Kutoka kwa Abuu Huraira radhi za Allah ziwe juu yake amesema: Palisemwa: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu waombee dua mbaya washirikina, akasema: "Hakika mimi sikutumwa kuwa mtoa laana, bali nilitumwa kuwa huruma".
Imepokelewa Imamu MuslimDarajaSahihi
Maelezo
Alitakwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake awaombee washirikina dua mbaya kwa Mwenyezi Mungu, akasema: Hakika mimi sikuagizwa na Mwenyezi Mungu na sikutumwa kuwa mtoa laana na kuwaombea watu kuwekwa mbali na rehema ya Mwenyezi Mungu na niwakatie heri, mimi sikutumwa kwa hayo, bali nilitumwa niwe sababu ya heri na rehema kwa watu wote, na kwa waumini hasa.
Mafunzo
Ukamilifu wa tabia zake rehema na amani ziwe juu yake.
Umuhimu wa kuusafisha ulimi kutokana na laana kwa kumuiga Mtume rehema na amani ziwe juu yake.
Hapa kuna katazo la kutoa laana.
Himizo la kuwahurumia watu.
Marejeo
صحيح مسلم (4/ 2006) (2599).
المفهم لما أشكل من تلخيص كتاب مسلم (6/ 582).
البحر المحيط الثجاج في شرح صحيح الإمام مسلم بن الحجاج (40/ 683).
Kila hadithi, daraja, maelezo na funzo hapa vinaonyeshwa kama HadeethEnc.com inavyovichapisha, kwa masharti yake ya kuchapisha upya. Daraja halimtaji aliyelitoa. Tafsiri na maelezo ni ya waandishi wake wenyewe, na baadhi hutaja hukumu; wahakiki wa Sabīl hawajavichunguza. Hadithi ya Kiarabu ndiyo matini. Chanzo: HadeethEnc.com