عن عائشةَ أمِّ المؤْمنِين رضي الله عنها قالت: لَمْ يَكُنِ النَّبِيُّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ عَلَى شَيْءٍ مِنَ النَّوَافِلِ أَشَدَّ مِنْهُ تَعَاهُدًا عَلَى رَكْعَتَيِ الفَجْرِ.
Imepokelewa kutoka kwa Aisha mama wa waumini radhi za Allah ziwe juu yake, amesema: Hakuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa na mkazo mkubwa na kudumu na jambo kama alivyokuwa katika rakaa mbili za Alfajiri.
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeDarajaSahihi
Maelezo
Ameeleza mama wa waumini Aisha radhi za Allah ziwe juu yake ya kwamba Mtume rehema na amani ziwe juu yake hakuwa na mkazo mkubwa katika swala za sunna zaidi ya jinsi alivyozikazia na kuzipupia na kuzihifadhi rakaa mbili za sunna ya kabla ya Alfajiri.
Mafunzo
- Sunna za swala ni zile zisizokuwa faradhi katika ibada, na makusudio yake hapa: Ni sunna zilizopangilia zinazofuatana na faradhi.
- Sunna zilizopangiliwa: Rakaa mbili kabla ya Alfajiri, na rakaa nne kabla ya Adhuhuri, na mbili baada yake, na rakaa mbili baada ya Magharibi, na rakaa mbili baada ya Ishaa.
- Sunna ya Alfajiri huswaliwa nyumbani na safarini, tofauti na sunna za Adhuhuri na Magharibi na Ishaa, hizo haziswaliwi isipokuwa nyumbani.
- Sunna hii imetikiliwa mkazo ya rakaa mbili za Alfajiri, haitakiwi kuzipuuza.
Marejeo
صحيح البخاري (2/ 57) (1169).
صحيح مسلم (1/ 501) (724).
تيسير العلام شرح عمدة الأحكام، لعبد الله البسام (ص113).
تنبيه الأفهام شرح عمدة الأحكام، لابن عثيمين (1/ 144).
Hadithi hii kwenye HadeethEnc.comعن عائشةَ أُمِّ المُؤْمِنينَ رضي الله عنها: أن النبي صلى الله عليه وسلم كان لا يَدع أربعا قَبل الظهر وركعتين قبل الغَدَاة.
Imenukuliwa kutoka kwa Aisha mama wa waumini radhi za Allah ziwe juu yake: Yakwamba Mtume -rehema na amani ziwe juu yake alikuwa haziachi rakaa nne kabla ya Adhuhuri na rakaa mbili kabla ya Alfajiri.
Imepokelewa na Al-BukhaariyDarajaSahihi
Maelezo
Ameeleza Aisha radhi za Allah ziwe juu yake yakuwa Mtume -rehema na amani ziwe juu yake alikuwa akidumu na swala za sunna ndani ya nyumba yake na wala haziachi: Rakaa nne kwa salamu mbili kabla ya swala ya Adhuhuri, na rakaa mbili kabla ya swala ya Alfajiri.
Mafunzo
- Sunna ya kuzihifadhi na kudumu na rakaa nne kabla ya swala ya Adhuhuri, na rakaa mbili kabla ya swala ya Alfajiri.
- Kilicho bora ni swala za sunna ziswaliwe nyumbani, na ndivyo alivyoeleza Aisha radhi za Allah ziwe juu yake.
Marejeo
صحيح البخاري (2/ 59) (1182).
توضيح الأحكام مِن بلوغ المرام، لعبد الله البسام (2/ 379).
Hadithi hii kwenye HadeethEnc.comعَنْ أُمِّ حَبِيبَةَ رضي الله عنها زَوْجِ النَّبِيِّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالت: سَمِعْتُ رَسُولَ اللهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ يَقُولُ: «مَنْ حَافَظَ عَلَى أَرْبَعِ رَكَعَاتٍ قَبْلَ الظُّهْرِ وَأَرْبَعٍ بَعْدَهَا حَرَّمَهُ اللَّهُ عَلَى النَّارِ».
Kutoka kwa Ummu Habiba, radhi za Allah ziwe juu yake, mke wa Mtume -rehema na amani ziwe juu yake, amesema: Nilimsikia Mtume -rehema na amani ziwe juu yake akisema: "Atakayehifadhi rakaa nne kabla ya Adhuhuri na rakaa nne baada yake basi Mwenyezi Mungu atamharamisha kuingia motoni".
Imepokelewa na Abu Daud, Tirmidhiy, Nasai, Ibn Majah na AhmadDarajaSahihi
Maelezo
Amempa habari njema Mtume -rehema na amani ziwe juu yake atakayeswali katika swala za sunna rakaa nne kabla ya swala ya Adhuhuri, na rakaa nne baada yake, na akadumu na akazihifadhi, kuwa Mwenyezi Mungu atamharamisha kuingia motoni.
Mafunzo
- Ni sunna kuhifadhi rakaa nne kabla ya Adhuhuri, na nne baada yake.
- Sunna zilizopangwa za kabla ya swala - Yaani kabla ya swala za faradhi-; zina hekima kubwa, miongoni mwake: Ni kumuandaa mwenye kuswali kwa ajili ya ibada kabla ya kuingia katika swala ya faradhi, na ama za baada ya swala miongoni mwa hekima zake ni kuziba mapungufu ya swala za faradhi.
- Sunna zilizopangiliwa zina faida kubwa, ikiwemo kuzidisha mema, na kufuta madhambi, na kunyanyua daraja.
- Kanuni ya Ahlussunna (wanaofuata mafundisho ya Mtume) katika hadithi za ahadi mfano wa hadithi hii: Ni kuchukuliwa kuwa, mpaka mtu afe katika hali ya kumpwekesha Mwenyezi Mungu, nakuwa makusudio yake ni kutokaa milele motoni, kwa sababu mfanya madhambi ni katika watu wa tauhidi, anastahiki adhabu lakini hatowekwa motoni milele endapo ataadhibiwa.
Marejeo
سنن أبي داود (2/ 448) (1269).
سنن الترمذي (1/ 452) (428).
سنن النسائي (3/ 265) (1816).
سنن ابن ماجه (2/ 238) (1160).
مسند أحمد (44/ 358) (26772).
سبل السلام شرح بلوغ المرام، لمحمد الصنعاني (1/ 336).
توضيح الأحكام مِن بلوغ المرام، لعبد الله البسام (2/ 381).
Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com