Ruka hadi kwenye maudhui
Hadithi zenye maelezo

Muongozo wake Mtume Rehema na Amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake katika swala

Hadithi 4

Nilihifadhi kutoka kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- rakaa kumi

عَنِ ابْنِ عُمَرَ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُمَا قَالَ: حَفِظْتُ مِنَ النَّبِيِّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ عَشْرَ رَكَعَاتٍ: رَكْعَتَيْنِ قَبْلَ الظُّهْرِ، وَرَكْعَتَيْنِ بَعْدَهَا، وَرَكْعَتَيْنِ بَعْدَ المَغْرِبِ فِي بَيْتِهِ، وَرَكْعَتَيْنِ بَعْدَ العِشَاءِ فِي بَيْتِهِ، وَرَكْعَتَيْنِ قَبْلَ صَلاَةِ الصُّبْحِ، وَكَانَتْ سَاعَةً لاَ يُدْخَلُ عَلَى النَّبِيِّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ فِيهَا، حَدَّثَتْنِي حَفْصَةُ أَنَّهُ كَانَ إِذَا أَذَّنَ المُؤَذِّنُ وَطَلَعَ الفَجْرُ صَلَّى رَكْعَتَيْنِ، وَفِي لَفْظٍ: أَنَّ النَّبِيَّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ كَانَ يُصَلِّي بَعْدَ الْجُمُعَةِ رَكْعَتَيْنِ.
Imeokewa Kutoka kwa bin Omari Radhi za Allah ziwe juu yake yeye na baba yake, amesema : Nilihifadhi kutoka kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- rakaa kumi: Rakaa mbili kabla ya Dhuhuri, na rakaa mbili baada yake, na rakaa mbili baada ya Magharibi nyumbani kwake, na rakaa mbili baada ya Ishaa nyumbani kwake, na rakaa mbili kabla ya swala ya Alfajiri, na muda huo ulikuwa ni wakati ambao haruhusiwi yeyote kuingia kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-, Hafswa ndiye aliyenisimulia kuwa alikuwa anapoadhini muadhini na ikachomoza Alfajiri anaswali rakaa mbili, na katika riwaya nyingine: Nikuwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- alikuwa akiswali baada ya Ijumaa rakaa mbili.
Imepokelewa na Al-Bukhaariy na Muslim katika riwaya zake zoteDarajaSahihi
Maelezo

Anabainisha Abdullahi bin Omari Radhi za Allah ziwe juu yake yeye na baba yake: Yakuwa miongoni mwa swala za sunna alizozihifadhi kutoka kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- ni rakaa kumi na huitwa kuwa ni sunna zilizopangiliwa, Rakaa mbili kabla ya Dhuhuri, na rakaa mbili baada yake, na rakaa mbili baada ya Magharibi nyumbani kwake, na rakaa mbili baada ya Ishaa nyumbani kwake, Na kabla ya Alfajiri rakaa mbili, Zikatimia rakaa kumi. Na ama swala ya Ijumaa aliswali baada yake rakaa mbili.

Mafunzo
  1. Imendezeshwa kuswali rakaa hizi zilizopangiliwa, na kudumu nazo.
  2. Sheria ya kuswali sunna nyumbani.
Marejeo

صحيح البخاري (2/ 58-59) (1180، 1181). صحيح مسلم (2/ 601) (882). تيسير العلام شرح عمدة الأحكام، للبسام (ص112).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Yakwamba Nabii -Rehema na Amani ziwe juu yake- alikuwa safarini, akaswali swala ya ishaa ya mwisho, akasoma katika moja ya rakaa mbili kwa sura ya wattin wazzaitun, sijawahi kumsikia yeyote mwenye sauti nzuri au kisomo kizuri zaidi yake

