عَنِ ابْنِ عُمَرَ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُمَا قَالَ: حَفِظْتُ مِنَ النَّبِيِّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ عَشْرَ رَكَعَاتٍ: رَكْعَتَيْنِ قَبْلَ الظُّهْرِ، وَرَكْعَتَيْنِ بَعْدَهَا، وَرَكْعَتَيْنِ بَعْدَ المَغْرِبِ فِي بَيْتِهِ، وَرَكْعَتَيْنِ بَعْدَ العِشَاءِ فِي بَيْتِهِ، وَرَكْعَتَيْنِ قَبْلَ صَلاَةِ الصُّبْحِ، وَكَانَتْ سَاعَةً لاَ يُدْخَلُ عَلَى النَّبِيِّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ فِيهَا، حَدَّثَتْنِي حَفْصَةُ أَنَّهُ كَانَ إِذَا أَذَّنَ المُؤَذِّنُ وَطَلَعَ الفَجْرُ صَلَّى رَكْعَتَيْنِ، وَفِي لَفْظٍ: أَنَّ النَّبِيَّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ كَانَ يُصَلِّي بَعْدَ الْجُمُعَةِ رَكْعَتَيْنِ.
Imeokewa Kutoka kwa bin Omari Radhi za Allah ziwe juu yake yeye na baba yake, amesema : Nilihifadhi kutoka kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- rakaa kumi: Rakaa mbili kabla ya Dhuhuri, na rakaa mbili baada yake, na rakaa mbili baada ya Magharibi nyumbani kwake, na rakaa mbili baada ya Ishaa nyumbani kwake, na rakaa mbili kabla ya swala ya Alfajiri, na muda huo ulikuwa ni wakati ambao haruhusiwi yeyote kuingia kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-, Hafswa ndiye aliyenisimulia kuwa alikuwa anapoadhini muadhini na ikachomoza Alfajiri anaswali rakaa mbili, na katika riwaya nyingine: Nikuwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- alikuwa akiswali baada ya Ijumaa rakaa mbili.
Imepokelewa na Al-Bukhaariy na Muslim katika riwaya zake zoteDarajaSahihi
Maelezo
Anabainisha Abdullahi bin Omari Radhi za Allah ziwe juu yake yeye na baba yake: Yakuwa miongoni mwa swala za sunna alizozihifadhi kutoka kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- ni rakaa kumi na huitwa kuwa ni sunna zilizopangiliwa, Rakaa mbili kabla ya Dhuhuri, na rakaa mbili baada yake, na rakaa mbili baada ya Magharibi nyumbani kwake, na rakaa mbili baada ya Ishaa nyumbani kwake, Na kabla ya Alfajiri rakaa mbili, Zikatimia rakaa kumi. Na ama swala ya Ijumaa aliswali baada yake rakaa mbili.
Mafunzo
- Imendezeshwa kuswali rakaa hizi zilizopangiliwa, na kudumu nazo.
- Sheria ya kuswali sunna nyumbani.
Marejeo
صحيح البخاري (2/ 58-59) (1180، 1181).
صحيح مسلم (2/ 601) (882).
تيسير العلام شرح عمدة الأحكام، للبسام (ص112).
Hadithi hii kwenye HadeethEnc.comعَنْ أَبِي قَتَادَةَ السَّلَمِيِّ رضي الله عنه أَنَّ رَسُولَ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: «إِذَا دَخَلَ أَحَدُكُمُ الْمَسْجِدَ فَلْيَرْكَعْ رَكْعَتَيْنِ قَبْلَ أَنْ يَجْلِسَ».
Kutoka kwa Abuu Qatada As-sulami Radhi za Allah ziwe juu yake- hakika Mtume Rehema na amani za Allah ziwe juu yake alisema: "Atakapoingia mmoja wenu msikitini basi asali rakaa mbili kabla hajakaa".
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeDarajaSahihi
Maelezo
Amemhimiza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- mwenye kuja msikitini na akaingia katika wakati wowote, na kwa lengo lolote, asali rakaa mbili kabla hajakaa, nazo ni rakaa mbili za salamu ya msikiti.
Mafunzo
- Sunna ya swala ya rakaa mbili kwa ajili ya salamu ya msikiti kabla ya kukaa.
- Amri hii ni kwa atakayetaka kukaa, atakayeingia msikitini na akatoka kabla ya kukaa, amri hii haimuhusu.
- Atakapoingia mwenye kuswali na watu wakiwa ndani ya swala, akaingia nao, basi hilo litamtosheleza na rakaa mbili.
Marejeo
صحيح البخاري (1/ 96) (444)، صحيح مسلم (1/ 495) (714)، المفهم لما أشكل من تلخيص كتاب مسلم (2/ 352)، فتح الباري لابن رجب (3/ 274)، التوضيح (5/524)، البحر المحيط الثجاج في شرح صحيح الإمام مسلم بن الحجاج (15/ 287).
Hadithi hii kwenye HadeethEnc.comعَنْ عَبْدِ اللهِ بْنِ مُغَفَّلٍ رضي الله عنه قَالَ: قَالَ النَّبِيُّ صلى الله عليه وسلم: «بَيْنَ كُلِّ أَذَانَيْنِ صَلَاةٌ، بَيْنَ كُلِّ أَذَانَيْنِ صَلَاةٌ» ثُمَّ قَالَ فِي الثَّالِثَةِ: «لِمَنْ شَاءَ».
