عن عائشة رضي الله عنها : أن النبي صلى الله عليه وسلم كان يصلي صلاته بالليل، وهي مُعْتَرِضَةٌ بين يديه، فإذا بقي الوتر، أيقظها فأوترت. وفي رواية له: فإذا بقي الوتر، قال: «قومي فأوْتِري يا عائشة».
Kutoka kwa Aisha -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- Yakwamba Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- alikuwa akiswali swala zake za usiku, naye akiwa kajilaza mbele yake, inapobakia witiri, anamuamsha na anaswali witiri. Na katika riwaya yake: inapobakia witiri, anasema: "Simama na uswali witiri ewe Aisha".
Wamekubaliana Bukhaariy na MuslimDarajaSahihi
Maelezo
Maana ya hadithi: Nikuwa Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- alikuwa akiswali swala za usiku, na Aisha -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- akiwa kajilaza mbele yake, na katika riwaya ya Bukhariy na Muslim kutoka kwake: "Nikuwa Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- alikuwa akiswali usiku na mimi nikiwa nimejilaza kati yake na kibla, kama linavyolazwa jeneza". Anapomaliza Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- swala ya usiku (tahajjudi), na kabla hajaanza swala ya witiri anamuamsha kwaajili ya witiri, na katika riwaya ya Muslim: Inapobakia witiri, anasema: "Simama na uswali witiri ewe Aisha". Na katika riwaya ya Abiidaudi: "Mpaka anapotaka kuswali witiri basi anamuamsha na anaswali witiri". Na maana yake: Nikuwa Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- alikuwa akimuacha Aisha -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- mwanzo wa usiku wala hamuamshi, mpaka anapomaliza swala zake na ikawa haijabakia isipokuwa witiri anamuamsha ili naye apate witiri yake, na afanye haraka kuswali witiri baada ya kuamka ili uvivu wa usingizi usimzidie, lau kama akimzembea ikampita.
Marejeo
كنوز رياض الصالحين، تأليف: حمد بن ناصر بن العمار، الناشر: دار كنوز أشبيليا، الطبعة الأولى: 1430 هـ
بهجة الناظرين، تأليف: سليم بن عيد الهلالي، الناشر: دار ابن الجوزي ، سنة النشر: 1418 هـ- 1997م
المنهاج شرح صحيح مسلم، تأليف: محيي الدين يحيى بن شرف النووي، الناشر: دار إحياء التراث العربي، الطبعة: الثانية 1392 هـ
صحيح مسلم، تأليف: مسلم بن الحجاج النيسابوري، تحقيق: محمد فؤاد عبد الباقي الناشر: دار إحياء التراث العربي – بيروت
رياض الصالحين، تأليف : محيي الدين يحيى بن شرف النووي ، تحقيق: د. ماهر بن ياسين الفحل ، الطبعة: الأولى، 1428 هـ
دليل الفالحين، تأليف: محمد بن علان، الناشر: دار الكتاب العربي، نسخة الكترونية ، لا يوجد بها بيانات نشر
شرح رياض الصالحين، تأليف: محمد بن صالح العثيمين، الناشر: دار الوطن للنشر، الطبعة: 1426 هـ
المنهاج شرح صحيح مسلم، تأليف: محيي الدين يحيى بن شرف النووي، الناشر: دار إحياء التراث العربي، الطبعة: الثانية 1392 هـ
صحيح البخاري-المحقق : محمد زهير بن ناصر الناصر-الناشر : دار طوق النجاة-الطبعة : الأولى 1422هـ
الموسوعة الفقهية الكويتية-صادر عن: وزارة الأوقاف والشئون الإسلامية - الكويت-عدد الأجزاء: 45 جزءا-الطبعة: من 1404 - 1427 هـ.
Hadithi hii kwenye HadeethEnc.comعن عائشة رضي الله عنها ، قالت: كُنَّا نُعِدُّ لرسول الله صلى الله عليه وسلم سِوَاكَهُ وَطَهُورَهُ، فَيَبْعَثُهُ الله ما شاء أن يَبْعَثَهُ من الليل، فَيَتَسَوَّكُ، ويتوضَّأ ويُصلي.
