Alikuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake na haya zaidi kuliko hata bikira ndani ya chumba chake, basi anapoona jambo asilolipenda tunajua kuwa hapendi kwa kupitia usoni kwake
Kutoka kwa Abuu Saidi Al Kudry -radhi za Allah ziwe juu yake- Amesema: Alikuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake na haya zaidi kuliko hata bikira ndani ya chumba chake, basi anapoona jambo asilolipenda tunajua kuwa hapendi kwa kupitia usoni kwake.
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeDarajaSahihi
Maelezo
Anasimulia Abuu Said Al-Khudri Mwenyezi Mungu amuwie radhi, kuwa alikuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake na haya zaidi kuliko msichana bikira ambaye hajaolewa na kuishi na wanaume aliyefichwa nyumbani kwake, na kwa sababu ya ukubwa wa aibu yake anapokichukia kitu uso wake unabadilika na wala hazungumzi, bali masahaba wake wanalibaini hilo katika uso wake.
Mafunzo
Kumebainishwa miongoni mwa sifa alizokuwa nazo Mtume rehema na amani zimshukie kama haya, ambayo ni tabia tukufu.
Haya ya Mtume rehema na amani ziwe juu yake, maadamu hayajatendeka makatazo ya Mwenyezi Mungu, yakitendeka basi rehema na amani ziwe juu yake alikuwa akikasirika na kuwaamrisha maswahaba zake na kuwakataza.
Himizo la kujipamba na sifa ya haya; kwa sababu huisukuma nafsi kufanya mazuri na kuacha machafu.
Marejeo
صحيح البخاري (8/ 26) (6102).
صحيح مسلم (4/ 1809) (2320).
بهجة الناظرين شرح رياض الصالحين، لسليم الهلالي (2/ 11).
شرح رياض الصالحين، لابن عثيمين (4/ 32).
نزهة المتقين شرح رياض الصالحين، لمجموعة من الباحثين (1/ 562).
Kila hadithi, daraja, maelezo na funzo hapa vinaonyeshwa kama HadeethEnc.com inavyovichapisha, kwa masharti yake ya kuchapisha upya. Daraja halimtaji aliyelitoa. Tafsiri na maelezo ni ya waandishi wake wenyewe, na baadhi hutaja hukumu; wahakiki wa Sabīl hawajavichunguza. Hadithi ya Kiarabu ndiyo matini. Chanzo: HadeethEnc.com