Ruka hadi kwenye maudhui
Hadithi zenye maelezo

Lilikuwa tandiko la Mtume rehema na amani ziwe juu yake ni kutokana na ngozi, na ndani limejazwa majani ya mitende

عَنْ عَائِشَةَ أُمِّ المُؤْمِنينَ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهَا قَالَتْ: كَانَ فِرَاشُ رَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ مِنْ أَدَمٍ، وَحَشْوُهُ مِنْ لِيفٍ، وَلِمُسلمٍ: كَانَ وِسَادَةُ رَسُولِ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ الَّتِي يَتَّكِئُ عَلَيْهَا مِنْ أَدَمٍ حَشْوُهَا لِيفٌ.
Imepokelewa kutoka kwa Aisha mama wa waumini radhi za Allah ziwe juu yake amesema: Lilikuwa tandiko la Mtume rehema na amani ziwe juu yake ni kutokana na ngozi, na ndani limejazwa majani ya mitende, na katika riwaya ya Muslim: ulikuwa mto wa Mtume rehema na amani ziwe juu yake aliokuwa akiegamia umetokana na ngozi ndani umejazwa majani.
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeDarajaSahihi
Maelezo

Ameeleza mama wa waumini Aisha radhi za Allah ziwe juu yake kuwa godoro alilokuwa akilalia Mtume rehema na amani ziwe juu yake lilikuwa limetengenezwa kwa ngozi, na limejazwa majani ya mitende, na vile vile mto wake aliokuwa akiegemea.

Mafunzo
  1. Kumebainishwa hali aliyokuwa nayo Mtume rehema na amani ziwe juu yake kama vile kuipa nyongo dunia na kuzipuuza ladha za dunia, pamnoja nakuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu alimpa uwezo wa hilo lau kama angetaka kustarehe nayo.
  2. Inafaa kutumia magodoro na mito, na kuvilalia na kuwa juu yake.
  3. Muislamu anatakiwa kuzingatia hali yake na hali ya maisha ya Nabii wake rehema na amani ziwe juu yake. Kwani yeye ndiye kiigizo chema, na kwamba mwenye kuiga nyenendo zake ataongoka na atafaulu duniani na Akhera.
  4. Kuwa na pupa ya kuiandaa Akhera, na muumini atosheke katika dunia na kile kinachomsaidia katika kumtii Mwenyezi Mungu, na asishughulike na kutafuta wingi wa mali ndani yake, na aliwakemea Mwenyezi Mungu watu, akasema: "Kumekupumbazeni kutafuta wingi (wa mali) mpaka mkayazuru makaburi" [Takathur: 1-2].
Marejeo

صحيح البخاري (8/ 97) (6456). صحيح مسلم (3/ 1650) (2082). البحر المحيط الثجاج في شرح صحيح الإمام مسلم بن الحجاج (34/ 662). إرشاد الساري لشرح صحيح البخاري (9/ 264). المفهم لما أشكل من تلخيص كتاب مسلم (5/ 403). النهاية في غريب الحديث والأثر (971).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com
Kuyasema vibaya mapenzi ya kuipenda dunia.

Kila hadithi, daraja, maelezo na funzo hapa vinaonyeshwa kama HadeethEnc.com inavyovichapisha, kwa masharti yake ya kuchapisha upya. Daraja halimtaji aliyelitoa. Tafsiri na maelezo ni ya waandishi wake wenyewe, na baadhi hutaja hukumu; wahakiki wa Sabīl hawajavichunguza. Hadithi ya Kiarabu ndiyo matini. Chanzo: HadeethEnc.com