Kutoka kwa Aisha -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- Amesema: Tulikuwa tukimuandalia Mjumbe wa Mwenyezi Mungu -Rehema na Amani ziwe juu yake- mswaki wake na (maji yake kwaajili ya) twahara, basi Mwenyezi Mungu anamuamsha kwa muda anaotaka aamke nyakati za usiku, anapiga mswaki, na anatawadha na anaswali
Imepokelewa na Imamu MuslimDarajaSahihi
Maelezo
Anaeleza Aisha -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- kuwa yeye alikuwa akimuandalia Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- mswaki wake, na maji ambayo atayatumia kutawadha usiku, kisha anamuamsha Mwenyezi Mungu Aliyetakasika na kutukuka nyakati za usiku, wakati wowote usiku, anapoamka tu anaanza kusugua meno yake kwa mswaki; ili aondoe harufu ya mdomo ambayo hutokea mara nyingi kwasababu ya kulala, kisha anatawadha udhu wake wa swala, kisha anaswali swala za usiku.
Marejeo
بهجة الناظرين شرح رياض الصالحين، سليم بن عيد الهلالي، دار ابن الجوزي، الدمام، الطبعة: الأولى 1415هـ.
رياض الصالحين من كلام سيد المرسلين، أبو زكريا محيي الدين النووي، تحقيق ماهر الفحل، دار ابن كثير، دمشق، بيروت، الطبعة: الأولى 1428هـ.
صحيح مسلم، مسلم بن الحجاج القشيري النيسابوري، تحقيق محمد فؤاد عبد الباقي، دار إحياء التراث العربي، بيروت، الطبعة: 1423 هـ.
نزهة المتقين شرح رياض الصالحين، مجموعة من الباحثين، مؤسسة الرسالة، بيروت، الطبعة: الرابعة عشر 1407هـ.
Hadithi hii kwenye HadeethEnc.comعن أبي هريرة رضي الله عنه قال: قال رسول الله صلى الله عليه وسلم: «مَنْ يَقُمْ لَيْلَةَ الْقَدْرِ إِيمَانًا وَاحْتِسَابًا غُفِرَ لَهُ مَا تَقَدَّمَ مِنْ ذَنْبِهِ»
Imepokewa Kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: "Mwenye kusimama usiku wenye cheo (Lailatul Qadri) kwa imani na kutaraji malipo, husamehewa madhambi yake yaliyotangulia."
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeDarajaSahihi
Maelezo
Anaeleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuhusu fadhila za kusimama usiku wa cheo unaokuwa katika siku kumi za mwisho wa Ramadhani, nakuwa yeyote mwenye kujitahidi ndani yake kwa ibada ya swala na dua na kusoma Qur'ani na kumtaja Allah, akiwa na imani na hayo, na kwa fadhila zilizoelezwa kwayo, akitaraji kwa amali yake malipo ya Allah Mtukufu, si kwa kutaka kuonekana na kusikika, basi husamehewa yaliyotangulia katika madhambi yake.
Mafunzo
- Fadhila za usiku wa cheo, na himizo la kusimama ndani yake.
- Matendo mema hayakubaliki isipokuwa kwa nia ya dhati na ya kweli.
- Fadhila za Allah na huruma yake, kwani mwenye kusimama usiku wa cheo kwa imani na kwa kutaraji malipo husamehewa madhambi yake yaliyotangulia.
Marejeo
صحيح البخاري (1/ 16) (35).
صحيح مسلم (1/ 523) (760).
كنوز رياض الصالحين، لمجموعة من الباحثين (14/ 435).
بهجة الناظرين، لسليم الهلالي (2/ 337).
نزهة المتقين، (2/ 846).
شرح النووي على مسلم (6/ 40).
شرح رياض الصالحين، لابن عثيمين (5/ 220).
شرح صحيح البخاري، لابن بطال (4/ 21).
