Ruka hadi kwenye maudhui
Hadithi zenye maelezo

Kuyasema vibaya mapenzi ya kuipenda dunia.

Hadithi 20

Hakika dunia ni tamu, ni ya kijani, na hakika Mwenyezi Mungu anakumilikisheni ndani yake aone ni namna gani mtafanya, iogopeni dunia na waogopeni wanawake

عَنْ أَبِي سَعِيدٍ الْخُدْرِيِّ رضي الله عنه عَنِ النَّبِيِّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: «إِنَّ الدُّنْيَا حُلْوَةٌ خَضِرَةٌ، وَإِنَّ اللهَ مُسْتَخْلِفُكُمْ فِيهَا، فَيَنْظُرُ كَيْفَ تَعْمَلُونَ، فَاتَّقُوا الدُّنْيَا وَاتَّقُوا النِّسَاءَ، فَإِنَّ أَوَّلَ فِتْنَةِ بَنِي إِسْرَائِيلَ كَانَتْ فِي النِّسَاءِ».
imepokewaKutoka kwa Abii Saidi Al-Khudry radhi za Allah ziwe juu yake kutoka kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Hakika dunia ni tamu, ni ya kijani, na hakika Mwenyezi Mungu anakumilikisheni ndani yake aone ni namna gani mtafanya, iogopeni dunia na waogopeni wanawake, kwani hakika fitina ya kwanza ya wana wa Israeli ilikuwa kwa wanawake"
Imepokelewa Imamu MuslimDarajaSahihi
Maelezo

Anabainisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa Dunia ina ladha tamu, na ni kijani katika mandhari, hivyo mwanadamu hudanganyika nayo na kuikimbilia na kuifanya kuwa ndio hamu yake kubwa. Nakuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu amewafanya baadhi yetu kuwa warithi wa wengine katika dunia hii, ili aone ni namna gani tutafanya, je tutasimama katika utiifu wake, au maasi yake? Kisha akasema: Tahadharini sana na zisikudanganyeni starehe za Dunia na mapambo yake, zikakupelekeeni kuacha aliyokuamrisheni Mwenyezi Mungu, na kuingia katika yale aliyokukatazeni. Na miongoni mwa mambo makubwa ya wajibu kutahadhari nayo katika fitina za Dunia ni fitina ya wanawake, nakuwa ndio iliyokuwa fitina ya kwanza waliotumbukia ndani yake wana wa Israeli.

Mafunzo
  1. Himizo la kushikamana na uchamungu, na kutojishughulisha na mambo ya kidunia na pambo lake.
  2. Tahadhari ya kufitinika na wanawake, kwa kuwatazama au kujiachia kwa kuchanganyika na wanaume wa kando, au mengineyo.
  3. Fitina ya wanawake ni katika fitina kubwa katika Dunia.
  4. Kuzingatia na kuchukua mafunzo kutoka katika umma zilizotangulia, kilichotokea kwa wana wa Israeli kinaweza kutokea kwa wengine pia.
  5. Fitina ya wanawake, akiwa ni mke anaweza kumbebesha mwanaume mzigo mkubwa wa matumizi asiouweza, na akamshughulisha na kutafuta mambo ya kidunia, na akampelekea kumaliza umri wake katika kuitafuta Dunia, na akiwa ni mwanamke wa kando, anaweza kumfitini kwa kumlaghai mwanaume na kumtoa katika haki pale wanawake wakitoka na kuchanganyika pamoja na wanaume, hasa hasa wakiwa hawajisitiri kisheria, na hili linaweza kupelekea kuingia katika zinaa kwa ngazi zake, hivyo ni lazima kwa muumini kujikinga kwa Mwenyezi Mungu, na kuelekea kwake ili kusalimika na fitina za zao.
Marejeo

صحيح مسلم (4/ 2098) (2742). بهجة الناظرين شرح رياض الصالحين، لسليم الهلالي (1/ 146). كنوز رياض الصالحين، لمجموعة من الباحثين (2/ 173). نزهة المتقين شرح رياض الصالحين، لمجموعة من الباحثين (1/ 103).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Dunia ni Gereza la Muumini na ni Pepo ya Kafiri

عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رَضيَ اللهُ عنه قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: «الدُّنْيَا سِجْنُ الْمُؤْمِنِ وَجَنَّةُ الْكَافِرِ».
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira -radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amesema: Mtume -rehema na amani ziwe juu yake-: "Dunia ni Gereza la Muumini na ni Pepo ya Kafiri".
Imepokelewa Imamu MuslimDarajaSahihi
Maelezo

Ameeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake ya kwamba maisha ya Dunia kwa muumini ni kama Gereza analoishi kwa amri za kisheria, kama kufanya maamrisho na kuacha makatazo, basi akifa anapumzika na haya na anahamia katika yale aliyomuandalia Mwenyezi Mungu Mtukufu kwake, katika neema za kudumu, nayo kwa Kafiri ni kama Pepo; kwa sababu anafanya ndani yake kila inachotamani nafsi yake na kuamrishwa na matamanio yake, basi akifa anahamia katika yale aliyomuandalia Mwenyezi Mungu Mtukufu siku ya Kiyama miongoni mwa adhabu za kudumu.

