Alikuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake na haya zaidi kuliko hata bikira ndani ya chumba chake, basi anapoona jambo asilolipenda tunajua kuwa hapendi kwa kupitia usoni kwake
Anasimulia Abuu Said Al-Khudri Mwenyezi Mungu amuwie radhi, kuwa alikuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake na haya zaidi kuliko msichana bikira ambaye hajaolewa na kuishi na wanaume aliyefichwa nyumbani kwake, na kwa sababu ya ukubwa wa aibu yake anapokichukia kitu uso wake unabadilika na wala hazungumzi, bali masahaba wake wanalibaini hilo katika uso wake.
- Kumebainishwa miongoni mwa sifa alizokuwa nazo Mtume rehema na amani zimshukie kama haya, ambayo ni tabia tukufu.
- Haya ya Mtume rehema na amani ziwe juu yake, maadamu hayajatendeka makatazo ya Mwenyezi Mungu, yakitendeka basi rehema na amani ziwe juu yake alikuwa akikasirika na kuwaamrisha maswahaba zake na kuwakataza.
- Himizo la kujipamba na sifa ya haya; kwa sababu huisukuma nafsi kufanya mazuri na kuacha machafu.
صحيح البخاري (8/ 26) (6102). صحيح مسلم (4/ 1809) (2320). بهجة الناظرين شرح رياض الصالحين، لسليم الهلالي (2/ 11). شرح رياض الصالحين، لابن عثيمين (4/ 32). نزهة المتقين شرح رياض الصالحين، لمجموعة من الباحثين (1/ 562).