عن أبي هريرة رضي الله عنه قال: كان رسولُ الله صلى الله عليه وسلم إذا عَطَس وضَعَ يَدَه -أو ثوبَهُ- على فيهِ، وخَفَضَ -أو غضَّ- بها صوتَهُ.
Kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Alikuwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- anapopiga chafya anaweka mkono wake au nguo yake juu ya kinywa chake, na anapunguza sauti yake.
Imepokelewa na Abu Daud, Tirmidhiy na AhmadDarajaSahihi
Maelezo
Alikuwa rehema na amani ziwe juu yake anapopiga chafya:
Jambo la kwanza: Anaweka mkono wake, au nguo yake juu ya kinywa chake; Kisije kutoka kinywani mwake au puani mwake chochote kitakachomuudhi aliyekaa naye.
Jambo la pili: Anashusha sauti yake na wala hainyanyui.
Mafunzo
- Hapa pamebainishwa muongozo wake rehema na amani ziwe juu yake, ikiwa ni pamoja na kumuiga katika hilo.
- Inapendekeza kuweka nguo au leso au mfano wa hayo mdomoni na puani mtu anapopiga chafya, ili kitu chochote kisitoke humo kitakachomuudhi mtu aliyekaa naye.
- Kupunguza sauti ya mtu wakati wa kupiga chafya kunahitajika, na ni ishara ya adabu kamili na maadili mema.
Marejeo
سنن أبي داود (7/ 375) (5029).
سنن الترمذي (4/ 461) (2745).
مسند أحمد (15/ 412) 9662).
شرح رياض الصالحين، لابن عثيمين (4/ 440).
تطريز رياض الصالحين، لفيصل آل مبارك (ص528).
بهجة الناظرين، لسليم الهلالي (2/ 149).
نزهة المتقين شرح رياض الصالحين، لمجموعة من الباحثين (1/ 678).
كنوز رياض الصالحين لمجموعة من الباحثين (11/ 432).
Hadithi hii kwenye HadeethEnc.comعن أبي هريرة رضي الله عنه قال: سمعت رسول الله صلى الله عليه وسلم يقول: «حَقُّ الْمُسْلِمِ عَلَى الْمُسْلِمِ خَمْسٌ: رَدُّ السَّلَامِ، وَعِيَادَةُ الْمَرِيضِ، وَاتِّبَاعُ الْجَنَائِزِ، وَإِجَابَةُ الدَّعْوَةِ، وَتَشْمِيتُ الْعَاطِسِ».
Imepokelewa Kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Nilimsikia Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akisema: "Haki za muislamu juu ya muislamu mwenzake ni tano: Kujibu salamu, na kumtembelea mgonjwa, na kufuata jeneza, na kuitika wito, na kumuombea dua mwenye kupiga chafya".
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeDarajaSahihi
Maelezo
Amebainisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- baadhi ya haki za muislamu juu ya ndugu yake muislamu, Haki ya kwanza katika hizi ni kujibu salamu kwa atakayekutolea salamu.
Haki ya pili: Kumtembelea mgonjwa na kumzuru.
Haki ya tatu: Kulifuata jeneza kutoka nyumbani kwake mpaka mahali pa kuswalia mpaka makaburini mpaka kuzika.
Haki ya nne: Kuitika wito anapomuita kuja katika walima wa harusi na mengineyo.
Haki ya tano: Kumuombea dua mwenye kupiga chafya, nako ni kumwambia -Yarhamukallaah- (Akuhurumie Mwenyezi Mungu) atakapomhimidi Allah kwa kusema (Al-hamdulillah): kisha mpiga chafya amjibu: -Yahdiikumullaahu wayuslih baalakum- (Akuongozeni Allah na akutengenezeeni mambo yenu).
Mafunzo
- Utukufu wa Uislamu katika kuzitilia mkazo haki baina ya waislamu na kuupa nguvu udugu na mapenzi kati yao.