Mafunzo
  1. Amesema Nawawi: Kila muumini ni mfungwa, amezuiliwa katika dunia kuyaendea matamanio yaliyoharamishwa pamoja na machukizo, amelazimishwa kufanya matendo ya utiifu na magumu, basi akifa anapumzika na haya, na anahamia katika yale aliyomuandalia Mwenyezi Mungu kwake miongoni mwa neema za kudumu, na raha halisi isiyokuwa na mapungufu, na ama Kafiri basi yeye huyamiliki hayo aliyoyapata katika starehe za dunia, pamoja nakuwa ni machache, na yamejawa tabu ziilizojaa vikwazo mbali mbali, hivyo, anapokufa anaingia katika adhabu ya kudumu, na mateso ya milele.
  2. Amesema Assanadi: Kauli yake: "Gereza la Muumini" Bila shaka hata kama ndani yake kuna neema, basi Pepo ni bora kwake kuliko hizo, "Na Pepo ya Kafiri" Basi hata kama kuna machukizo ila Moto ndio shari zaidi kwake kuliko hayo.
  3. Udhalili wa Dunia kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu.
  4. Dunia ni nyumba ya majaribu na mitihani kwa wenye imani.
  5. Kafiri ameiwahisha Pepo yake Duniani; akaadhibiwa kwa kunyimwa Pepo Akhera na neema zake.
Marejeo

صحيح مسلم (4/ 2272) (2956). بهجة الناظرين شرح رياض الصالحين، لسليم الهلالي (1/ 535). نزهة المتقين شرح رياض الصالحين، لمجموعة من الباحثين (1/ 419). شرح رياض الصالحين، لابن عثيمين (3/ 367). موسوعة فقه القلوب، لمحمد التويجري (4/ 3471). كتاب العلم، لابن عثيمين (ص37).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Laiti Dunia ingelingana na ubawa wa mbu kwa thamani yake mbele ya Allah mtukufu basi kafiri asingekunywa fundo moja la maji.

عن سهل بن سعد الساعدي ـرضي الله عنه- قَالَ رَسُول اللَّه -صَلّى اللهُ عَلَيْهِ وسَلَّم-: «لو كانت الدنيا تَعدل عند الله جَناح بَعوضة، ما سَقَى كافراً منها شَرْبَة ماء».
Kutoka kwa Sahli bin Sa'di Assaaidiy -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- Amesema Mjumbe wa Mwenyezi Mungu -Rehema na Amani ziwe juu yake-: "Laiti Dunia ingelingana na ubawa wa mbu kwa thamani yake mbele ya Allah mtukufu basi kafiri asingekunywa fundo moja la maji".
Imepokelewa na Imamu TirmidhiyDarajaSahihi
Maelezo

Katika hadithi kumebainishwa udhalili wa Dunia kwa Mwenyezi Mungu -Mtukufu- nakuwa haina thamani, na lau ingekuwa hata na thamani ndogo zaidi kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu basi asingemnywesha kafiri hata funda moja ya maji, achilia mbali kule kuneemeka kwake nayo na kustareheka na mambo yake mazuri, Hivyo ikawa dunia ni dhalili mbele ya Mwenyezi Mungu Mtukufu, tofauti na Akhera, kwani hiyo ni nyumba ya neema za kudumu kwa watu wenye imani na ni maalumu kwaajili yao kinyume na makafiri, hivyo inawapasa watu wenye imani wajue uhalisia wa hii dunia na wasiiegemee, kwani ni nyumba ya kupita na si nyumba ya kudumu, wachukue ndani yake yale yatakayowasidia Akhera ambayo ndiyo nyumba ya kudumu. Amesema Mtukufu: "Na hakuna chochote mlichopewa basi hicho ni starehe ya dunia na pambo lake, na yaliyo kwa Mwenyezi Mungu ndiyo bora na ni yenye kubakia, hivi hamzingatii, hivi kwani tuliyemuahidi ahadi nzuri naye atakutana nayo anaweza kuwa sawa na tuliyemstarehesha starehe za maisha ya dunia kisha yeye siku ya kiyama atakuwa ni miongoni mwa wenye kuhudhurishwa".

