مسلم (4/ 2007) (2601).
عمدة القاري شرح صحيح البخاري (22/ 310).
إرشاد الساري لشرح صحيح البخاري (9/ 207).
Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com