عَنْ عَائِشَةَ أُمِّ المُؤمنينَ رضي الله عنها قَالَتْ: كَانَ النَّبِيُّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ يُعْجِبُهُ التَّيَمُّنُ، فِي تَنَعُّلِهِ، وَتَرَجُّلِهِ، وَطُهُورِهِ، وَفِي شَأْنِهِ كُلِّهِ.
Imepokelewa kutoka kwa Aisha mama wa waumini radhi za Allah ziwe juu yake amesema: Alikuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake akipendezwa sana na kuanzia kulia, katika kuvaa kwake viatu, na kutana kwake nywele, na twahara yake, na katika mambo yake yote.
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeDarajaSahihi
Maelezo
Mtume rehema na amani ziwe juu yake alikuwa akipenda na akipendelea kuanza na upande wa kulia katika mambo yake yanayostahiki heshima, na miongoni mwake ni: Kuanza na mguu wa kulia katika kuvaa viatu vyake, na kuanzia kulia katika kutana nywele za kichwa chake, kuziachanisha kwake na kuzipaka kwake mafuta, na katika kutawadha kwake, anatanguliza kulia kabla ya kushoto katika mikono na miguu.
Mafunzo
- Amesema Imam Nawawi: Hii ni kanuni endelevu katika Sheria, kuwa kila jambo la heshima na utukufu kama vile kuvaa nguo, suruali, kandambili, kuingia msikitini, kupiga mswaki, kupaka wanja, kukata kucha, kupunguza masharubu, kuchana nywele, kung'oa nywele za kwapa, kunyoa kichwa, kutoa salam ya kumaliza swala, na kuosha viungo kwa ajili ya usafi, na kutoka nje ya choo, kula na kunywa, kupeana mikono, kugusa Jiwe Jeusi, na mambo mengine yenye kufanana na haya, basi ni sunna kuanza na upande wa kulia, na ama yale yaliyo kinyume chake, kama vile kuingia chooni, kutoka msikitini, kukidhi haja ndogo, kujisafisha, kuvua nguo, suruali, kandambili, na kadhalika, haya ni sunna kuanza na upande wa kushoto, na yote hayo ni kwa sababu ya heshima ya upande wa kulia na utukufu wake.
- "Anapendezwa na kuanzia kulia" Inajumuisha: Kuanza vitendo kwa mkono wa kulia, mguu wa kulia, upande wa kulia, na kushughulikia kitu kwa mkono wa kulia.
- Amesema Imam Nawawi: Tambueni kuwa miongoni mwa sehemu za udhu kuna ambazo hazipendezi kuanzia kulia; ambazo ni masikio, viganja, na mashavu, bali vitasafishwa vyote kwa wakati mmoja, ikiwa halitowezekana hilo kama ilivyo kwa mtu aliyekatwa sikio na mfano wake; basi atatanguliza upande wa kulia.
Marejeo
صحيح البخاري (1/ 45) (168).
صحيح مسلم (1/ 226) (268).
Hadithi hii kwenye HadeethEnc.comعَنْ أَنَسٍ رضي الله عنه: أَنَّ نَفَرًا مِنْ أَصْحَابِ النَّبِيِّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ سَأَلُوا أَزْوَاجَ النَّبِيِّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ عَنْ عَمَلِهِ فِي السِّرِّ؟ فَقَالَ بَعْضُهُمْ: لَا أَتَزَوَّجُ النِّسَاءَ، وَقَالَ بَعْضُهُمْ: لَا آكُلُ اللَّحْمَ، وَقَالَ بَعْضُهُمْ: لَا أَنَامُ عَلَى فِرَاشٍ، فَحَمِدَ اللهَ وَأَثْنَى عَلَيْهِ، فَقَالَ: «مَا بَالُ أَقْوَامٍ قَالُوا كَذَا وَكَذَا؟ لَكِنِّي أُصَلِّي وَأَنَامُ، وَأَصُومُ وَأُفْطِرُ، وَأَتَزَوَّجُ النِّسَاءَ، فَمَنْ رَغِبَ عَنْ سُنَّتِي فَلَيْسَ مِنِّي».