Marejeo

كنوز رياض الصالحين أ. د . حمد بن ناصر بن عبد الرحمن العمار - دار كنوز اشبيليا ـ الطبعة الأولى : 1430 هـ. بهجة الناظرين - الشيخ: سليم بن عيد الهلالي - دار ابن الجوزي. نزهة المتقين - د . مصطفى سيعد الخن، د. مصطفى البغا، محي الدين مستو، علي الشرجبي، محمد أمين لطفي، مؤسسة الرسالة ، بيروت - الطبعة الأولى : 1397 هـ 1977 م الطبعة الرابعة عشر 1407هـ 1987م. شرح رياض الصالحين - المؤلف: محمد بن صالح بن محمد العثيمين - الناشر: دار الوطن للنشر، الرياض الطبعة: 1426 هـ. رياض الصالحين د. ماهر بن ياسين الفحل - الناشر: دار ابن كثير للطباعة والنشر والتوزيع، دمشق - بيروت الطبعة: الأولى، 1428 هـ - 2007 م. صحيح مسلم- مسلم بن الحجاج القشيري النيسابوري - المحقق: محمد فؤاد عبد الباقي الناشر: دار إحياء التراث العربي - بيروت. سنن الترمذي- المؤلف: محمد بن عيسى الترمذي، أبو عيسى - تحقيق وتعليق: أحمد محمد شاكر (جـ 1، 2) ومحمد فؤاد عبد الباقي (جـ 3) وإبراهيم عطوة عوض المدرس في الأزهر الشريف (جـ 4، 5) الناشر: شركة مكتبة ومطبعة مصطفى البابي الحلبي - مصر - الطبعة: الثانية، 1395 هـ - 1975 م. صحيح وضعيف سنن الترمذي - المؤلف: محمد ناصر الدين الألباني- مصدر الكتاب: برنامج منظومة التحقيقات الحديثية - المجاني - من إنتاج مركز نور الإسلام لأبحاث القرآن والسنة بالإسكندرية تيسير الكريم الرحمن في تفسير كلام المنان - المؤلف: عبد الرحمن بن ناصر بن عبد الله السعدي - المحقق: عبد الرحمن بن معلا اللويحق - الناشر: مؤسسة الرسالة -الطبعة: الأولى 1420هـ -2000 م.

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Ewe Hakim, hakika mali hii ni kijani kibichi kitamu

عَنْ حَكِيمِ بْنِ حِزَامٍ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ قَالَ: سَأَلْتُ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ فَأَعْطَانِي، ثُمَّ سَأَلْتُهُ فَأَعْطَانِي، ثُمَّ قَالَ لِي: «يَا حَكِيمُ، إِنَّ هَذَا المَالَ خَضِرٌ حُلْوٌ، فَمَنْ أَخَذَهُ بِسَخَاوَةِ نَفْسٍ، بُورِكَ لَهُ فِيهِ، وَمَنْ أَخَذَهُ بِإِشْرَافِ نَفْسٍ لَمْ يُبَارَكْ لَهُ فِيهِ، وَكَانَ كَالَّذِي يَأْكُلُ وَلاَ يَشْبَعُ، وَاليَدُ العُلْيَا خَيْرٌ مِنَ اليَدِ السُّفْلَى»، قَالَ حَكِيمٌ: فَقُلْتُ: يَا رَسُولَ اللَّهِ، وَالَّذِي بَعَثَكَ بِالحَقِّ لاَ أَرْزَأُ أَحَدًا بَعْدَكَ شَيْئًا حَتَّى أُفَارِقَ الدُّنْيَا، فَكَانَ أَبُو بَكْرٍ يَدْعُو حَكِيمًا لِيُعْطِيَهُ العَطَاءَ، فَيَأْبَى أَنْ يَقْبَلَ مِنْهُ شَيْئًا، ثُمَّ إِنَّ عُمَرَ دَعَاهُ لِيُعْطِيَهُ، فَيَأْبَى أَنْ يَقْبَلَهُ، فَقَالَ: يَا مَعْشَرَ المُسْلِمِينَ، إِنِّي أَعْرِضُ عَلَيْهِ حَقَّهُ الَّذِي قَسَمَ اللَّهُ لَهُ مِنْ هَذَا الفَيْءِ، فَيَأْبَى أَنْ يَأْخُذَهُ. فَلَمْ يَرْزَأْ حَكِيمٌ أَحَدًا مِنَ النَّاسِ بَعْدَ النَّبِيِّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ حَتَّى تُوُفِّيَ رَحِمَهُ اللَّهُ.
Imepokelewa kutoka kwa Hakiim Bin Hizaam radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake amesema: Nilimuomba Mtume rehema na amani ziwe juu yake akanipa, kisha nikamuomba tena akanipa, kisha akasema kuniambia: "Ewe Hakim, hakika mali hii ni kijani kibichi kitamu, atakayeichukua kwa ukarimu wa nafsi, basi atabarikiwa ndani yake, na atakayeichukua kwa kujikweza hatobarikiwa ndani yake, na atakuwa sawa na yule anayekula wala hashibi, na mkono wa juu ni bora kuliko mkono wa chini", Hakim anasema: Nikasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, ninamuapa yule aliyekutuma kwa haki, sitompunguzia yeyote mali yake baada yako kamwe mpaka ntakapoondoka duniani, akawa Abubakari akimuita Hakim ili ampe chochote, akawa anakataa kupokea chochote kutoka kwake, kisha Omari alimuita ili ampe, akakataa kupokea, akasema: Enyi Waislamu, hakika mimi ninamletea haki yake ambayo Mwenyezi Mungu kamgawia katika ngawira, anakataa kuichukua. Hakim hakumuomba tena mtu yeyote baada ya Mtume rehema na amani ziwe juu yake, mpaka alipofariki Mwenyezi Mungu amrehe
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeDarajaSahihi
Maelezo

