Imepokelewa kutoka kwa Baraa -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake amesema: Sijawahi kumuona mwenye nywele ndefu na vazi jekundu zuri kuliko Mtume wa Mwenyezi Mungu rehema na amani ziwe juu yake, nywele zake zinapigapiga mabega yake, na mabega yake yako mbali mbali, si mrefu wala mfupi.
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeDarajaSahihi
Maelezo
Anaeleza Baraa bin Azibi radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake ya kwamba hajawahi kumuona yeyote nywele za kichwa chake ni ndefu zimefika katika mabega yake, na anayevaa kikoi na shuka jeusi na lenye mistari myekundu zuri kuliko Mtume wa Mwenyezi Mungu rehema na amani ziwe juu yake, na kwamba miongoni mwa sifa zake za kimaumbile ni kwamba mabega yake yalikuwa mbali mbali, mwenye kifua kipana, na alikuwa na kimo cha kati na kati, kati mrefu na mfupi.
Mafunzo
Hapa kumebainishwa baadhi ya sifa nzuri za Mtume- rehema na amani ziwe juu yake- katika muonekano, kama uzuri wa nywele na upana wa kifua, na uzuri wa kimo, na mengineyo.
Mapenzi ya Maswahaba watukufu kwa Mtume- rehema na amani ziwe juu yake-, kiasi kwamba mpaka walikuwa wakielezea na wakiwanukulia waliokuja baada yao miongoni mwa muonekano wake na sifa zake za kimwili na za kimaana (zisizoonekana).
Marejeo
صحيح البخاري (4/ 188) (3551).
صحيح مسلم (4/ 1818) (2337).
تيسير العلام شرح عمدة الأحكام، لعبد الله البسام (ص730).
Imepokelewa kutoka kwa Aisha mama wa waumini radhi za Allah ziwe juu yake amesema: Alikuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake akipendezwa sana na kuanzia kulia, katika kuvaa kwake viatu, na kutana kwake nywele, na twahara yake, na katika mambo yake yote.
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeDarajaSahihi
Maelezo
Mtume rehema na amani ziwe juu yake alikuwa akipenda na akipendelea kuanza na upande wa kulia katika mambo yake yanayostahiki heshima, na miongoni mwake ni: Kuanza na mguu wa kulia katika kuvaa viatu vyake, na kuanzia kulia katika kutana nywele za kichwa chake, kuziachanisha kwake na kuzipaka kwake mafuta, na katika kutawadha kwake, anatanguliza kulia kabla ya kushoto katika mikono na miguu.
Mafunzo
Amesema Imam Nawawi: Hii ni kanuni endelevu katika Sheria, kuwa kila jambo la heshima na utukufu kama vile kuvaa nguo, suruali, kandambili, kuingia msikitini, kupiga mswaki, kupaka wanja, kukata kucha, kupunguza masharubu, kuchana nywele, kung'oa nywele za kwapa, kunyoa kichwa, kutoa salam ya kumaliza swala, na kuosha viungo kwa ajili ya usafi, na kutoka nje ya choo, kula na kunywa, kupeana mikono, kugusa Jiwe Jeusi, na mambo mengine yenye kufanana na haya, basi ni sunna kuanza na upande wa kulia, na ama yale yaliyo kinyume chake, kama vile kuingia chooni, kutoka msikitini, kukidhi haja ndogo, kujisafisha, kuvua nguo, suruali, kandambili, na kadhalika, haya ni sunna kuanza na upande wa kushoto, na yote hayo ni kwa sababu ya heshima ya upande wa kulia na utukufu wake.
"Anapendezwa na kuanzia kulia" Inajumuisha: Kuanza vitendo kwa mkono wa kulia, mguu wa kulia, upande wa kulia, na kushughulikia kitu kwa mkono wa kulia.
Amesema Imam Nawawi: Tambueni kuwa miongoni mwa sehemu za udhu kuna ambazo hazipendezi kuanzia kulia; ambazo ni masikio, viganja, na mashavu, bali vitasafishwa vyote kwa wakati mmoja, ikiwa halitowezekana hilo kama ilivyo kwa mtu aliyekatwa sikio na mfano wake; basi atatanguliza upande wa kulia.
Marejeo
صحيح البخاري (1/ 45) (168).
صحيح مسلم (1/ 226) (268).
Kila hadithi, daraja, maelezo na funzo hapa vinaonyeshwa kama HadeethEnc.com inavyovichapisha, kwa masharti yake ya kuchapisha upya. Daraja halimtaji aliyelitoa. Tafsiri na maelezo ni ya waandishi wake wenyewe, na baadhi hutaja hukumu; wahakiki wa Sabīl hawajavichunguza. Hadithi ya Kiarabu ndiyo matini. Chanzo: HadeethEnc.com