Imepokelewa kutoka kwa Anas -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe ju yake-: Ya kwamba kuna kundi miongoni mwa wanafunzi wa Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- waliwauliza wake za Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- kuhusu amali zake za siri? (walipojibiwa) wakasema baadhi yao: Mimi sitooa wanawake. Na wakasema baadhi yao: Na mimi sitokula nyama. Na wakasema baadhi yao: Sitolala juu ya godoro. Hilo likamfikia Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- akamshukuru Mwenyezi Mungu na akamsifia, na akasema: "Wana nini watu waliosema kadhaa wa kadhaa? lakini mimi ninaswali na ninalala na ninafunga na ninakula, na ninaoa wanawake; atakayeuchukia muongozo wangu basi hayuko nami".
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeDarajaSahihi
Maelezo
Lilikuja kundi la Maswahaba radhi za Allah ziwe juu yao, katika nyumba za wake za Mtume rehema na amani ziwe juu yake, wakiuliza kuhusu ibada zake za siri ndani ya nyumba yake, walipoelezwa wakawa kana kwamba za kwao wameziona ndogo, wakasema: Na tuko wapi sisi na Mtume rehema na amani ziwe juu yake? hali yakuwa amekwisha samehewa yaliyotangulia katika madhambi yake na yajayo, ukilinganisha na ambaye hajajua hata kupatikana kwa msamaha, huyu anahitaji kupitiliza katika kufanya ibada huenda akaupata msamaha huo. Kisha wakasema baadhi yao: Sitooa wanawake. Na wakasema baadhi yao: Sitokula nyama. Na wakasema baadhi yao: Sitolala katika godoro. Hilo likamfikia Mtume rehema na amani ziwe juu yake, akachukia, na akawahutubia watu, akamhimidi Mwenyezi Mungu na akamtukuza, na akasema: Wana nini watu fulani waliosema kadhaa wa kadhaa?! Wallahi mimi ndiye ninayemuhofu sana Mwenyezi Mungu kuliko watu wote na ndiyo mchamungu wenu, lakini ninalala ili nipate nguvu ya kusimama, na ninafungua ili nipate nguvu ya kufunga, na ninaoa wanawake, atakayeipuuza njia yangu, na akaona njia nyingine ndio iliyokamilika, na akachukua njia ya asiyekuwa mimi, huyu hayuko nami.
Mafunzo
- Mapenzi ya kheri kwa Maswahaba radhi za Allah ziwe juu yao, na shauku yao juu yake, na kwa baadhi yao kumuiga Mtume rehema na amani ziwe juu yake.
- Upole wa sheria hii na wepesi wake, kwa kuchukua kutoka katika matendo ya Nabii wao na muongozo wake.
- Kheri na baraka iko katika kumuiga Mtume rehema na amani ziwe juu yake, na kwa kufuata hali zake tukufu.
- Kemeo la kuitilia mkazo nafsi katika ibada kwa yale isiyoyaweza, nakuwa hili ni katika hali za wazushi.
- Amesema bin Hajari: Kuchukua kwa mkazo katika ibada kunapelekea katika uchovu unaokata asili yake, na kudumu na kuishia katika faradhi peke yake, na kuacha kufanya sunna kunapelekea kuamsha uvivu, na kukosa uchangamfu katika ibada, na jambo bora ni la kati na kati.
- Hapa kuna fundisho la kufuatilia hali za wakubwa kwa ajili kuiga kutoka katika matendo yao, nakuwa inaposhindikana kulijua hilo kutoka kwa wanaume inafaa kulibaini hilo kutoka kwa wanawake.
- Hapa kuna mawaidha na kutoa maswala ya kielemu na kubainisha hukumu kwa watu wazima, na kuondoa utata kwa wale wenye kujitahidi.
- Amri ya kujihurumia katika ibada, ikiwa ni pamoja na kuihifadhi na kuzihifadhi faradhi na sunna; ili muislamu achunge haki za mtu mwingine.