Hakim bin Hizam alimuomba Mtume rehema na amani ziwe juu yake mahitaji ya kidunia akampatia, kisha akamuomba mara nyingine akampatia, kisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake akasema kumwambia: Ewe Hakim, hakika mali hii huvutia na hupendwa sana, atakayeipata bila kuomba na akaichukua pasina kujikweza na pupa, basi atabarikiwa ndani yake, na atakayeichukua kwa pupa na tamaa ya nafsi basi hatobarikiwa ndani yake, na atakuwa kama yule anayekula wala hashibi, na mkono wa juu wenye kutoa ni bora mbele ya Mwenyezi Mungu kuliko mkono wa chini unaoomba, anasema Hakim: Nikasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, namuapa yule aliyekutuma kwa haki, sitopunguza mali ya yeyote kwa kumuomba chochote baada yako mpaka niondoke duniani. Basi akawa khalifa wa Mtume wa Mwenyezi Mungu Abubakari radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, akimuita Hakim ili ampatie sadaka, anakataa kupokea chochote, kisha kiongozi wa Waumini Omari radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake alimuita ili ampatie mali, akakataa kuchukua, basi Omari akasema: Enyi Waislamu, hakika mimi nimemletea haki yake aliyomgawia Mwenyezi Mungu kutoka katika mali ya Ngawira waliyoipata Waislamu kutoka kwa Makafiri pasina vita wala mapigano, akakataa kuichukua, Hakim hakupunguza mali ya yeyote kwa kumuomba baada ya Mtume rehema na amani ziwe juu yake, mpaka alipofariki radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake.

Mafunzo
  1. Kuchukua mali na kuikusanya kwa njia za kisheria hakupingani na kuiepuka dunia; kwa sababu kuipa mgongo dunia ni ukwasi wa nafsi na moyo kutofungamana na mali.
  2. Kumebainishwa ukubwa wa ukarimu wa Mtume rehema na amani ziwe juu yake, na kwamba alikuwa akitoa utoaji wa mtu asiyeogopa umasikini kamwe!
  3. Kutoa nasaha na kupupia katika kuwanufaisha ndugu, wakati wa kutoa msaada; kwa sababu wakati huo nafsi huwa imejiandaa kupokea maneno mazuri.
  4. Kujizuia kuwaomba watu, na kuchukia kufanya hivyo, hasa hasa panapokuwa hakuna haja.
  5. Hapa kuna ubaya wa kupupia mali na kuombaomba sana.
  6. Muombaji atakapolazimisha kuomba, hakuna tatizo kumnyima na kumfelisha, na kumpa nasaha, na kumuamrisha kujizuia kuomba, na kuacha pupa ya kutaka kuchukua.
  7. Hastahiki yeyote kuchukua chochote kutoka katika Hazina ya mali za Waislamu isipokuwa baada ya kupepwa na kiongozi, na ama kabla kuwagawanywa kwa ngawira, hastahiki pia kufanya hivyo.
  8. Inafaa kuomba kukiwa na haja.
  9. Amesema bin Hajari: Ndani ya kisa hiki nikuwa, inatakiwa kwa kiongozi kutombainishia muombaji madhara yaliyoko katika uombaji isipokuwa baada ya kukidhi haja yake ili mawaidha yake yafike mahala pake, ili asifikirie kuwa huenda hiyo ndio sababu ya kumnyima shida yake.
  10. Ubora wa Hakim radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake na kushikamana kwake na ahadi aliyomuahidi Mwenyezi Mungu na Mtume wa Mwenyezi Mungu rehema na amani ziwe juu yake.
  11. Amesema Is-haka bin Rahawaihi: Alifariki Hakim radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake ulipofikia wakati wa kufa, na hakika alikuwa amekwisha kuwa tajiri mwenye mali nyingi kuliko Makuraishi wote.
Marejeo