عن الْبَرَاء بْن عَازِبٍ رضي الله عنهما «أن النبي صلى الله عليه وسلم كان في سفر، فصلى العشاء الآخِرَةَ، فقرأ في إحدى الركعتين بِالتِّينِ وَالزَّيْتُون فما سمعت أحدًا أحسن صوتًا أو قراءة منه».
Kutoka kwa Barraa bin A'zib -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao- "Yakwamba Nabii -Rehema na Amani ziwe juu yake- alikuwa safarini, akaswali swala ya ishaa ya mwisho, akasoma katika moja ya rakaa mbili kwa sura ya wattin wazzaitun, sijawahi kumsikia yeyote mwenye sauti nzuri au kisomo kizuri zaidi yake".
Wamekubaliana Bukhaariy na MuslimDarajaSahihi
Maelezo

Alisoma Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- kwa sura ya wattin wazzaitun ndani ya rakaa ya kwanza katika swala ya ishaa; kwasababu yeye alikuwa safarini, na safari ni lazima izingatiwe kufanya wepesi (tahfifu) kwasababu ya shida na matatizo yake, na pamoja nakuwa Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- alikuwa msafiri, lakini hakuyaacha yale yanayochochea kupatikana kwa utulivu na kuhudhurisha moyo wakati wa kusikiliza Qur'ani, nako ni kupendezesha sauti katika kisomo cha swala.

Marejeo

تيسير العلام شرح عمدة الأحكام، عبد الله بن عبد الرحمن البسام، تحقيق: محمد صبحي حلاق، مكتبة الصحابة، الإمارات، مكتبة التابعين، القاهرة، الطبعة: العاشرة 1426هـ. تنبيه الأفهام شرح عمدة الأحكام، محمد بن صالح العثيمين، مكتبة الصحابة، الإمارات، الطبعة: الأولى، 1426هـ. الإلمام بشرح عمدة الأحكام، إسماعيل بن محمد الأنصاري، دار الفكر، دمشق، الطبعة: الأولى، 1381هـ. صحيح البخاري، محمد بن إسماعيل البخاري الجعفي، تحقيق: محمد زهير الناصر، دار طوق النجاة (مصورة عن السلطانية بإضافة ترقيم: محمد فؤاد عبد الباقي)، الطبعة: الأولى، 1422هـ. صحيح مسلم، مسلم بن الحجاج القشيري النيسابوري، تحقيق محمد فؤاد عبد الباقي، دار إحياء التراث العربي، بيروت، 1423هـ.

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Yakwamba Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- alikuwa anapo swali anatanua kati ya mikono yake mpaka unaonekana weupe wa kwapa zake

عَنْ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ مَالِكٍ ابْنِ بُحَيْنَةَ رضي الله عنه: أَنَّ النَّبِيَّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ كَانَ إِذَا صَلَّى فَرَّجَ بَيْنَ يَدَيْهِ حَتَّى يَبْدُوَ بَيَاضُ إِبْطَيْهِ.
Kutoka kwa Abdallah bin Maliki bin Buhaina radhi za Allah ziwe juu yake: Yakwamba Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- alikuwa anapo swali anatanua kati ya mikono yake mpaka unaonekana weupe wa kwapa zake.
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeDarajaSahihi
Maelezo

Alikuwa rehema na amani zimshukie anaposwali, anaikunjua mikono yake wakati wa kusujudu. Alisogeza kila mkono kutoka upande wa karibu yake, kama mbawa mbili, mpaka rangi ya ngozi ya makwapa yake inaonekana; Hii ni katika kupitiliza kuitanua mikono na kuitenganisha na mbavu zake.

Mafunzo
  1. Mkao huu unapendeza katika sijida, nao ni kuweka mbali vikwapa na mbavu.
  2. Maamuma ambaye jirani yake anakereka kwa kutanua kwake mikono; si sheria kwake kufanya hivyo.
  3. Katika kutanua mikono katika sijida, kuna hekima na faida nyingi, miongoni mwake ni: kuonyesha uchangamfu na hamu ya kusali, na kwamba ikiwa mtu ataegemea viungo vyote katika sijida, kila kiungo kitapata sehemu yake ya ibada. Ikasemwa kuwa: Hekima katika hili ni kuwa ni sawa na unyenyekevu, na inafaa zaidi katika kuweka paji la uso na pua karibu na ardhi, na pia ili kila kiungo kiweze kutofautishwa peke yake.
Marejeo