- Katika hadithi kuna dalili juu ya fadhila za ndoa na himizo lake.
Marejeo
صحيح البخاري (7/ 2) (5063).
صحيح مسلم (2/ 1020) (1401).
تيسير العلام شرح عمدة الأحكام، لعبد الله البسام (ص566).
خلاصة الكلام شرح عمدة الأحكام، لفيصل آل مبارك (ص282).
Hadithi hii kwenye HadeethEnc.comعَنْ عَائِشَةَ أُمِّ المُؤْمِنينَ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهَا قَالَتْ: مَا أَكَلَ آلُ مُحَمَّدٍ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ أَكْلَتَيْنِ فِي يَوْمٍ إِلَّا إِحْدَاهُمَا تَمْرٌ.
Imepokelewa kutoka kwa Aisha mama wa waumini radhi za Allah ziwe juu yake amesema: Hakuwahi kula Muhammadi rehema na amani ziwe juu yake milo miwili kwa siku isipokuwa mlo mmoja utakuwa ni tende.
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeDarajaSahihi
Maelezo
Anaeleza mama wa waumini Aisha radhi za Allah ziwe juu yake kwamba watu wa nyumba ya Mtume rehema na amani ziwe juu yake hawakuwahi kula milo miwili kwa siku moja isipokuwa mlo mmoja kati ya hiyo utakuwa ni tende.
Mafunzo
- Unyenyekevu wa Mtume rehema na amani ziwe juu yake na watu wa nyumba yake, huenda kuna wakati hawakupata mlo zaidi ya mmoja.
- Tende ilikuwa rahisi kwao kuliko chochote.
- Ubora wa kuipa nyongo dunia na kutosheka na kichache katika maisha, na kuwa hilo ni katika tabia za Mtume rehema na amani ziwe juu yake bwana wa Mitume.
- Kula milo miwili kwa siku ni katika mambo halali na yanayofaa, nayo ni katika desturi za Waarabu inafahamika, walikuwa wakila kwa siku milo miwili, chakula cha mchana, na chakula cha usiku.
Marejeo
صحيح البخاري (8/ 97) (6455).
صحيح مسلم (4/ 2282) (2971).
فتح الباري لابن حجر (11/ 292).
Hadithi hii kwenye HadeethEnc.comعَنْ عَائِشَةَ أُمِّ المُؤْمِنينَ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهَا قَالَتْ: مَا شَبِعَ آلُ مُحَمَّدٍ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ مُنْذُ قَدِمَ المَدِينَةَ مِنْ طَعَامِ البُرِّ ثَلاَثَ لَيَالٍ تِبَاعًا، حَتَّى قُبِضَ.
Imepokelewa kutoka kwa Aisha mama wa waumini radhi za Allah ziwe juu yake: Hawakuwahi kushiba katika chakula cha ngano watu wa famili ya Muhammadi rehema na amani ziwe juu yake tangu alipofika Madina, kwa siku tatu mfululizo, mpaka alipofariki.
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeDarajaSahihi
Maelezo
Anaeleza mama wa waumini Aisha radhi za Allah ziwe juu yake kuwa, watu wa nyumba ya Mtume rehema na amani ziwe juu yake hawakuwahi kushiba tangu walipoingia Madina kwa chakula cha ngano kwa muda wa siku tatu mfululizo, mpaka alipofariki rehema na amani ziwe juu yake.
Mafunzo
- Kumebainishwa hali aliyokuwa nayo Mtume rehema na amani ziwe juu yake ya maisha ya chini, kwani maisha halisi ni maisha ya Akhera.
- Amesema bin Hajari: Na kinachoonekana nikuwa sababu ya kutoshiba kwao mara nyingi ilikuwa ni kwa sababu ya uchache wa upatikanaji wa chochote kwao, yaani walikuwa wakipata chakula lakini walikuwa wakithamini wenye shida zaidi yao kuliko nafsi zao.
Marejeo
صحيح البخاري (7/ 75) (5416).