صحيح البخاري (4/ 5) (2750). صحيح مسلم (2/ 717) (1035). كنوز رياض الصالحين، لمجموعة من الباحثين (8/ 13). بهجة الناظرين، لسليم الهلالي (1/ 584). نزهة المتقين، لمجموعة من الباحثين (1/ 459). شرح رياض الصالحين، لابن عثيمين (3/ 386). منار القاري، لحمزة قاسم (3/ 45). المنهاج شرح صحيح مسلم، للنووي (7/ 126). إكمال المعلم بفوائد مسلم، للقاضي عياض (3/ 566).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Hakika kila umma una mtihani wake, na mtihani wa umma wangu: ni mali

عن كعب بن عياض رضي الله عنه قال: سمعت رسول الله صلى الله عليه وسلم يقول: «إن لكل أُمَّة فتنة، وفِتنة أُمَّتي: المال».
Kutoka kwa ka'bu bin Iyadh- Radhi za Allah ziwe juu yake- Amesema: Nilimsikia Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- " Akisema: "Hakika kila umma una mtihani wake, na mtihani wa umma wangu: ni mali".
Imepokelewa na Imamu Tirmidhiy - Imepokelewa na An-Nasaaiy - Imepokelewa na AhmadDarajaSahihi
Maelezo

Amesema Ka'bu bin Iyadh -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- Nilimsikia Mjumbe wa Mwenyezi Mungu -Rehema na Amani ziwe juu yake- Akisema: (Hakika kila umma una mtihani wake) Nayo ni ile wanayotahiniwa kwayo na kujaribiwa katika mambo. (Na mtihani wa Umma wangu ni mali) kwasababu ndio unaozuia ukamilifu wa kuandaa marejeo; Hivyo upuuzi hushughulisha hisia na kusimamia mambo ya utiifu na kusahau Akhera.

Marejeo

كنوز رياض الصالحين، أ.د. حمد بن ناصر بن عبد الرحمن العمار، دار كنوز اشبيليا، الطبعة الأولى : 1430 هـ. بهجة الناظرين، سليم بن عيد الهلالي، دار ابن الجوزي. نزهة المتقين، د. مصطفى سعيد الخن، د. مصطفى البغا، محي الدين مستو، علي الشرجبي، محمد أمين لطفي، مؤسسة الرسالة، بيروت، الطبعة الأولى: 1397 هـ 1977 م، الطبعة الرابعة عشر 1407 هـ 1987م. التعليقات الحسان على صحيح ابن حبان وتمييز سقيمه من صحيحه، وشاذه من محفوظه، مؤلف الأصل: محمد بن حبان أبو حاتم الدارمي البُستي، ترتيب: الأمير أبو الحسن علي بن بلبان بن عبد الله، علاء الدين الفارسي الحنفي، مؤلف التعليقات الحسان: أبو عبد الرحمن محمد ناصر الدين الألباني، الناشر: دار با وزير للنشر والتوزيع، جدة - المملكة العربية السعودية، الطبعة: الأولى، 1424 هـ - 2003 م. رياض الصالحين، د. ماهر بن ياسين الفحل، الناشر: دار ابن كثير للطباعة والنشر والتوزيع، دمشق - بيروت، الطبعة: الأولى، 1428 هـ - 2007 م. صحيح مسلم، المؤلف: مسلم بن الحجاج أبو الحسن القشيري النيسابوري، المحقق: محمد فؤاد عبد الباقي، الناشر: دار إحياء التراث العربي - بيروت. سنن الترمذي، المؤلف: محمد بن عيسى بن سَوْرة بن موسى بن الضحاك الترمذي، تحقيق وتعليق: أحمد محمد شاكر (جـ 1، 2) ومحمد فؤاد عبد الباقي (جـ 3) وإبراهيم عطوة عوض المدرس في الأزهر الشريف (جـ 4، 5)، الناشر: شركة مكتبة ومطبعة مصطفى البابي الحلبي - مصر، الطبعة: الثانية، 1395 هـ - 1975 م. صحيح وضعيف سنن الترمذي، المؤلف: محمد ناصر الدين الألباني، مصدر الكتاب: برنامج منظومة التحقيقات الحديثية - المجاني - من إنتاج مركز نور الإسلام لأبحاث القرآن والسنة بالإسكندرية. مسند الإمام أحمد بن حنبل، المؤلف: أبو عبد الله أحمد بن محمد بن حنبل بن هلال بن أسد الشيباني، المحقق: شعيب الأرناؤوط - عادل مرشد، وآخرون، إشراف: د عبد الله بن عبد المحسن التركي، الناشر: مؤسسة الرسالة، الطبعة: الأولى، 1421 هـ - 2001 م. مشكاة المصابيح، المؤلف: محمد بن عبد الله الخطيب العمري أبو عبد الله التبريزي، المحقق: محمد ناصر الدين الألباني، الناشر: المكتب الإسلامي - بيروت الطبعة: الثالثة، 1985. صحيح الجامع الصغير وزياداته، المؤلف: أبو عبد الرحمن محمد ناصر الدين الألباني، الناشر: المكتب الإسلامي.

