Ruka hadi kwenye maudhui
Hadithi zenye maelezo

Nilihifadhi kutoka kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- rakaa kumi

عَنِ ابْنِ عُمَرَ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُمَا قَالَ: حَفِظْتُ مِنَ النَّبِيِّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ عَشْرَ رَكَعَاتٍ: رَكْعَتَيْنِ قَبْلَ الظُّهْرِ، وَرَكْعَتَيْنِ بَعْدَهَا، وَرَكْعَتَيْنِ بَعْدَ المَغْرِبِ فِي بَيْتِهِ، وَرَكْعَتَيْنِ بَعْدَ العِشَاءِ فِي بَيْتِهِ، وَرَكْعَتَيْنِ قَبْلَ صَلاَةِ الصُّبْحِ، وَكَانَتْ سَاعَةً لاَ يُدْخَلُ عَلَى النَّبِيِّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ فِيهَا، حَدَّثَتْنِي حَفْصَةُ أَنَّهُ كَانَ إِذَا أَذَّنَ المُؤَذِّنُ وَطَلَعَ الفَجْرُ صَلَّى رَكْعَتَيْنِ، وَفِي لَفْظٍ: أَنَّ النَّبِيَّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ كَانَ يُصَلِّي بَعْدَ الْجُمُعَةِ رَكْعَتَيْنِ.
Imeokewa Kutoka kwa bin Omari Radhi za Allah ziwe juu yake yeye na baba yake, amesema : Nilihifadhi kutoka kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- rakaa kumi: Rakaa mbili kabla ya Dhuhuri, na rakaa mbili baada yake, na rakaa mbili baada ya Magharibi nyumbani kwake, na rakaa mbili baada ya Ishaa nyumbani kwake, na rakaa mbili kabla ya swala ya Alfajiri, na muda huo ulikuwa ni wakati ambao haruhusiwi yeyote kuingia kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-, Hafswa ndiye aliyenisimulia kuwa alikuwa anapoadhini muadhini na ikachomoza Alfajiri anaswali rakaa mbili, na katika riwaya nyingine: Nikuwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- alikuwa akiswali baada ya Ijumaa rakaa mbili.
Imepokelewa na Al-Bukhaariy na Muslim katika riwaya zake zoteDarajaSahihi
Maelezo

Anabainisha Abdullahi bin Omari Radhi za Allah ziwe juu yake yeye na baba yake: Yakuwa miongoni mwa swala za sunna alizozihifadhi kutoka kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- ni rakaa kumi na huitwa kuwa ni sunna zilizopangiliwa, Rakaa mbili kabla ya Dhuhuri, na rakaa mbili baada yake, na rakaa mbili baada ya Magharibi nyumbani kwake, na rakaa mbili baada ya Ishaa nyumbani kwake, Na kabla ya Alfajiri rakaa mbili, Zikatimia rakaa kumi. Na ama swala ya Ijumaa aliswali baada yake rakaa mbili.

Mafunzo
  1. Imendezeshwa kuswali rakaa hizi zilizopangiliwa, na kudumu nazo.
  2. Sheria ya kuswali sunna nyumbani.
Marejeo

صحيح البخاري (2/ 58-59) (1180، 1181). صحيح مسلم (2/ 601) (882). تيسير العلام شرح عمدة الأحكام، للبسام (ص112).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com
Swala ya Kujikurubisha kwa Mwenyezi Mungu.

Kila hadithi, daraja, maelezo na funzo hapa vinaonyeshwa kama HadeethEnc.com inavyovichapisha, kwa masharti yake ya kuchapisha upya. Daraja halimtaji aliyelitoa. Tafsiri na maelezo ni ya waandishi wake wenyewe, na baadhi hutaja hukumu; wahakiki wa Sabīl hawajavichunguza. Hadithi ya Kiarabu ndiyo matini. Chanzo: HadeethEnc.com