صحيح مسلم (4/ 2282) (2970).
المفهم لما أشكل من تلخيص كتاب مسلم (7/ 129).
البحر المحيط الثجاج في شرح صحيح الإمام مسلم بن الحجاج (45/ 129).
Hadithi hii kwenye HadeethEnc.comعَنْ عَائِشَةَ أُمِّ المُؤْمِنينَ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهَا قَالَتْ: كَانَ فِرَاشُ رَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ مِنْ أَدَمٍ، وَحَشْوُهُ مِنْ لِيفٍ، وَلِمُسلمٍ: كَانَ وِسَادَةُ رَسُولِ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ الَّتِي يَتَّكِئُ عَلَيْهَا مِنْ أَدَمٍ حَشْوُهَا لِيفٌ.
Imepokelewa kutoka kwa Aisha mama wa waumini radhi za Allah ziwe juu yake amesema: Lilikuwa tandiko la Mtume rehema na amani ziwe juu yake ni kutokana na ngozi, na ndani limejazwa majani ya mitende, na katika riwaya ya Muslim: ulikuwa mto wa Mtume rehema na amani ziwe juu yake aliokuwa akiegamia umetokana na ngozi ndani umejazwa majani.
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeDarajaSahihi
Maelezo
Ameeleza mama wa waumini Aisha radhi za Allah ziwe juu yake kuwa godoro alilokuwa akilalia Mtume rehema na amani ziwe juu yake lilikuwa limetengenezwa kwa ngozi, na limejazwa majani ya mitende, na vile vile mto wake aliokuwa akiegemea.
Mafunzo
- Kumebainishwa hali aliyokuwa nayo Mtume rehema na amani ziwe juu yake kama vile kuipa nyongo dunia na kuzipuuza ladha za dunia, pamnoja nakuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu alimpa uwezo wa hilo lau kama angetaka kustarehe nayo.
- Inafaa kutumia magodoro na mito, na kuvilalia na kuwa juu yake.
- Muislamu anatakiwa kuzingatia hali yake na hali ya maisha ya Nabii wake rehema na amani ziwe juu yake. Kwani yeye ndiye kiigizo chema, na kwamba mwenye kuiga nyenendo zake ataongoka na atafaulu duniani na Akhera.
- Kuwa na pupa ya kuiandaa Akhera, na muumini atosheke katika dunia na kile kinachomsaidia katika kumtii Mwenyezi Mungu, na asishughulike na kutafuta wingi wa mali ndani yake, na aliwakemea Mwenyezi Mungu watu, akasema: "Kumekupumbazeni kutafuta wingi (wa mali) mpaka mkayazuru makaburi" [Takathur: 1-2].
Marejeo
صحيح البخاري (8/ 97) (6456).
صحيح مسلم (3/ 1650) (2082).
البحر المحيط الثجاج في شرح صحيح الإمام مسلم بن الحجاج (34/ 662).
إرشاد الساري لشرح صحيح البخاري (9/ 264).
المفهم لما أشكل من تلخيص كتاب مسلم (5/ 403).
النهاية في غريب الحديث والأثر (971).
Hadithi hii kwenye HadeethEnc.comعَنْ عَمْرِو بْنِ الحَارِثِ خَتَنِ رَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ أَخِي أُمِّ المؤمِنين جُوَيْرِيَةَ بِنْتِ الحَارِثِ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُم، قَالَ: مَا تَرَكَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ عِنْدَ مَوْتِهِ دِرْهَمًا وَلاَ دِينَارًا وَلاَ عَبْدًا وَلاَ أَمَةً وَلاَ شَيْئًا، إِلَّا بَغْلَتَهُ البَيْضَاءَ، وَسِلاَحَهُ، وَأَرْضًا جَعَلَهَا صَدَقَةً.