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Ewe Mwenyezi Mungu hakuna maisha bora isipokuwa maisha ya Akhera, basi wasamehe Maanswari (watu wa Madina) na Muhajirina (waliohama kutoka kutoka Makkah)

عَنْ أَنَسِ بْنِ مَالِكٍ رَضيَ اللهُ عنه عَنِ النَّبِيِّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ أَنَّهُ قَالَ: «اللهُمَّ لَا عَيْشَ إِلَّا عَيْشُ الْآخِرَهْ، فَاغْفِرْ لِلْأَنْصَارِ وَالْمُهَاجِرَهْ».
Kutoka kwa Anasi bin Maliki radhi za Allah ziwe juu yake kutoka kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake amesema: "Ewe Mwenyezi Mungu hakuna maisha bora isipokuwa maisha ya Akhera, basi wasamehe Maanswari (watu wa Madina) na Muhajirina (waliohama kutoka kutoka Makkah)".
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeDarajaSahihi
Maelezo

Ameeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake ya kwamba hakuna maisha halisi isipokuwa maisha ya Akhera katika radhi za Mwenyezi Mungu na rehema zake na pepo yake; kwa sababu maisha ya Dunia huondoka, na maisha ya Akhera ndio ya kudumu na kubakia, kisha akawaombea msamaha na ukarimu na kutengemaa rehema na amani ziwe juu yake Maanswari wale waliompa makazi Mtume rehema na amani ziwe juu yake pamoja Muhajirina wale walioacha miji yao na mali zao wakitafuta fadhila kutoka kwa Mwenyezi Mungu na radhi zake.

Mafunzo
  1. Kutoipenda kwake Dunia rehema na amani ziwe juu yake na kuilekea kwake Akhera.
  2. Kuuepushia Mtume rehema na amani ziwe juu yake umma wake na kupenda starehe za Dunia zenye kuondoka.
  3. Kumebainishwa nafasi ya Muhajirina na Answari, kiasi kwamba walibahatika kupata dua ya Mtume rehema na amani ziwe juu yake ya kuwaombea msamaha.
  4. Mja hafurahii yale anayoyapata katika Dunia kwani huondoka upesi pamoja nakuwa na mateso makubwa, bali nyumba ya makazi ya kudumu ni Akhera.
Marejeo

صحيح البخاري (8/ 88) (6413). صحيح مسلم (3/ 1431) (1805). مرقاة المفاتيح، لعلي القاري (7/ 3016). فتح الباري شرح صحيح البخاري، لابن حجر (11/ 231). شرح رياض الصالحين، لابن عثيمين (3/ 362). كنوز رياض الصالحين، لمجموعة من الباحثين (7/ 223). بهجة الناظرين شرح رياض الصالحين، لسليم الهلالي (1/ 529). نزهة المتقين شرح رياض الصالحين، لمجموعة من الباحثين (1/ 412).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Tambueni kuwa dunia imelaaniwa, na vimelaaniwa vilivyomo, isipokuwa kumtaja Mwenyezi Mungu na yanayompendeza, na msomi, au mwanafunzi

عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رَضيَ اللهُ عنهُ سمعتُ رَسُولَ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ يقولُ: «أَلاَ إِنَّ الدُّنْيَا مَلْعُونَةٌ، مَلْعُونٌ مَا فِيهَا، إِلاَّ ذِكْرُ اللهِ وَمَا وَالاَهُ وَعَالِمٌ أَوْ مُتَعَلِّمٌ».
Imepokewa kutoka kwa Abuu Huraira radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Nilimsikia Mtume rehema na amani ziwe juu yake akisema: "Tambueni kuwa dunia imelaaniwa, na vimelaaniwa vilivyomo, isipokuwa kumtaja Mwenyezi Mungu na yanayompendeza, na msomi, au mwanafunzi".
Imepokelewa na Tirmidhi na bin MajahDarajaNi nzuri (Hasan)
Maelezo

Ameeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake ya kwamba dunia na vilivyomo inachukiwa mbele ya Mwenyezi Mungu na haipendezi bali imetengwa mbali, yameachwa yote yaliyomo hayasifiki kwa uzuri; kwakuwa dunia na vilivyomo hushughulisha na kuwatenga mbali watu na Mwenyezi Mungu Mtukufu, isipokuwa kumtaja Mwenyezi Mungu na kila kinachokaribia hilo na kuwa katika aina hiyo katika yale anayoyapenda Mwenyezi Mungu, au mwalimu wa elimu ya kisheria anayewafundisha watu, au mwenye kujifunza.

Mafunzo
  1. Haifai kuilaani dunia kwa ujumla; kwa kunukuliwa hadithi zinazokataza hilo, lakini inafaa kuyaalani yale yanayomfanya mtu kuwa mbali na Mwenyezi Mungu Mtukufu na kumshughulisha mtu na kumtii Mwenyezi Mungu.
  2. Yote yaliyomo duniani ni mchezo na ni upuuzi isipokuwa kumtaja Mwenyezi Mungu na yanayokuwa sababu na kisaidizi cha hilo.
  3. Kumebainishwa fadhila za elimu na wasomi wake na wanafunzi wake.
  4. Amesema bin Taimia: Bali husemwa vibaya yale ya haramu yaliyopatikana pasina njia nzuri, au halali iliyokuja kwa mfumo wa wingi na kujifaharisha, na yanayolimbikizwa kwa lengo la kujigamba na kujitapa, haya ndio yanayochukiwa kwa mwenye akili.
Marejeo

سنن الترمذي (4/ 151) (2322). سنن ابن ماجه (5/ 231) (4112). بهجة الناظرين شرح رياض الصالحين، لسليم الهلالي (1/ 542). نزهة المتقين شرح رياض الصالحين، لمجموعة من الباحثين (1/ 424). كنوز رياض الصالحين، لمجموعة من الباحثين (7/ 325). شرح رياض الصالحين، لابن عثيمين (3/ 374).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Lau kama ningekuwa na dhahabu kubwa mfano wa mlima Uhudi, basi ningependa zisipite siku tatu nikiwa namiliki chochote katika mali hiyo zaidi ya kile ninachokihifadhi kwaajili ya kulipa madeni

عن أبي هريرة رضي الله عنه عن رسول الله صلى الله عليه وسلم قال: «لو كان لي مِثْلُ أحدٍ ذهبًا، لسرني أن لا تمر عليَّ ثلاث ليالٍ وعندي منه شيءٌ إلا شيء أرْصُدُهُ لِدَيْنٍ».
Kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- kutoka kwa Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake-Amesema: "Lau kama ningekuwa na dhahabu kubwa mfano wa mlima Uhudi, basi ningependa zisipite siku tatu nikiwa namiliki chochote katika mali hiyo zaidi ya kile ninachokihifadhi kwaajili ya kulipa madeni".
Imepokelewa na Al-Bukhaariy na Muslim na tamko ni la BukhaariyDarajaSahihi
Maelezo

Lau kama ningekuwa ninamiliki katika mali kiasi cha dhahabu halisi kama mlima Uhudi, basi ningekitoa chote katika njia ya Mwenyezi Mungu, na nisingebakisha katika mali hiyo ila kiasi ninachokihitaji kwa kukidhi mahitaji, na kulipa madeni ninayodaiwa.

Marejeo

كنوز رياض الصالحين، أ.د. حمد بن ناصر بن عبد الرحمن العمار، دار كنوز اشبيليا، الطبعة الأولى : 1430 هـ. منار القاري شرح مختصر صحيح البخاري، المؤلف: حمزة محمد قاسم، راجعه: الشيخ عبد القادر الأرناؤوط، عني بتصحيحه ونشره: بشير محمد عيون، الناشر: مكتبة دار البيان، دمشق - الجمهورية العربية السورية، مكتبة المؤيد، الطائف - المملكة العربية السعودية عام النشر: 1410 هـ - 1990 م. نزهة المتقين، د. مصطفى سعيد الخن، د. مصطفى البغا، محي الدين مستو، علي الشرجبي، محمد أمين لطفي، مؤسسة الرسالة، بيروت، الطبعة الأولى : 1397 هـ 1977 م، الطبعة الرابعة عشر 1407 هـ 1987م. شرح رياض الصالحين، المؤلف: محمد بن صالح بن محمد العثيمين، الناشر: دار الوطن للنشر، الرياض، الطبعة: 1426 هـ. رياض الصالحين، د. ماهر بن ياسين الفحل، الناشر: دار ابن كثير للطباعة والنشر والتوزيع، دمشق - بيروت، الطبعة: الأولى، 1428 هـ - 2007 م. صحيح مسلم، المؤلف: مسلم بن الحجاج القشيري النيسابوري، المحقق: محمد فؤاد عبد الباقي، الناشر: دار إحياء التراث العربي - بيروت. صحيح البخاري، المؤلف: محمد بن إسماعيل أبو عبدالله البخاري الجعفي، المحقق: محمد زهير بن ناصر الناصر، الناشر: دار طوق النجاة (مصورة عن السلطانية بإضافة ترقيم محمد فؤاد عبد الباقي)، الطبعة: الأولى، 1422هـ.

