Ruka hadi kwenye maudhui
Hadithi zenye maelezo

Yakwamba Mtume -rehema na amani ziwe juu yake alikuwa haziachi rakaa nne kabla ya Adhuhuri na rakaa mbili kabla ya Alfajiri

عن عائشةَ أُمِّ المُؤْمِنينَ رضي الله عنها: أن النبي صلى الله عليه وسلم كان لا يَدع أربعا قَبل الظهر وركعتين قبل الغَدَاة.
Imenukuliwa kutoka kwa Aisha mama wa waumini radhi za Allah ziwe juu yake: Yakwamba Mtume -rehema na amani ziwe juu yake alikuwa haziachi rakaa nne kabla ya Adhuhuri na rakaa mbili kabla ya Alfajiri.
Imepokelewa na Al-BukhaariyDarajaSahihi
Maelezo

Ameeleza Aisha radhi za Allah ziwe juu yake yakuwa Mtume -rehema na amani ziwe juu yake alikuwa akidumu na swala za sunna ndani ya nyumba yake na wala haziachi: Rakaa nne kwa salamu mbili kabla ya swala ya Adhuhuri, na rakaa mbili kabla ya swala ya Alfajiri.

Mafunzo
  1. Sunna ya kuzihifadhi na kudumu na rakaa nne kabla ya swala ya Adhuhuri, na rakaa mbili kabla ya swala ya Alfajiri.
  2. Kilicho bora ni swala za sunna ziswaliwe nyumbani, na ndivyo alivyoeleza Aisha radhi za Allah ziwe juu yake.
Marejeo

صحيح البخاري (2/ 59) (1182). توضيح الأحكام مِن بلوغ المرام، لعبد الله البسام (2/ 379).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com
Sunna za kila siku zilizopangiliwa

Kila hadithi, daraja, maelezo na funzo hapa vinaonyeshwa kama HadeethEnc.com inavyovichapisha, kwa masharti yake ya kuchapisha upya. Daraja halimtaji aliyelitoa. Tafsiri na maelezo ni ya waandishi wake wenyewe, na baadhi hutaja hukumu; wahakiki wa Sabīl hawajavichunguza. Hadithi ya Kiarabu ndiyo matini. Chanzo: HadeethEnc.com