Ruka hadi kwenye maudhui
Hadithi zenye maelezo

Mambo ya Mtume.

Hadithi 32

Alikuwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- anapopiga chafya anaweka mkono wake au nguo yake juu ya kinywa chake, na anapunguza sauti yake

عن أبي هريرة رضي الله عنه قال: كان رسولُ الله صلى الله عليه وسلم إذا عَطَس وضَعَ يَدَه -أو ثوبَهُ- على فيهِ، وخَفَضَ -أو غضَّ- بها صوتَهُ.
Kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Alikuwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- anapopiga chafya anaweka mkono wake au nguo yake juu ya kinywa chake, na anapunguza sauti yake.
Imepokelewa na Abu Daud, Tirmidhiy na AhmadDarajaSahihi
Maelezo

Alikuwa rehema na amani ziwe juu yake anapopiga chafya: Jambo la kwanza: Anaweka mkono wake, au nguo yake juu ya kinywa chake; Kisije kutoka kinywani mwake au puani mwake chochote kitakachomuudhi aliyekaa naye. Jambo la pili: Anashusha sauti yake na wala hainyanyui.

Mafunzo
  1. Hapa pamebainishwa muongozo wake rehema na amani ziwe juu yake, ikiwa ni pamoja na kumuiga katika hilo.
  2. Inapendekeza kuweka nguo au leso au mfano wa hayo mdomoni na puani mtu anapopiga chafya, ili kitu chochote kisitoke humo kitakachomuudhi mtu aliyekaa naye.
  3. Kupunguza sauti ya mtu wakati wa kupiga chafya kunahitajika, na ni ishara ya adabu kamili na maadili mema.
Marejeo

سنن أبي داود (7/ 375) (5029). سنن الترمذي (4/ 461) (2745). مسند أحمد (15/ 412) 9662). شرح رياض الصالحين، لابن عثيمين (4/ 440). تطريز رياض الصالحين، لفيصل آل مبارك (ص528). بهجة الناظرين، لسليم الهلالي (2/ 149). نزهة المتقين شرح رياض الصالحين، لمجموعة من الباحثين (1/ 678). كنوز رياض الصالحين لمجموعة من الباحثين (11/ 432).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Laiti nisingeliogopea uzito kwa waumini -au kwa umma wangu-; ningeliwaamrisha kupiga mswaki kila wakati wa swala

عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رضي الله عنه عَنِ النَّبِيِّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: «لَوْلَا أَنْ أَشُقَّ عَلَى الْمُؤْمِنِينَ -أَوْ: عَلَى أُمَّتِي- لَأَمَرْتُهُمْ بِالسِّوَاكِ عِنْدَ كُلِّ صَلَاةٍ».
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira -radhi za Allah ziwe juu yake- kutoka kwa Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Laiti nisingeliogopea uzito kwa waumini -au kwa umma wangu-; ningeliwaamrisha kupiga mswaki kila wakati wa swala".
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeDarajaSahihi
Maelezo

Anaeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake lau kama si hofu ya kuwatia tabu waumini katika umma wake basi angeliwawajibishia juu yao kutumia mswaki kwa kila swala.

Mafunzo
  1. Huruma ya Mtume rehema na amani ziwe juu yake kwa umma wake, na kuchelea kwake kuwatia tabu juu yao.
  2. Asili katika amri za Mtume rehema na amani ziwe juu yake ni ulazima, isipokuwa itakapokuja dalili kuwa ni sunna.
  3. Sunna ya kupiga mswaki na fadhila zake wakati wa kila swala.
  4. Amesema bin Daqiq Al-Idd: Hekima ya kufanywa sunna ya mswaki wakati wa kusimama katika swala ni kwa sababu ni mtu ajikurubisha kwa Mwenyezi Mungu, ikawa ni lazima awe katika hali ya ukamilifu na usafi na kuonyesha heshima ya ibada.
  5. Ujumla wa hadithi unajumuisha kupiga mswaki kwa mfungaji hata ikiwa baada ya kupinduka jua, kama swala mbili za Adhuhuri na Lasiri.
Marejeo

