Alikuwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- anapopiga chafya anaweka mkono wake au nguo yake juu ya kinywa chake, na anapunguza sauti yake
عن أبي هريرة رضي الله عنه قال: كان رسولُ الله صلى الله عليه وسلم إذا عَطَس وضَعَ يَدَه -أو ثوبَهُ- على فيهِ، وخَفَضَ -أو غضَّ- بها صوتَهُ.
Kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Alikuwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- anapopiga chafya anaweka mkono wake au nguo yake juu ya kinywa chake, na anapunguza sauti yake.
Imepokelewa na Abu Daud, Tirmidhiy na AhmadDarajaSahihi
Maelezo
Alikuwa rehema na amani ziwe juu yake anapopiga chafya:
Jambo la kwanza: Anaweka mkono wake, au nguo yake juu ya kinywa chake; Kisije kutoka kinywani mwake au puani mwake chochote kitakachomuudhi aliyekaa naye.
Jambo la pili: Anashusha sauti yake na wala hainyanyui.
Mafunzo
Hapa pamebainishwa muongozo wake rehema na amani ziwe juu yake, ikiwa ni pamoja na kumuiga katika hilo.
Inapendekeza kuweka nguo au leso au mfano wa hayo mdomoni na puani mtu anapopiga chafya, ili kitu chochote kisitoke humo kitakachomuudhi mtu aliyekaa naye.
Kupunguza sauti ya mtu wakati wa kupiga chafya kunahitajika, na ni ishara ya adabu kamili na maadili mema.
Marejeo
سنن أبي داود (7/ 375) (5029).
سنن الترمذي (4/ 461) (2745).
مسند أحمد (15/ 412) 9662).
شرح رياض الصالحين، لابن عثيمين (4/ 440).
تطريز رياض الصالحين، لفيصل آل مبارك (ص528).
بهجة الناظرين، لسليم الهلالي (2/ 149).
نزهة المتقين شرح رياض الصالحين، لمجموعة من الباحثين (1/ 678).
كنوز رياض الصالحين لمجموعة من الباحثين (11/ 432).
Kila hadithi, daraja, maelezo na funzo hapa vinaonyeshwa kama HadeethEnc.com inavyovichapisha, kwa masharti yake ya kuchapisha upya. Daraja halimtaji aliyelitoa. Tafsiri na maelezo ni ya waandishi wake wenyewe, na baadhi hutaja hukumu; wahakiki wa Sabīl hawajavichunguza. Hadithi ya Kiarabu ndiyo matini. Chanzo: HadeethEnc.com