Ruka hadi kwenye maudhui
Hadithi zenye maelezo

Historia na Taarekh.

Hadithi 51

Ewe Abubakari, kwani ipi dhana yako kwa wawili ambao Mwenyezi Mungu ndiye wa tatu wao

عَنْ أَبِي بَكْرٍ الصِّدِّيقَ رَضيَ اللهُ عنه قَالَ: نَظَرْتُ إِلَى أَقْدَامِ الْمُشْرِكِينَ عَلَى رُءُوسِنَا وَنَحْنُ فِي الْغَارِ، فَقُلْتُ: يَا رَسُولَ اللهِ لَوْ أَنَّ أَحَدَهُمْ نَظَرَ إِلَى قَدَمَيْهِ أَبْصَرَنَا تَحْتَ قَدَمَيْهِ، فَقَالَ: «يَا أَبَا بَكْرٍ، مَا ظَنُّكَ بِاثْنَيْنِ اللهُ ثَالِثُهُمَا».
Kutoka kwa Abubakari Swiddiq radhi za Allah ziwe juu yake amesema: Niliitazama miguu ya washirikina juu ya vichwa vyetu, na sisi tukiwa pangoni, nikasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, lau kama mmoja wao angelitazama katika nyayo zake angetuona chini ya nyayo zake, akasema: "Ewe Abubakari, kwani ipi dhana yako kwa wawili ambao Mwenyezi Mungu ndiye wa tatu wao".
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeDarajaSahihi
Maelezo

Alisema kiongozi wa waumini Abubakari Swiddiq radhi za Allah ziwe juu yake wakati wa kuhama: Nilitazama katika nyayo za washirikina nao wakiwa wamesimama juu ya vichwa vyetu juu ya pango na sisi tukiwa ndani yake, nikasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, lau kama mmoja wao angelitazama katika nyayo zake angetuona chini ya nyayo zake, akasema: Ewe Abubakari, kwani ni ipi dhana yako kwa wawili ambao Mwenyezi Mungu ndiye wa tatu wao kwa kuwanusuru na kuwasaidia, na kuwahifadhi na kuwapa muongozo?!

Mafunzo
  1. Nafasi ya Abubakari Swiddiq radhi za Allah ziwe juu yake kwa kuambatana kwake na Mtume rehema na amani ziwe juu yake katika kuhama kwake kutoka Makka kwenda Madina, na kutengena kwake na familia yake na mali yake.
  2. Huruma ya Abubakari radhi za Allah ziwe juu yake, na kiwango cha mapenzi yake kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake, na hofu yake kwake dhidi ya maadui.
  3. Uwajibu wa kuwa na imani na Mwenyezi Mungu Mtukufu, na kutulizana katika ulinzi wake na himaya yake, baada ya kutumia juhudi katika kukwepa na kuchukua tahadhari.
  4. Mwenyezi Mungu kuwajali Manabii wake na Mawalii wake, na kuwalinda kwa kuwapa ushindi, amesema Mtukufu: "Hakika sisi tunawanusuru Mitume wetu na wale walioamini katika maisha ya dunia na siku watakaposimama mashahidi".
  5. Angalizo kuwa yeyote atakayemtegemea Mwenyezi Mungu basi atamtosheleza, na atamnusuru, na atamsaidia, na atamlinda na atamuhifadhi.
  6. Ukamilifu wa Mtume rehema na amani ziwe juu yake wa kumtegemea Mola wake Mlezi, na kwamba yeye anategemea kwake, na anakabidhi kwake mambo yake.
  7. Ushujaa wa Mtume rehema na amani ziwe juu yake, na kuzituliza kwake nyoyo na nafsi.
  8. Kukimbia kwa ajili ya dini kwa kumuogopa adui, na kuchukua sababu za kuokoka.
Marejeo

صحيح البخاري (5/ 4) (3653). صحيح مسلم (4/ 1854) (2381). شرح صحيح مسلم (149/15). فتح الباري (11/7). كنوز رياض الصالحين، لمجموعة من الباحثين (276/2) شرح رياض الصالحين لابن عثيمين (563/1).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Kila hadithi, daraja, maelezo na funzo hapa vinaonyeshwa kama HadeethEnc.com inavyovichapisha, kwa masharti yake ya kuchapisha upya. Daraja halimtaji aliyelitoa. Tafsiri na maelezo ni ya waandishi wake wenyewe, na baadhi hutaja hukumu; wahakiki wa Sabīl hawajavichunguza. Hadithi ya Kiarabu ndiyo matini. Chanzo: HadeethEnc.com