Marejeo
صحيح البخاري (2/ 71) (1240).
صحيح مسلم (4/ 1704) (2162).
كنوز رياض الصالحين، لمجموعة من الباحثين (4/ 512).
بهجة الناظرين شرح رياض الصالحين، لسليم الهلالي (1/ 327).
نزهة المتقين شرح رياض الصالحين، مجموعة من الباحثين (1/ 253).
شرح رياض الصالحين، لابن عثيمين (2/ 591).
بهجة قلوب الأبرار، لابن سعدي (ص81).
Hadithi hii kwenye HadeethEnc.comعَن أَبِي سَعِيدٍ الْخُدْرِيِّ رضي الله عنه قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: «إِذَا تَثَاءَبَ أَحَدُكُمْ فَلْيُمْسِكْ بِيَدِهِ عَلَى فِيهِ، فَإِنَّ الشَّيْطَانَ يَدْخُلُ».
Imepokelewa kutoka kwa Saidi Al-Khuduriy -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -rehema na amani ziwe juu yake-: "Atakapopiga mwayo mmoja wenu basi na ashike mkono wake juu ya kinywa chake, kwani Shetani huingia".
Imepokelewa Imamu MuslimDarajaSahihi
Maelezo
Amemuelekeza Mtume rehema na amani ziwe juu yake mwenye kupiga mwayo pale alipofungua kinywa chake kwa sababu ya uvivu au kujaa na mfano wake; kuwa aweke mkono wake juu ya kinywa chake ili akifunge kwa mkono; na hii ni kwa sababu Shetani huingia ndani yake anapokiacha wazi, kuweka mkono kunakuwa ni kizuizi cha kumzuia kuingia.
Mafunzo
- Atakapotaka mtu kupiga miayo anatakiwa auzuie kwa kadiri awezavyo, kwa kuuzuia mdomo wake, na aubakishe ukiwa umefungwa wala usifunguke, asipoweza kuubakisha mdomo wake ukiwa umefungwa basi aweke mkono wake juu ya mdomo wake, afunike kinywa chake kwa mkono wake.
- Kushikamana na adabu za kiislamu katika hali zote; kwa sababu ndio anwani ya ukamilifu na tabia njema.
- Kuchukua tahadhari ya kila mapitio ya Shetani kwa mwanadamu.
Marejeo
صحيح مسلم (4/ 2293) (2995).
بهجة الناظرين شرح رياض الصالحين، لسليم الهلالي (2/ 151).
شرح رياض الصالحين، لابن عثيمين (4/ 436).
تطريز رياض الصالحين، لفيصل آل مبارك (ص529).
نزهة المتقين شرح رياض الصالحين، مجموعة من الباحثين (1/ 679).
Hadithi hii kwenye HadeethEnc.comعَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رضي الله عنه أَنَّ رَسُولَ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: «حَقُّ الْمُسْلِمِ عَلَى الْمُسْلِمِ سِتٌّ» قِيلَ: مَا هُنَّ يَا رَسُولَ اللهِ؟، قَالَ: «إِذَا لَقِيتَهُ فَسَلِّمْ عَلَيْهِ، وَإِذَا دَعَاكَ فَأَجِبْهُ، وَإِذَا اسْتَنْصَحَكَ فَانْصَحْ لَهُ، وَإِذَا عَطَسَ فَحَمِدَ اللهَ فَسَمِّتْهُ، وَإِذَا مَرِضَ فَعُدْهُ وَإِذَا مَاتَ فَاتَّبِعْهُ».
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- yakwamba Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Haki za muislamu juu ya muislamu mwenzake ni sita" Pakasemwa: Na ni zipi hizo ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu?, akasema: "Ukikutana naye msalimie, na akikuita muitikie, na akikutaka nasaha mnasihi, na akipiga chafya akamhimidi Mwenyezi Mungu basi muombee dua ya rehema, na akiugua mtembelee, na akifariki msindikize".