صحيح مسلم (1/ 220) (252). صحيح البخاري (2/ 4) (887). تيسير العلام شرح عمدة الأحكام، لعبد الله البسام (ص46). تنبيه الأفهام شرح عمدة الأحكام، لابن عثيمين (1/ 50).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Ya kwamba Mtume rehema na amani ziwe juu yake alikuwa anaposwali Alfajiri anakaa katika mswala wake mpaka Jua linachomoza vizuri

عَنْ جَابِرِ بْنِ سَمُرَةَ رَضيَ اللهُ عَنْهُ: أَنَّ النَّبِيَّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ كَانَ إِذَا صَلَّى الفَجْرَ جَلَسَ فِي مُصَلَّاهُ حَتَّى تَطْلُعَ الشَّمْسُ حَسَنًا، وَقَالَ: كَانَ لَا يَقُومُ مِنْ مُصَلَّاهُ الَّذِي يُصَلِّي فِيهِ الصُّبْحَ أَوِ الغَدَاةَ، حَتَّى تَطْلُعَ الشَّمْسُ، فَإِذَا طَلَعَتِ الشَّمْسُ قَامَ، وَكَانُوا يَتَحَدَّثُونَ فَيَأْخُذُونَ فِي أَمْرِ الجَاهِلِيَّةِ، فَيَضْحَكُونَ وَيَتَبَسَّمُ.
Kutoka kwa Jabiri bin Samura radhi za Allah ziwe juu yake: Ya kwamba Mtume rehema na amani ziwe juu yake alikuwa anaposwali Alfajiri anakaa katika mswala wake mpaka Jua linachomoza vizuri, na akasema: Alikuwa hanyanyuki kutoka katika mswala wake alioswalia hapo Alfajiri au asubuhi, mpaka linapochomoza Jua, basi linapochomoza Jua anasimama, na walikuwa wakizungumza wanajikuta wameingia katika mazungumzo ya zama za ujinga, wanacheka na yeye anatabasamu.
Imepokelewa Imamu MuslimDarajaSahihi
Maelezo

Na miongoni mwa sunna za Mtume rehema na amani ziwe juu yake ni kuwa anaposwali Alfajiri anakaa katika mswala wake mpaka Jua linachomoza kwa kunyanyuka, na alikuwa hasimami kutoka katika mswala wake aliouswalia Alfajiri, mpaka Jua lichomoze. Jua linapochomoza anasimama, na walikuwa wakizungumza wanachukua katika baadhi ya mambo yao ya kabla ya Uislamu na huku yeye kanyamaza, wanacheka, na huenda yeye akatabasamu pamoja nao.

Mafunzo
  1. Sunna ya kufanya dhikiri asubuhi mpaka Jua lichomoze, na kubaki katika kikao chake anapokuwa hana udhuru.
  2. Kumebainishwa hali aliyokuwa nayo Mtume rehema na amani ziwe juu yake miongoni mwa tabia njema na upole, kiasi kwamba alikuwa akikaa na Maswahaba zake, na akisikiliza mazungumzo yao na simulizi zao, na anatabasamu kwa sababu yake.
  3. Inafaa kufanya mazungumzo na kukumbushia enzi za ujinga msikitini.
  4. Inafaa kucheka na kutabasamu; kwa sababu kilichokatazwa ni kukithirisha kucheka.
Marejeo

صحيح مسلم (1/ 464) (670). البحر المحيط الثجاج في شرح صحيح الإمام مسلم بن الحجاج (14/ 407). المفهم لما أشكل من تلخيص كتاب مسلم (2/ 296).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Kila hadithi, daraja, maelezo na funzo hapa vinaonyeshwa kama HadeethEnc.com inavyovichapisha, kwa masharti yake ya kuchapisha upya. Daraja halimtaji aliyelitoa. Tafsiri na maelezo ni ya waandishi wake wenyewe, na baadhi hutaja hukumu; wahakiki wa Sabīl hawajavichunguza. Hadithi ya Kiarabu ndiyo matini. Chanzo: HadeethEnc.com