Hadithi hii kwenye HadeethEnc.comعَنْ عَبْدُ اللَّهِ بْنُ سَلَامٍ رضي الله عنه قَالَ: لَمَّا قَدِمَ النَّبِيُّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ الْمَدِينَةَ انْجَفَلَ النَّاسُ قِبَلَهُ، وَقِيلَ: قَدِمَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، قَدِمَ رَسُولُ اللَّهِ، قَدِمَ رَسُولُ اللَّهِ، ثَلَاثًا، فَجِئْتُ فِي النَّاسِ لِأَنْظُرَ، فَلَمَّا تَبَيَّنْتُ وَجْهَهُ، عَرَفْتُ أَنَّ وَجْهَهُ لَيْسَ بِوَجْهِ كَذَّابٍ، فَكَانَ أَوَّلُ شَيْءٍ سَمِعْتُهُ تَكَلَّمَ بِهِ أَنْ قَالَ: «يَا أَيُّهَا النَّاسُ، أَفْشُوا السَّلَامَ، وَأَطْعِمُوا الطَّعَامَ، وَصِلُوا الْأَرْحَامَ، وَصَلُّوا بِاللَّيْلِ وَالنَّاسُ نِيَامٌ، تَدْخُلُوا الْجَنَّةَ بِسَلَامٍ».
Kutoka kwa Abdullah bin Salam radhi za Allah ziwe juu yake amesema: Alipokuja Madina Mtume rehema na amani ziwe juu yake, watu walikusanyika mbele yake, pakasemwa: Amefika Mtume wa Mwenyezi Mungu rehema na amani ziwe juu yake, Amefika Mtume wa Mwenyezi Mungu, Amefika Mtume wa Mwenyezi Mungu, wakasema mara tatu, nikaja pamoja na watu kutazama, na nilipouona uso wake nikajua kuwa uso wake si uso wa muongo, kwa hivyo jambo la kwanza nililomsikia akizungumza alisema kuwa: "Enyi watu, toleaneni salamu na muunge udugu, na mlishe chakula, na msali usiku watu wakiwa wamelala, mtaingia peponi kwa amani".
Imepokelewa na Tirmidhiy, Ibn Majah na AhmadDarajaSahihi
Maelezo
Mtume rehema na amani ziwe juu yake alipokuja Madina na watu wakamuona, haraka sana walimfuata, na miongo mwa waliomfuata ni Abdallah bin Salam radhi za Allah ziwe juu yake na alikuwa ni katika Mayahudi wakati huo, alipomuona akajua kuwa uso wake haukuwa wa mtu muongo; Kwa sababu ya kile kinachoonekana kwake kama, nuru, na uzuri, na heshima na ukweli, ikawa jambo la kwanza alilolisikia kutoka kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake ni kuwataka watu wafanye matendo yatakayopelekea kuingia Peponi, ikiwemo:
La kwanza: kusambaza salamu ya amani, na kuionyesha na kuikithirisha kwa wale unaowajua na usiowajua.
La pili: Kulishiza chakula kwa sadaka na zawadi na kukaribisha ugeni.
La tatu: Kuunga udugu kwa wale kinachowaunganisha kizazi au ukaribu wa udugu upande wa baba au mama.
La nne: Swala za sunna, kisimamo cha usiku na watu wakiwa wamelala.
Mafunzo
- Ni sunna kueneza salamu ya amani baina ya Waislamu ama kwa asiye Muislamu haanzwi kwa salamu, na akimtolea salamu kwa kusema: Amani iwe juu yako, (Assalaam alaikum) amjibu kwa kusema: Na juu yako (Wa alaikum).
Marejeo
سنن ابن ماجه (4/ 397) (3251).
سنن الترمذي (4/ 264) (2485).
مسند أحمد (39/ 201) (23784).
توضيح الأحكام من بلوغ المرام، لعبد الله البسام (2/ 454).
منحة العلام في شرح بلوغ المرام، لعبد الله الفوزان (3/ 299).
فتح ذي الجلال والإكرام، لابن عثيمين (6/ 440).
سبل السلام بشرح بلوغ المرام، لمحمد الصنعاني (2/ 693).