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com
8 kati ya 20
Hadithi 20
  1. Hakika dunia ni tamu, ni ya kijani, na hakika Mwenyezi Mungu anakumilikisheni ndani yake aone ni namna gani mtafanya, iogopeni dunia na waogopeni wanawake
  2. Dunia ni Gereza la Muumini na ni Pepo ya Kafiri
  3. Laiti Dunia ingelingana na ubawa wa mbu kwa thamani yake mbele ya Allah mtukufu basi kafiri asingekunywa fundo moja la maji.
  4. Ewe Hakim, hakika mali hii ni kijani kibichi kitamu
  5. Hakika kila umma una mtihani wake, na mtihani wa umma wangu: ni mali
  6. Ewe Mwenyezi Mungu hakuna maisha bora isipokuwa maisha ya Akhera, basi wasamehe Maanswari (watu wa Madina) na Muhajirina (waliohama kutoka kutoka Makkah)
  7. Tambueni kuwa dunia imelaaniwa, na vimelaaniwa vilivyomo, isipokuwa kumtaja Mwenyezi Mungu na yanayompendeza, na msomi, au mwanafunzi
  8. Lau kama ningekuwa na dhahabu kubwa mfano wa mlima Uhudi, basi ningependa zisipite siku tatu nikiwa namiliki chochote katika mali hiyo zaidi ya kile ninachokihifadhi kwaajili ya kulipa madeni
  9. Si chochote dunia katika Akhera isipokuwa ni kama mfano wa mmoja wenu anapoweka kidole chake baharini, kisha atazame kimerudi na nini?
  10. Hakika mimi ninakuhofieni baada yangu, yale mtakayofunguliwa juu yenu katika maua ya dunia na pambo lake
  11. Yanamfuata maiti mambo matatu: familia yake na mali yake na matendo yake, vinarudi vitu viwili na kinabakia kimoja: wanarudi familia yake na mali yake, na yanabakia matendo yake
  12. Hivi leo hii nyinyi si mnapata chakula na kinywaji mkitakacho? Kwa hakika mimi nilimuona Nabii wenu rehema na amani ziwe juu yake inafika mahala hapati hata tende mbovu ya kutosha kujaza tumbo lake
  13. Lau mwanadamu angelikuwa na mabonde mawili ya mali basi angelitafuta la tatu
  14. Hakika watu wanaotumia mali ya Mwenyezi Mungu pasina haki, hao (wana adhabu ya) moto siku ya Kiyama
  15. Hakika amefaulu aliye jisalimisha, na akaruzukiwa kujizuia na kuombaomba, na Allah akamkinaisha kwa kile alichompa
  16. Msitengeze mabustani, mkajakuipenda sana dunia
  17. Nina haja gani mimi na dunia, kwani mimi katika dunia hii ni kama msafiri aliyeshuka chini ya mti kisha akaondoka akauacha
  18. Lilikuwa tandiko la Mtume rehema na amani ziwe juu yake ni kutokana na ngozi, na ndani limejazwa majani ya mitende
  19. Moyo wa mzee huendelea kuwa kijana katika mambo mawili: Katika kupenda dunia na matumaini ya muda mrefu
  20. Zidisheni sana kukikumbuka kikata ladha" Yaani: Kifo

Kila hadithi, daraja, maelezo na funzo hapa vinaonyeshwa kama HadeethEnc.com inavyovichapisha, kwa masharti yake ya kuchapisha upya. Daraja halimtaji aliyelitoa. Tafsiri na maelezo ni ya waandishi wake wenyewe, na baadhi hutaja hukumu; wahakiki wa Sabīl hawajavichunguza. Hadithi ya Kiarabu ndiyo matini. Chanzo: HadeethEnc.com