صحيح البخاري (1/ 87) (390). صحيح مسلم (1/ 356) (495). تيسير العلام شرح عمدة الأحكام، للبسام (ص162). تنبيه الأفهام شرح عمدة الأحكام، لابن عثيمين (2/ 207). الإلمام بشرح عمدة الأحكام، لإسماعيل الأنصاري (1/ 134).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Alikuwa Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- akiitembelea msikiti wa Qubaa kwa kipando na pia kwa miguu, anaswali ndani yake rakaa mbili

عن عبد الله بن عمر رضي الله عنهما قال: كان النبي صلى الله عليه وسلم يزورُ قُبَاءَ راكبًا وماشيًا، فيُصَلِّي فيه ركعتين. وفي رواية: كان النبي صلى الله عليه وسلم يأتي مسجد قُبَاءَ كل سَبْتٍ راكبًا وماشيًا، وكان ابن عُمر يفعله.
Kutoka kwa Abdallah bin Omar -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao- Amesema: Alikuwa Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- akiitembelea msikiti wa Qubaa kwa kipando na kwa miguu, anaswali ndani yake rakaa mbili. Na katika riwaya nyingine: Alikuwa Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- akienda msikiti wa Qubaa kila juma mosi akiwa katika kipando na kwa miguu, na alikuwa bin Omar akifanya hivyo.
Imepokelewa na Al-Bukhaariy na Muslim kwa riwaya zakeDarajaSahihi
Maelezo

Eneo la Qubaa ambapo umejengwa hapo msikiti wa kwanza katika uislamu ni kijiji kilichopo karibu na kituo cha Madina tokea pande za kusini mashariki ya mji wa Madina,akawa Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- anautembelea msikiti wa Qubaa akiwa katika kipando na akiwa kwa miguu, na aliposema kila juma mosi: makusudio nikuwa alikuwa akitenga baadhi ya siku kwaajili ya ziara, na hekima ya Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake kuja Qubaa siku ya juma mosi katika kila wiki, ilikuwa ni ajili ya kuunga udugu na maanswari na kujua hali zao na hali ya yule aliyechelewa kuipata swala ya ijumaa pamoja naye,na hii ndio siri ya kuichagua ziara katika sikuya juma mosi.

Marejeo

رياض الصالحين للنووي، ط1، تحقيق: ماهر ياسين الفحل، دار ابن كثير، دمشق، بيروت، 1428هـ. رياض الصالحين، ط4، تحقيق: عصام هادي، وزارة الأوقاف والشؤون الإسلامية القطرية، دار الريان، بيروت، 1428هـ. شرح رياض الصالحين، للشيخ ابن عثيمين، دار الوطن للنشر، الرياض، 1426هـ. فتح الباري شرح صحيح البخاري، للحافظ ابن حجر العسقلاني، قام بإخراجه وصححه وأشرف على طبعه: محب الدين الخطيب، رقم كتبه وأبوابه وأحاديثه: محمد فؤاد عبد الباقي، عليه تعليقات العلامة: عبد العزيز بن عبد الله بن باز، دار المعرفة، بيروت، 1379هـ. المنهاج شرح صحيح مسلم بن الحجاج، للنووي، ط2، دار إحياء التراث العربي - بيروت، 1392هـ. صحيح البخاري، تحقيق: محمد زهير بن ناصر الناصر، ط1، دار طوق النجاة (مصورة عن السلطانية بإضافة ترقيم: محمد فؤاد عبد الباقي)، 1422هـ. صحيح مسلم، تحقيق: محمد فؤاد عبد الباقي، دار إحياء التراث العربي، بيروت. نزهة المتقين شرح رياض الصالحين، لمجموعة من الباحثين، ط14، مؤسسة الرسالة، 1407هـ.

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Kila hadithi, daraja, maelezo na funzo hapa vinaonyeshwa kama HadeethEnc.com inavyovichapisha, kwa masharti yake ya kuchapisha upya. Daraja halimtaji aliyelitoa. Tafsiri na maelezo ni ya waandishi wake wenyewe, na baadhi hutaja hukumu; wahakiki wa Sabīl hawajavichunguza. Hadithi ya Kiarabu ndiyo matini. Chanzo: HadeethEnc.com