Kutoka kwa Amri bin Harithi shemeji yake na Mtume rehema na amani ziwe juu yake, kaka yake na mama wa waumini Juwairia binti Harithi radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao, amesema: Hakuacha Mtume rehema na amani ziwe juu yake wakati wa kifo chake Dirham moja wala Dinari, wala mtumwa wala kijakazi wala chochote, isipokuwa nyumbu wake mweupe, na silaha yake, na kipande cha Ardhi alichokitoa kama sadaka.
Imepokelewa na Al-BukhaariyDarajaSahihi
Maelezo
Alifariki Mtume rehema na amani ziwe juu yake na wala hakuacha Dirham ya fedha wala Dinari ya dhahabu, wala mtumwa mmilikiwa wala kijakazi mmilikiwa, wala mbuzi wala ngamia wala chochote katika mali, isipokuwa nyumbu wake mweupe aliyekuwa akimpanda, na silaha yake aliyokuwa akiibeba, na kipande cha Ardhi alichokitoa wakfu kwa ajili ya wasafiri.
Mafunzo
- Manabii hawarithiwi.
- Kumebainishwa alivyoviacha Mtume rehema na amani ziwe juu yake baada ya kifo chake.
- Alifariki Mtume rehema na amani ziwe juu yake na wala hakuacha kitu chochote cha msingi, kutokana na ukarimu wake na utoaji wake na wema wake.
- Amesema Al-Karmani: Dhamiri katika kauli yake "na akavifanya" hii inarudi katika vitu vitatu: Yaani; nyumbu na silaha na Ardhi na si katika Ardhi peke yake.
- Shemeji: Ni kaka wa dada, na neno "Akhtani" hutumika kwa ndugu wa mwanamke.
Marejeo
صحيح البخاري (4/ 2) (2739).
النهاية في غريب الحديث والأثر (254).
فتح الباري لابن حجر (5/ 360).
عمدة القاري شرح صحيح البخاري (14/ 31).
Hadithi hii kwenye HadeethEnc.comعَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ قَالَ: قِيلَ: يَا رَسُولَ اللهِ ادْعُ عَلَى المُشْرِكِينَ قَالَ: «إِنِّي لَمْ أُبْعَثْ لَعَّانًا، وَإِنَّمَا بُعِثْتُ رَحْمَةً».
Kutoka kwa Abuu Huraira radhi za Allah ziwe juu yake amesema: Palisemwa: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu waombee dua mbaya washirikina, akasema: "Hakika mimi sikutumwa kuwa mtoa laana, bali nilitumwa kuwa huruma".
Imepokelewa Imamu MuslimDarajaSahihi
Maelezo
Alitakwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake awaombee washirikina dua mbaya kwa Mwenyezi Mungu, akasema: Hakika mimi sikuagizwa na Mwenyezi Mungu na sikutumwa kuwa mtoa laana na kuwaombea watu kuwekwa mbali na rehema ya Mwenyezi Mungu na niwakatie heri, mimi sikutumwa kwa hayo, bali nilitumwa niwe sababu ya heri na rehema kwa watu wote, na kwa waumini hasa.
Mafunzo
- Ukamilifu wa tabia zake rehema na amani ziwe juu yake.
- Umuhimu wa kuusafisha ulimi kutokana na laana kwa kumuiga Mtume rehema na amani ziwe juu yake.
- Hapa kuna katazo la kutoa laana.
- Himizo la kuwahurumia watu.
Marejeo
صحيح مسلم (4/ 2006) (2599).
المفهم لما أشكل من تلخيص كتاب مسلم (6/ 582).
البحر المحيط الثجاج في شرح صحيح الإمام مسلم بن الحجاج (40/ 683).
Hadithi hii kwenye HadeethEnc.comKila hadithi, daraja, maelezo na funzo hapa vinaonyeshwa kama HadeethEnc.com inavyovichapisha, kwa masharti yake ya kuchapisha upya. Daraja halimtaji aliyelitoa. Tafsiri na maelezo ni ya waandishi wake wenyewe, na baadhi hutaja hukumu; wahakiki wa Sabīl hawajavichunguza. Hadithi ya Kiarabu ndiyo matini. Chanzo: HadeethEnc.com