Hadithi hii kwenye HadeethEnc.comعَنْ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ عُمَرَ رَضيَ اللهُ عنهما: سَأَلَ رَجُلٌ النَّبِيَّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ وَهُوَ عَلَى المِنْبَرِ، مَا تَرَى فِي صَلاَةِ اللَّيْلِ، قَالَ: «مَثْنَى مَثْنَى، فَإِذَا خَشِيَ الصُّبْحَ صَلَّى وَاحِدَةً، فَأَوْتَرَتْ لَهُ مَا صَلَّى» وَإِنَّهُ كَانَ يَقُولُ: «اجْعَلُوا آخِرَ صَلاَتِكُمْ وِتْرًا» فَإِنَّ النَّبِيَّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ أَمَرَ بِهِ.
Imepokelewa kutoka kwa Abdallah bin Omari -radhi za Allah ziwe juu yake yeye na baba yake-: Bwana mmoja alimuuliza Mtume Muhammad rehema na amani za Allah ziwe juu yake akiwa juu ya mimbari, waonaje kuhusu swala za usiku, akasema: "Ni rakaa mbili mbili, atapochelea Alfajiri aswali rakaa moja, iwe ni witri kwa aliyo swali" na yeye alikuwa akisema: "Fanyeni swala yenu ya mwisho iwe ni witri", kwa hakika Mtume rehema na amani za Allah zimshukie kaamrisha hivyo.
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeDarajaSahihi
Maelezo
Mtu mmoja alimuuliza Mtume rehema na amani ziwe juu yake naye akiwa anahutubia juu ya Mimbari: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu nifundishe ni namna gani nitaswali usiku?. Akasema rehema na amani ziwe juu yake: Utaswali na kutoa salamu katika kila rakaa mbili, ukihofia kuchomoza kwa Afajiri basi swali rakaa moja itakufanyia kuwa witiri rakaa zingine ulizoswali, na hakika yeye rehema na amani ziwe juu yake alikuwa akiusia kuifanya swala ya mwisho ya usiku kuwa ni witiri.
Mafunzo
- Asili katika swala za usiku ni mtu atoe salamu katika kila rakaa mbili, nje na witiri.
- Nikuwa swala za usiku hazina idadi maalumu; kwa kuwa tamko liliachwa wazi.
- Amesema Nawawi: "Swala za usiku na mchana ni rakaa mbili mbili", hadithi hii inachukuliwa kama kubainisha kilicho bora zaidi, nayo ni atoe salamu katika kila rakaa mbili, na sawa sawa ziwe ni sunna za usiku na mchana, na ni sunna atoe salamu kwa kila rakaa mbili.
- Amesema Nawawi: Hapa kuna ushahidi kuwa sunna ni kuifanya witiri kuwa swala ya mwisho wa usiku, na kwamba wakati wake unamalizika kwa kuchomoza Alfajiri, na ndio kauli mashuhuri katika madhehebu yetu, na ndivyo lilivyosema jopo la wanachuoni.
Marejeo
صحيح البخاري (1/ 102) (472).
صحيح مسلم (1/ 517) (751).
إرشاد الساري لشرح صحيح البخاري، لابن حجر(1/ 456).
توضيح الأحكام مِن بلوغ المرام، لعبد الله البسام (2/ 394).
فتح ذي الجلال والإكرام شرح بلوغ المرام، لابن عثيمين (2/ 233).
تيسير العلام شرح عمدة الأحكام، لعبد الله البسام (ص217).
Hadithi hii kwenye HadeethEnc.comKila hadithi, daraja, maelezo na funzo hapa vinaonyeshwa kama HadeethEnc.com inavyovichapisha, kwa masharti yake ya kuchapisha upya. Daraja halimtaji aliyelitoa. Tafsiri na maelezo ni ya waandishi wake wenyewe, na baadhi hutaja hukumu; wahakiki wa Sabīl hawajavichunguza. Hadithi ya Kiarabu ndiyo matini. Chanzo: HadeethEnc.com