Imepokelewa kutoka kwa Abdallahi bin Amru -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake-amesema: Amesema Mtume -rehema na amani ziwe juu yake-: "Kati ya kila adhana mbili kuna swala, kati ya kila adhana mbili kuna swala" Kisha akasema katika mara ya tatu: "Kwa atakayetaka"
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeDarajaSahihi
Maelezo
Amebainisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa baina ya kila adhana na ikama kuna swala ya sunna, na akalirudia hilo mara tatu, na akaeleza katika mara ya tatu kuwa hilo ni sunna na inapendeza kwa atakayetaka kuswali.
Mafunzo
- Inapendeza kuswali baina ya adhana na ikama.
- Muongozo wa Mtume rehema na amani ziwe juu yake katika kuirudiarudia kauli, na hii ni kwakutaka isikike vizuri na kutia mkazo kwa umuhimu wa yale anayoyasema.
- Makusudio ya dhana mbili: Ni adhana na ikama, na zimeitwa zote kuwa ni adhana kama kuichanganya ikama ndani ya adhana, kama kusema miezi miwili (Jua na Mwezi) na akina Omari wawili, yaani: (Abubakari na Omari).
- Adhana ni tangazo la kuingia kwa wakati, na ikama ni tangazo la kuwadia muda wa kuswali.
Marejeo
صحيح البخاري (1/ 128) (627)، صحيح مسلم (1/ 573) (838)، البحر المحيط الثجاج في شرح صحيح الإمام مسلم بن الحجاج (16/ 671)، النهاية في غريب الحديث والأثر (31).
Hadithi hii kwenye HadeethEnc.comعَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ أَنَّ النَّبِيَّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ لِبِلاَلٍ عِنْدَ صَلاَةِ الفَجْرِ: «يَا بِلاَلُ، حَدِّثْنِي بِأَرْجَى عَمَلٍ عَمِلْتَهُ فِي الإِسْلاَمِ، فَإِنِّي سَمِعْتُ دَفَّ نَعْلَيْكَ بَيْنَ يَدَيَّ فِي الجَنَّةِ» قَالَ: مَا عَمِلْتُ عَمَلًا أَرْجَى عِنْدِي أَنِّي لَمْ أَتَطَهَّرْ طَهُورًا، فِي سَاعَةِ لَيْلٍ أَوْ نَهَارٍ، إِلَّا صَلَّيْتُ بِذَلِكَ الطُّهُورِ مَا كُتِبَ لِي أَنْ أُصَلِّيَ.
kutoka kwa Abuu Huraira radhi za Allah ziwe juu yake- hakika Mtume rehema na amani za Allah ziwe juu yake alisema kumwambia Bilali wakati wa swala ya Alfajiri: "Ewe Bilali, hebu nihadithie kuhusu amali yenye matarajio makubwa zaidi uliyowahi kuifanya ndani ya Uislamu, kwani mimi nilisikia mkanyago wa viavu vyako mbele yangu huko Peponi" Akasema: Sijawahi kufanya amali yoyote yenye matarajio kwangu isipokuwa sijawahi kutia udhu wowote, katika nyakati za usiku au mchana, isipokuwa ninaswali kwa udhu huo kiasi nilichoandikiwa niswali katika rakaa.
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeDarajaSahihi
Maelezo
Aliona Mtume rehema na amani ziwe juu yake usingizini kuwa yuko Peponi, akasema kumwambia Bilal bin Rabaha: Nieleze kuhusu amali yoyote ya sunna yenye matarajio makubwa uliowahi kuifanya ndani ya Uislamu? kwani mimi nilisikia sauti ya chini ya viatu vyako wakati wa kuvitikisa kwa kutembea mbele yangu Peponi. Bilal akasema: Sikuwahi kufanya amali yoyote yenye matarajio makubwa yoyote kwangu zaidi yakuwa sijawahi kutengukwa udhu wakati wowote iwe usiku au mchana isipokuwa ninatawadha, kisha ninaswali kwa ajili ya Mola wangu kwa udhu huo swala za sunna zisizo na mpaka kiasi nilichoandikiwa kuswali.
Mafunzo
- Ubora wa amali aliyoisema Bilal radhi za Allah ziwe juu yake, nayo ni swala kila anapopata twahara na akatia udhu, na kwamba hiyo ni miongoni mwa amali inayotarajiwa zaidi, na ni sababu ya kuingia Peponi.
- Sunna ya kuswali baada ya kila udhu.
- Kiigizo na mlezi kuuliza matendo ya mwanafunzi wake; ili amhimize kudumu nayo kama ni matendo mazuri, na kama si hivyo basi amkataze.
- Ushahidi kutoka kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake kwa Bilal radhi za Allah ziwe juu yake kuwa yeye ni katika watu wa peponi.
- Swali hili lilikuwa wakati wa swala ya Alfajiri, na kwa hili ni ishara kuwa tukio hili lilitokea katika ndoto yake rehema na amani ziwe juu yake, na ndoto za Manabii ni kweli.
Marejeo
صحيح البخاري (2/ 53) (1149).
صحيح مسلم (4/ 1910) (2458).
عمدة القاري شرح صحيح البخاري (7/ 206).
إرشاد الساري لشرح صحيح البخاري (2/ 326).
Hadithi hii kwenye HadeethEnc.comKila hadithi, daraja, maelezo na funzo hapa vinaonyeshwa kama HadeethEnc.com inavyovichapisha, kwa masharti yake ya kuchapisha upya. Daraja halimtaji aliyelitoa. Tafsiri na maelezo ni ya waandishi wake wenyewe, na baadhi hutaja hukumu; wahakiki wa Sabīl hawajavichunguza. Hadithi ya Kiarabu ndiyo matini. Chanzo: HadeethEnc.com