Imepokelewa Imamu MuslimDarajaSahihi
Maelezo
Amebainisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa miongoni mwa haki za muislamu juu ya ndugu yake muislamu ni mambo sita: La kwanza: Amsalimie akikutana naye kwa kusema: Assalaam alaikum, naye atajibu salamu kwa kusema: Waalaikumussalaam. La pili: Kuitika wito wake atakapomuita kwa ajili ya sherehe ya harusi au nyingineyo. La tatu: Kumpa nasaha akizihitajia, na wala usimsifie bure, au kumfanyia udanganyifu. La nne: Akipiga chafya akasema: Alhamdulillaah, basi muombee dua kwa kusema: Yar-hamkallaah (Akuhurumie Mwenyezi Mungu), naye ajibu kwa kusema: Yah-diikumullaahu wayuslih baalakum (Akuongozeni Mwenyezi Mungu na kutengenezeeni hali zenu). La tano: Akamuone na amtembelee atakapougua. La sita: Amswalie atakapofariki, na alisindikize jeneza lake mpaka azikwe.
Mafunzo
- Amesema Shaukani: Na makusudio ya kauli yake: (Haki za muislamu) Nikuwa haitakiwi kuziacha, na kunakuwa kuzifanya kwake ima ni wajibu au sunna iliyotiwa mkazo inayofanana na wajibu ambayo haitakikani kuiacha.
- Kujibu salamu ni faradhi ya lazima, mwenye kusalimiwa atakapokuwa mmoja, na wakiwa wengi basi mmoja anatosheleza, ama kuanza salamu asili yake ni sunna.
- Mgonjwa kutembelewa ni katika haki zake juu ya ndugu zake waislamu; kwa sababu humuingizia furaha na liwazo ndani ya moyo wake, na ni faradhi ya kujitosheleza, wakifanya wenye kutosheleza basi wengine hawana dhambi.
- Uwajibu wa kuitika wito kukiwa hakuna madhmbi ndani yake; ikiwa ni wito wa sherehe ya harusi basi jopo la wanachuoni wamesema kuwa ni wajibu kuitika, isipokuwa kukiwa na udhuru wa kisheria, ama ikiwa si sherehe ya harusi jopo la wanachuoni wakasema kuwa ni sunna.
- Kumuombea dua aliyepiga chafya ni wajibu juu ya yule aliyesikia kumhimidiwa Mwenyezi Mungu mpiga chafya.
- Ukamilifu wa sheria na pupa yake katika kuunganisha nguvu na umoja wa jamii na imani, na nyenzo za mapenzi kati ya mtu mmoja mmoja.
- "Muombee rehema" Yaani kumuombea dua ya kheri na baraka, na tashmiiti (kumuombea dua) imesemekana maana yake: Mwenyezi Mungu akuweke mbali na kuchekwa na maadui, na ayaweke mbali nawe yale yatakayofanya adui yako akucheke, na tasmiit (kwa siin): Maana yake: Mwenyezi Mungu akuongoze katika ustaarabu ulionyooka.
Marejeo
صحيح مسلم (4/ 1705) (2162).
منحة العلام في شرح بلوغ المرام، لعبد الله الفوزان (10/ 7).
توضيح الأحكام من بلوغ المرام، للبسام (3/ 128).
بهجة الناظرين شرح رياض الصالحين، لسليم الهلالي (1/ 327).
Hadithi hii kwenye HadeethEnc.comKila hadithi, daraja, maelezo na funzo hapa vinaonyeshwa kama HadeethEnc.com inavyovichapisha, kwa masharti yake ya kuchapisha upya. Daraja halimtaji aliyelitoa. Tafsiri na maelezo ni ya waandishi wake wenyewe, na baadhi hutaja hukumu; wahakiki wa Sabīl hawajavichunguza. Hadithi ya Kiarabu ndiyo matini. Chanzo: HadeethEnc.com